Majirani zangu wameanza kununa

Majirani zangu wameanza kununa

Kiukweli siku ya Jana nimedhihirisha ule usemi, kuwa majiran watakupenda wakiona mafanikio yako yapo chini,..na maisha yako Ni duni kuliko wao, ila ukiwazid kidogo Basi usitegemee ushirikiano wait Tena..

Mimi Ni kijana tu wa miaka,ya makamo..nlijichanga nikanunua mahali kiwanja..mwaka 2018.kwenye maeneo Hayo Kuna jirani ZANGU ambao nliwakuta tayari wameshajenga na wanaishi na familia zao..tulikuwa tunasalimiana vizuri mnoo..Tena walikuwa wakinikaribisha Kila wakati nnapokwenda saiti kuangalia kiwanja changu na kulimia limia sehemu penye nyasi..

Baada ya mwaka mmoja nikaanza kumwaga mawe,.kwa ajili ya kujengea msingi..ushirikiano ulikuwa Bado Ni mzuri na majirani ZANGU...nnaopakana nao..Basi mwaka huo huo 2019 nikaamua kujenga msingi..na jirani akaniambia usiwe na Shaka maji utatumia tu haya haya..Mana yeye ana kisima kikubwa Sana..na huwa kinajaa maji Kila baada ya siku mbili..

Mungu akajalia msingi wa vyumba vitatu vya kulala kimoja Ni master yangu.jiko sitting room,dinning stoo,na public toilet..ukaisha wote na kuupiga lipu.(Kuufuta kwa juu)..jirani yangu baada ya kuona huo msingi akaanza kunipiga stop kutumia kisima chake,.nikamuomba niweke maji yangu kwenye kisima hicho pia akakataa,..akaanza kuninunia yeye pamoja na mkewe

Basi nikaomba sehemu mapipa nikayajaza maji ujenzi ukaendelea..nikaleta tofali za block Basi jirani ndo akazid kuonyesha makucha yake ya chuki bila sababu..kuna mtu akaniambia ungejenga chumba kimoja angekupa maji..Hadi mwisho..ila kwa vile umejenga nyumba kubwa kuliko yeye ..hapo anahisi utampiku ndo Mana anakufanyia visa ili ushindwe kujenga nyumba hiyo.

Cha ajabu Zaidi, nlikuwa natumia chumba chake Cha nje ambayo Ni stoo yake kuwekea vifaa vyangu vya ujenzi, siku ya Jana nlipopeleka mifuko yangu ya cement kwa ajili ya kumalizia over lenta akawaambia wale watu wa gari kuwa iwekeni nje msiingize ndani Mana jirani hanisalimii vizuri, na Cha ajabu Hali ya hewa kulikuwa na mvua..wale vijana waliponipigia simu ikabidi nipande kwa haraka, nikamuuliza jirani mbona Kila siku tunasalimiana,.unasemaje sikusalimii vizuri akawa mpole akainamia chini..huyu Ni mke wa jirani yangu Mana mumewe hakuwepo hapo nyumbani.

Basi baada ya kuona hanijibu nikahamisha mifuko yangu kwa mzee mmoja ambae amejenga nyumba yake ila yeye haishi hapo

Aisee hata rafiki zako watakupenda ukiwa unalingana nao kipato,.na maisha au upo chini yao...Ila ukiwazidi tu Basi subiria kunyanyapaliwa...huku uswazi kweli shida aisee...

Sent using Jamii Forums mobile app
Yawezekana ni mtazamo wako ndio tatizo.
 
Hata na wewe utajengaje kimasikini kwa kutegemea msaada na fadhila za wenyeji bila kuwapa chochote? Maji upewe bure! Mahali pa kuweka na kutunzia cementi upewe bure! Alafu hata kujiongeza angalau ukaenda na kilo mbili za nyama au hata 20,000 ya kushukuru hapana? Weee ndo mswahili! Alikuwa akikufadhili ulipokuwa unaonyesha bado hujajipanga! Sasa unajenga vifaaa vya mamilioni vinapita unaishia kumlisha vumbi? Weee ndo hujapevuka!
Mimi niliwahi kujenga lakini kila fadhila niliyokuwa napewa na wenyeji nilikuwa natoa mkono wa asante! Kuna siku mama mmoja nilichota maji yake yakaisha tena ya kisima cha kuchimba lakini baada ya kuyatumia nikampa 5,000 akashukuru mahusiano yakaendelea! Mimi nakuona wewe ndo mswahili unashindwa kusoma jamii unayohamia na kusema heti wanakuonea wivu! Winu gani sasa!
Una point hapa kubwa sana
 
Mkuu napo nawewe bega kwa bega kwa hiki ulichokiandika
Mama angu kaanza kujenga tangia 2011 mwanzo kuna mzee tulimuamini sana na kupelekea kumpa hela zote za material lakini akawa anazifanyia mambo yake

Mama akaamua kuachana naye asa kile kitendo kilimuuma sana kwani mama alishampata fundi mwingine

Yule fundi aliteleza wakat wanapauwa walikutana na mauzauza mengi sana ikiwemo kuumwa kichwa, kuhisi uchovu na hata kunusurika kuanguka lakini walifanikiwa kupauwa

Baada ya hapo ndani kukawa kuajaa matandabui kwenye kona zote ikimaanisha kuifunga nyuma isiendelee

Daaah binadamu binadamu binadamu mbona tupo hivi

Eeeh Mungu shusha gharika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata na wewe utajengaje kimasikini kwa kutegemea msaada na fadhila za wenyeji bila kuwapa chochote? Maji upewe bure! Mahali pa kuweka na kutunzia cementi upewe bure! Alafu hata kujiongeza angalau ukaenda na kilo mbili za nyama au hata 20,000 ya kushukuru hapana? Weee ndo mswahili! Alikuwa akikufadhili ulipokuwa unaonyesha bado hujajipanga! Sasa unajenga vifaaa vya mamilioni vinapita unaishia kumlisha vumbi? Weee ndo hujapevuka!
Mimi niliwahi kujenga lakini kila fadhila niliyokuwa napewa na wenyeji nilikuwa natoa mkono wa asante! Kuna siku mama mmoja nilichota maji yake yakaisha tena ya kisima cha kuchimba lakini baada ya kuyatumia nikampa 5,000 akashukuru mahusiano yakaendelea! Mimi nakuona wewe ndo mswahili unashindwa kusoma jamii unayohamia na kusema heti wanakuonea wivu! Winu gani sasa!
Umenena vyema....
Inawezekana kabisa jamaa anatumia maji mpaka wanakosa ya kutumia, na haombi radhi kwa yanaayotokea...
Majirani wanahangaika kutafuta maji siku 2 kabla kisima hakijajaa...
Inawezekana, hivyo vifaa akiweka siku ya kuchukua anasemea pembeni vifaa vyake vingine havioni...

Ajitafakari alipokosea...hakuna kama jirani ndiye ndugu yako wa kwanza..ishi naye vizuri..

Everyday is Saturday..................... 😎
 
Jichunguze kwanza huenda tatizo limeanzia kwako,, huenda na wewe ni aina ya wale wakipata zaidi kidogo huwa wanawaona wengine mavi,,
Maisha ni haya haya huitaji kujiona bora zaidi ya binadamu wengine,,
Ila binafsi watu kama hao huwa nawachukulia simple pasi na kumuonesha tofauti yoyote namuacha akafie mbele huko na dharau zake,,
Mafundi ni watu wenye ustaarabu hafifu. Usipokuwa makini wanakugombanisha na majirani bure.
 
Mkuu hongera binadamu ndo tulivyo siku zote "mtu anayekufahamu ukimwambia au akiona mafanikio yako roho ya kwanza kumjia ni roho mbaya sasa hapo ndo anahiyari yake kuipokea au kuikataa"

Ila nini mkuu fanya basi hata buku mchana upite vizuri boss

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe!!nilidhan ni kitaa chetu tu,mpaka nakiitaga kiwanja kilichokuwa kinafanyiwa mikutano Na wachawi

mwongo atofautiani Na mchawi
 
Back
Top Bottom