Majirani zangu wameanza kununa

Majirani zangu wameanza kununa

Sema hujakutana nao wenye roho za korosho, jirani anaziba njia ili usipitishe material yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii niliona kwa wamama flan mtaani kwetu Enzi hizo Kuna kijana kajenga na muda mfupi kanunua Gari, kufika kwake lazima anazipita nyumba za Hao kina mama ili kufika kwake, walimchimba barabara ili asipite na Gari yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya hutokea mara nyingi, japo pia mara nyingine huchangiwa na wewe mhusika. Mtu huvuna apandacho. Kauli na matendo mazuri ya mtu huilainisha mioyo hasidi. Jitahidi kujishusha, haitakugharimu. Kumbuka kumtumikia kafiri ili upate mradi wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiishi na mswahilina karibu ni taabu tupu, atatamani akuzibie hadi njia na mavituko kibao, nafikiri wanaongoza kwa fitina, roho mbaya na ma uchawi uchawi. kiujumla ngozi nyeusi tuna roho za korosho ndo maana wazungu wametupiga gepu kinooomaaaaa, maofisini ndo usiseme watu wanatamani upotee ili usikae kwenye position....
 
Mtani mbona kujenga ni kitu cha kawaida tu now days.

Unaniangusha ujue 😀
Yeah ni kawaida kujenga siku hizi lkn nashangaa ndugu yetu anatangaza ana mjengo wa vyumba vitatu kwa kisingizio cha majirani wanamuwekea ing'oo.. ila mtani tangu ligi isimamishwe atugumiani kabisa nimekumisi ujue☺
 
Good
Hata na wewe utajengaje kimasikini kwa kutegemea msaada na fadhila za wenyeji bila kuwapa chochote? Maji upewe bure! Mahali pa kuweka na kutunzia cementi upewe bure! Alafu hata kujiongeza angalau ukaenda na kilo mbili za nyama au hata 20,000 ya kushukuru hapana? Weee ndo mswahili! Alikuwa akikufadhili ulipokuwa unaonyesha bado hujajipanga! Sasa unajenga vifaaa vya mamilioni vinapita unaishia kumlisha vumbi? Weee ndo hujapevuka!
Mimi niliwahi kujenga lakini kila fadhila niliyokuwa napewa na wenyeji nilikuwa natoa mkono wa asante! Kuna siku mama mmoja nilichota maji yake yakaisha tena ya kisima cha kuchimba lakini baada ya kuyatumia nikampa 5,000 akashukuru mahusiano yakaendelea! Mimi nakuona wewe ndo mswahili unashindwa kusoma jamii unayohamia na kusema heti wanakuonea wivu! Winu gani sasa!
 
Kiukweli siku ya Jana nimedhihirisha ule usemi, kuwa majiran watakupenda wakiona mafanikio yako yapo chini,..na maisha yako Ni duni kuliko wao, ila ukiwazid kidogo Basi usitegemee ushirikiano wait Tena..

Mimi Ni kijana tu wa miaka,ya makamo..nlijichanga nikanunua mahali kiwanja..mwaka 2018.kwenye maeneo Hayo Kuna jirani ZANGU ambao nliwakuta tayari wameshajenga na wanaishi na familia zao..tulikuwa tunasalimiana vizuri mnoo..Tena walikuwa wakinikaribisha Kila wakati nnapokwenda saiti kuangalia kiwanja changu na kulimia limia sehemu penye nyasi..

Baada ya mwaka mmoja nikaanza kumwaga mawe,.kwa ajili ya kujengea msingi..ushirikiano ulikuwa Bado Ni mzuri na majirani ZANGU...nnaopakana nao..Basi mwaka huo huo 2019 nikaamua kujenga msingi..na jirani akaniambia usiwe na Shaka maji utatumia tu haya haya..Mana yeye ana kisima kikubwa Sana..na huwa kinajaa maji Kila baada ya siku mbili..

Mungu akajalia msingi wa vyumba vitatu vya kulala kimoja Ni master yangu.jiko sitting room,dinning stoo,na public toilet..ukaisha wote na kuupiga lipu.(Kuufuta kwa juu)..jirani yangu baada ya kuona huo msingi akaanza kunipiga stop kutumia kisima chake,.nikamuomba niweke maji yangu kwenye kisima hicho pia akakataa,..akaanza kuninunia yeye pamoja na mkewe

Basi nikaomba sehemu mapipa nikayajaza maji ujenzi ukaendelea..nikaleta tofali za block Basi jirani ndo akazid kuonyesha makucha yake ya chuki bila sababu..kuna mtu akaniambia ungejenga chumba kimoja angekupa maji..Hadi mwisho..ila kwa vile umejenga nyumba kubwa kuliko yeye ..hapo anahisi utampiku ndo Mana anakufanyia visa ili ushindwe kujenga nyumba hiyo.

Cha ajabu Zaidi, nlikuwa natumia chumba chake Cha nje ambayo Ni stoo yake kuwekea vifaa vyangu vya ujenzi, siku ya Jana nlipopeleka mifuko yangu ya cement kwa ajili ya kumalizia over lenta akawaambia wale watu wa gari kuwa iwekeni nje msiingize ndani Mana jirani hanisalimii vizuri, na Cha ajabu Hali ya hewa kulikuwa na mvua..wale vijana waliponipigia simu ikabidi nipande kwa haraka, nikamuuliza jirani mbona Kila siku tunasalimiana,.unasemaje sikusalimii vizuri akawa mpole akainamia chini..huyu Ni mke wa jirani yangu Mana mumewe hakuwepo hapo nyumbani.

Basi baada ya kuona hanijibu nikahamisha mifuko yangu kwa mzee mmoja ambae amejenga nyumba yake ila yeye haishi hapo

Aisee hata rafiki zako watakupenda ukiwa unalingana nao kipato,.na maisha au upo chini yao...Ila ukiwazidi tu Basi subiria kunyanyapaliwa...huku uswazi kweli shida aisee...

Sent using Jamii Forums mobile app
hao ndo watanzania mzee
 
Hata Mimi wakati najenga gorofa langu pale Osterbay, majirani zangu wakaanza kulalamika, eti kwa nini najenga gorofa wakati wao vyoo vyao ni vya uwani na pia havijaezekwa si nitakua nnawachungulia, basi kwa kua mimi hua sipendi migogoro na majirani na wao pia nikawajengea kila jirani gorofa lake,
Alisikika mmasai mmoja kutoka Bukoba anaongea hayo maneno kwenye taarifa ya habari ya BBC ile ya kiingreza achana na ile BBC ya Salumu Kikeke.
 
Nakazia... tutajuaje humu jf kama una nyumba ya vyumba vitatu kimoja master na dainingi juu!!
Mtoa Uzi tupia picha basi hapa tupate uhalisia wa unachosema!
Ila hata humu jamvini wako wengi wenye wivu! Utawagundua tu kwa comments zao!!
 
Hata na wewe utajengaje kimasikini kwa kutegemea msaada na fadhila za wenyeji bila kuwapa chochote? Maji upewe bure! Mahali pa kuweka na kutunzia cementi upewe bure! Alafu hata kujiongeza angalau ukaenda na kilo mbili za nyama au hata 20,000 ya kushukuru hapana? Weee ndo mswahili! Alikuwa akikufadhili ulipokuwa unaonyesha bado hujajipanga! Sasa unajenga vifaaa vya mamilioni vinapita unaishia kumlisha vumbi? Weee ndo hujapevuka!
Mimi niliwahi kujenga lakini kila fadhila niliyokuwa napewa na wenyeji nilikuwa natoa mkono wa asante! Kuna siku mama mmoja nilichota maji yake yakaisha tena ya kisima cha kuchimba lakini baada ya kuyatumia nikampa 5,000 akashukuru mahusiano yakaendelea! Mimi nakuona wewe ndo mswahili unashindwa kusoma jamii unayohamia na kusema heti wanakuonea wivu! Winu gani sasa!
Kuna watu wanapenda sana mteremko halafu mbaya zaiddi hawajui kujiongeza.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom