Majirani zangu wameanza kununa

Majirani zangu wameanza kununa

Unazuiwa unamwaga mbali na kuanza kusomba kwa kichwa chezea waswahili mie sina hamu, ulipofikia wewe komaa tu wasalimie tu pita zako wataona aibu tu wao wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna watu wana roho mbaya mpaka ukiwaona unawaza labda wanatokea sayari ya tofauti mana kiuhalisia mambo wanayoyafanya ni yatofauti kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mbona kawaida sana hiyo? Mimi nilifukuzwa na mwenye nyumba kisa mlo wangu uko vizuri!? Leo kuku ndizi/wali kesho rost maini kesho kutwa natoka out na shemeji yako yeye dagaa wanapishana daily.no outings Yaan Ni shida
 
Pole Sana kwa mkasa..uliowakuta
Mkuu napo nawewe bega kwa bega kwa hiki ulichokiandika
Mama angu kaanza kujenga tangia 2011 mwanzo kuna mzee tulimuamini sana na kupelekea kumpa hela zote za material lakini akawa anazifanyia mambo yake

Mama akaamua kuachana naye asa kile kitendo kilimuuma sana kwani mama alishampata fundi mwingine

Yule fundi aliteleza wakat wanapauwa walikutana na mauzauza mengi sana ikiwemo kuumwa kichwa, kuhisi uchovu na hata kunusurika kuanguka lakini walifanikiwa kupauwa

Baada ya hapo ndani kukawa kuajaa matandabui kwenye kona zote ikimaanisha kuifunga nyuma isiendelee

Daaah binadamu binadamu binadamu mbona tupo hivi

Eeeh Mungu shusha gharika

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Yani ungekuwa unaishi maeneo haya nahisi ungemuelewa huyu jirani vizuri..maji yake nliacha kuyatumia,..na salamu nikawa nawapa Kila kukicha..Sasa sijajua tatizo Ni Nini..
Umenena vyema....
Inawezekana kabisa jamaa anatumia maji mpaka wanakosa ya kutumia, na haombi radhi kwa yanaayotokea...
Majirani wanahangaika kutafuta maji siku 2 kabla kisima hakijajaa...
Inawezekana, hivyo vifaa akiweka siku ya kuchukua anasemea pembeni vifaa vyake vingine havioni...

Ajitafakari alipokosea...hakuna kama jirani ndiye ndugu yako wa kwanza..ishi naye vizuri..

Everyday is Saturday..................... 😎

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha ha ha..uchum hauko sawa kwa Sasa..biashara hazitembei Kama mwanzo..ila worry not next time..
Mkuu hongera binadamu ndo tulivyo siku zote "mtu anayekufahamu ukimwambia au akiona mafanikio yako roho ya kwanza kumjia ni roho mbaya sasa hapo ndo anahiyari yake kuipokea au kuikataa"

Ila nini mkuu fanya basi hata buku mchana upite vizuri boss

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole Sana kiongozi...
Mkuu mbona kawaida sana hiyo? Mimi nilifukuzwa na mwenye nyumba kisa mlo wangu uko vizuri!? Leo kuku ndizi/wali kesho rost maini kesho kutwa natoka out na shemeji yako yeye dagaa wanapishana daily.no outings Yaan Ni shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli siku ya Jana nimedhihirisha ule usemi, kuwa majiran watakupenda wakiona mafanikio yako yapo chini,..na maisha yako Ni duni kuliko wao, ila ukiwazid kidogo Basi usitegemee ushirikiano wait Tena..

Mimi Ni kijana tu wa miaka,ya makamo..nlijichanga nikanunua mahali kiwanja..mwaka 2018.kwenye maeneo Hayo Kuna jirani ZANGU ambao nliwakuta tayari wameshajenga na wanaishi na familia zao..tulikuwa tunasalimiana vizuri mnoo..Tena walikuwa wakinikaribisha Kila wakati nnapokwenda saiti kuangalia kiwanja changu na kulimia limia sehemu penye nyasi..

Baada ya mwaka mmoja nikaanza kumwaga mawe,.kwa ajili ya kujengea msingi..ushirikiano ulikuwa Bado Ni mzuri na majirani ZANGU...nnaopakana nao..Basi mwaka huo huo 2019 nikaamua kujenga msingi..na jirani akaniambia usiwe na Shaka maji utatumia tu haya haya..Mana yeye ana kisima kikubwa Sana..na huwa kinajaa maji Kila baada ya siku mbili..

Mungu akajalia msingi wa vyumba vitatu vya kulala kimoja Ni master yangu.jiko sitting room,dinning stoo,na public toilet..ukaisha wote na kuupiga lipu.(Kuufuta kwa juu)..jirani yangu baada ya kuona huo msingi akaanza kunipiga stop kutumia kisima chake,.nikamuomba niweke maji yangu kwenye kisima hicho pia akakataa,..akaanza kuninunia yeye pamoja na mkewe

Basi nikaomba sehemu mapipa nikayajaza maji ujenzi ukaendelea..nikaleta tofali za block Basi jirani ndo akazid kuonyesha makucha yake ya chuki bila sababu..kuna mtu akaniambia ungejenga chumba kimoja angekupa maji..Hadi mwisho..ila kwa vile umejenga nyumba kubwa kuliko yeye ..hapo anahisi utampiku ndo Mana anakufanyia visa ili ushindwe kujenga nyumba hiyo.

Cha ajabu Zaidi, nlikuwa natumia chumba chake Cha nje ambayo Ni stoo yake kuwekea vifaa vyangu vya ujenzi, siku ya Jana nlipopeleka mifuko yangu ya cement kwa ajili ya kumalizia over lenta akawaambia wale watu wa gari kuwa iwekeni nje msiingize ndani Mana jirani hanisalimii vizuri, na Cha ajabu Hali ya hewa kulikuwa na mvua..wale vijana waliponipigia simu ikabidi nipande kwa haraka, nikamuuliza jirani mbona Kila siku tunasalimiana,.unasemaje sikusalimii vizuri akawa mpole akainamia chini..huyu Ni mke wa jirani yangu Mana mumewe hakuwepo hapo nyumbani.

Basi baada ya kuona hanijibu nikahamisha mifuko yangu kwa mzee mmoja ambae amejenga nyumba yake ila yeye haishi hapo

Aisee hata rafiki zako watakupenda ukiwa unalingana nao kipato,.na maisha au upo chini yao...Ila ukiwazidi tu Basi subiria kunyanyapaliwa...huku uswazi kweli shida aisee...

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo Hali ni ya mtu na mtu, umempata jirani mbaya.katika maisha wapo watu wa aina hiyo wengi tu.

Mm ninao majirani 5, kiukweli jirani mmoja kidogo hakupendezwa na ujenzi wangu lkn sikuwa namtegemea kwa chochote ila alibadirika na kuacha kusalimia familia yangu.

Mwingine mm nilihamia kabla yy hajamalizia nyumba yake, na niliona anapata tabu ya kuhifadhi bati zake , nikamkaribisha kwangu na amehifadhi bati zake zilizobakia mpaka leo ziko kwangu zipatazo zaidi ya 50.

Kwani kwake bado hajaweka uzio. Mwingine, yy wakati najenga ukuta nilikuta yy tayari ameweka ukuta nikamuomba niuimarishe akakubali nikaweka nondo juu na kupiga zege Kisha nikaziba nyufa na kuupiga plasta.

Tunashirikiana vyema, aliyeko mbele yangu tunasalimiana kwa furaha .huyu aliyenuna, mwisho wa siku alimtuma mtu aje kwangu kuniomba atumie ukuta wangu kuweka geti, aliamini mm ntakataa.

Lkn nilimruhusu bila kikwazo. Naamini Kuna kitu kajifunza.
 
Mkuu una busara ambayo vijana wengi hawana leo hii.

Kuishi na waswahili tunahitaji busara na akili ya kujiongeza sio mbwembwe za kitoto.

Kuna wakati fulani nanmie nilikuwa na ujenzi maeneo fulani ya mamwinyi ma alwatani . Mmoja wa mzee mmoja jirani yangu inasadikika aliogopeka sana kwa uchawi.
Baada ya kufahamu hilo kabla ya kujenga nikajotambulisha kwake, nikajifanya lofa. Nikamwambia mi ni mgeni wakuja sina wazazi hivyo naomba anisimamie kama baba.

Nikaongea uongo mwingi na kumletea vizawadi kila nikija site. Vifaa vyangu nikawa nahifadhi kwake, akawa ndo baba.
Mtihani ukaja pale nimemaliza kujenga akaniambia aje kuzindika nyumba yangu. Mi si muumini wa mazindiko, nikamwambia kwa upole kuwa mi sihitaji mazindiko kwa sababu we baba upo hakuna wa kunigusa mtaa huu, na kama nitahisi kuonewa utaniona kwako .

Mzee akaona ninaimani naye sana , akacheka, akaondoka kwa kuridhika na tukaishi vizuri yeye na familia yangu. Nikisafiri nampigia simu, nikipata cha kumbebea nambebea nikirudi ananipatia mrejesho wa usalama wa familia yangu.
Mwisho alikuwa na eneo/kiwanja kizuri kimepakana na mimi mzee akagoma kukiuza kwa mtu yeyote akaniuliza kama mi nakihitaji tuandikishane nikichukue pesa nimpatie kidogokidogo.

Tukaishi vizuri japo alikuwa anasifika kwa uchawi hatari , nikawa msaada kwa wanae kuwatafutia connection maisha yakaendelea vizur
Hata na wewe utajengaje kimasikini kwa kutegemea msaada na fadhila za wenyeji bila kuwapa chochote? Maji upewe bure! Mahali pa kuweka na kutunzia cementi upewe bure! Alafu hata kujiongeza angalau ukaenda na kilo mbili za nyama au hata 20,000 ya kushukuru hapana? Weee ndo mswahili! Alikuwa akikufadhili ulipokuwa unaonyesha bado hujajipanga! Sasa unajenga vifaaa vya mamilioni vinapita unaishia kumlisha vumbi? Weee ndo hujapevuka!
Mimi niliwahi kujenga lakini kila fadhila niliyokuwa napewa na wenyeji nilikuwa natoa mkono wa asante! Kuna siku mama mmoja nilichota maji yake yakaisha tena ya kisima cha kuchimba lakini baada ya kuyatumia nikampa 5,000 akashukuru mahusiano yakaendelea! Mimi nakuona wewe ndo mswahili unashindwa kusoma jamii unayohamia na kusema heti wanakuonea wivu! Winu gani sasa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mafundi Ni wasabato wenzie..na huwa wanakutana Sana kwenye ziara za makanisa..sidhani Kama wananifanyia hivyo kwasababu ya mafund

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo ndiyo utajua wewe ni mtu wa mataifa...
Wao wanaongea lugha ingine...
Mafundi siyo watu wazuri kila neno zuri na baya wanalifikisha kwa jirani..
Sijajua umeshindwa nini mpaka sasa kumuuliza jirani kuna shida gani??

JF hatumjui jirani yako ila tunajua sasa unajenga nyumba ya aina yake...

Everyday is Saturday....................😎
 
Du kweli ulitumia saikolojia ya Hali ya juu,.hongera kwa Hilo..kiongozi
Mkuu una busara ambayo vijana wengi hawana leo hii.

Kuishi na waswahili tunahitaji busara na akili ya kujiongeza sio mbwembwe za kitoto.

Kuna wakati fulani nanmie nilikuwa na ujenzi maeneo fulani ya mamwinyi ma alwatani . Mmoja wa mzee mmoja jirani yangu inasadikika aliogopeka sana kwa uchawi.
Baada ya kufahamu hilo kabla ya kujenga nikajotambulisha kwake, nikajifanya lofa. Nikamwambia mi ni mgeni wakuja sina wazazi hivyo naomba anisimamie kama baba.

Nikaongea uongo mwingi na kumletea vizawadi kila nikija site. Vifaa vyangu nikawa nahifadhi kwake, akawa ndo baba.
Mtihani ukaja pale nimemaliza kujenga akaniambia aje kuzindika nyumba yangu. Mi si muumini wa mazindiko, nikamwambia kwa upole kuwa mi sihitaji mazindiko kwa sababu we baba upo hakuna wa kunigusa mtaa huu, na kama nitahisi kuonewa utaniona kwako .

Mzee akaona ninaimani naye sana , akacheka, akaondoka kwa kuridhika na tukaishi vizuri yeye na familia yangu. Nikisafiri nampigia simu, nikipata cha kumbebea nambebea nikirudi ananipatia mrejesho wa usalama wa familia yangu.
Mwisho alikuwa na eneo/kiwanja kizuri kimepakana na mimi mzee akagoma kukiuza kwa mtu yeyote akaniuliza kama mi nakihitaji tuandikishane nikichukue pesa nimpatie kidogokidogo.

Tukaishi vizuri japo alikuwa anasifika kwa uchawi hatari , nikawa msaada kwa wanae kuwatafutia connection maisha yakaendelea vizur

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo jirani aliyekunyima kuweka mifuko yako ya simenti ni mpare au mngoni?
 
Back
Top Bottom