Majirani wanamcheka mpenzi wangu

Majirani wanamcheka mpenzi wangu

Mapenz ni hisia juu ya mtu husika so kama unampenda na kumthamin huna haja ya kuona aibu wanavyomcheka mpenzio amin kuna cku hao hao watakusifu na huyo mpenzio na wataona wivu kabisa believe me my sister
We ni mmalila au jina tu mkuu?
 
Lucz usipate tabu sana, huyo jamaa yako bado anatafuta na ipo siku atapata mtaji wake na atafanya shughuri zake na atakuwa mtanashati.

Hii imenikumbusha yule jamaa aliyekuja humu akidai mpenzi wake anamcheka eti kisa anavaa minguo kama kwaya masta.
Jambo lingine kwa kuwa unampenda mshauri kama kuna kiasi chochote cha pesa mfunue biashara yenu maana mabosi nao si watu wazuri hasa hwa wanaoajili watu madukani hujipenda wao tu.

Jambo lingine amabalo nahisi huyu jamaa yako hamuendani aidha ki imri, mwonekano na hata kitabia ndio maana marafiki wanapomwona humkejeli.
Anyways unapaswa kuangalia kipi kinafiti moyo wako kwa raha zako mwenyewe
 
Poleni na mihangaiko wana JF.

Naomba ushauri nifanyeje hapa nilipopanga majirani zangu wanamcheka mpenzi wangu walikuwa ndani wakicheka huku housegirl akiwa mlangoni nikaona housegirl naye anacheka huku akijibu eeh kaja aliponiona mimi akafunga mlango.

Mimi nilihisi wanacheka jinsi anavyo vaa siku za kazi. Kuanzia nguo hadi viatu upande wa viatu anavaa malapa ni kama ya kuogea sio kuvaa kwenda mjini. Upande wa mashati mara yamepauka au kua na tobo kabisa.

Mimi ni mtumishi serikalini yeye anauza duka la ndugu yake na kukaa kwa ndugu yake anadai ni kaka yake. Mimi pia kwa upande wangu nilishamuonya juu ya huo uvaaji kwa sababu nipo njiani na watumishi wenzangu nikikutana nae napita kama simjui yaani nashindwa hata kumtambulisha kuwa huyu ni shemeji yenu.

Wakati tunaanza mahusiano nilimpenda sana kiasi kwamba nikachukua hela kidogo nikaenda kumnunulia shati na tishirt nikampa hakuyachukua mpaka nilipo mlazimisha na hajawahi kuvaa hata siku moja. Mimi nilichohisi huko anakokaa wanamkataza kuvaa nguo ambayo hajanunuliwa nikamuuliza kwa nini havai hakunipa sababu inayoeleweka.

Ila siku za jumapili huvaa nguo nzuri na viatu vizuri hupendeza sana hadi nafurahi. Kuna kipindi nikaamua awe anakuja jumapili tu. Kumpenda nampenda lakini nashindwa nifanyeje kuhusu hili.
sikujua km leo nikacheka hivi l
 
UMENIKUMBUSHA MBALI KDOGO MLETA MADA....tukiwa chuo mwaka 2012, nilibahatka kumpata mwenzi wa uchumba, nikampa mtego huo wa kujiweka rafu kimavaz kila awapo yeye(hakuwa mwanachuo)..alipopata fursa ya kwenda CHUO CHA UKUTUBI akawa hatak nimsogelee akiwa na marafki zake...nkajua hana ule UCHUMBA WA KUJIDHABIHU.....
ushauri kwenu, punguzeni UCHUMBA WA KIBONGO MOVIE...nendeni kwenye uhalisia
 
Nguo zilizo chanika tena?Huyu kweli gagulo lake halitoi uvundo mkuu?

Sidhani kama anafua chupi huyu ehehehe
 
Nguo zilizo chanika tena?Huyu kweli gagulo lake halitoi uvundo mkuu?

Sidhani kama anafua chupi huyu ehehehe
Mara zote mnatuona wanawake wachafu......huyo ni mwanaume na aliyeleta malalamiko ni mwanamke........
 
Poleni na mihangaiko wana JF.

Naomba ushauri nifanyeje hapa nilipopanga majirani zangu wanamcheka mpenzi wangu walikuwa ndani wakicheka huku housegirl akiwa mlangoni nikaona housegirl naye anacheka huku akijibu eeh kaja aliponiona mimi akafunga mlango.

Mimi nilihisi wanacheka jinsi anavyo vaa siku za kazi. Kuanzia nguo hadi viatu upande wa viatu anavaa malapa ni kama ya kuogea sio kuvaa kwenda mjini. Upande wa mashati mara yamepauka au kua na tobo kabisa.

Mimi ni mtumishi serikalini yeye anauza duka la ndugu yake na kukaa kwa ndugu yake anadai ni kaka yake. Mimi pia kwa upande wangu nilishamuonya juu ya huo uvaaji kwa sababu nipo njiani na watumishi wenzangu nikikutana nae napita kama simjui yaani nashindwa hata kumtambulisha kuwa huyu ni shemeji yenu.

Wakati tunaanza mahusiano nilimpenda sana kiasi kwamba nikachukua hela kidogo nikaenda kumnunulia shati na tishirt nikampa hakuyachukua mpaka nilipo mlazimisha na hajawahi kuvaa hata siku moja. Mimi nilichohisi huko anakokaa wanamkataza kuvaa nguo ambayo hajanunuliwa nikamuuliza kwa nini havai hakunipa sababu inayoeleweka.

Ila siku za jumapili huvaa nguo nzuri na viatu vizuri hupendeza sana hadi nafurahi. Kuna kipindi nikaamua awe anakuja jumapili tu. Kumpenda nampenda lakini nashindwa nifanyeje kuhusu hili.
Ata usiumie moyo. Ilimradi moyo wako umeridhika kuwa na amani. Huyo ni mpenzi wako sio mpenzi wa majirani zako. Be ureself. Yawezekana wao wanamcheka lakini hawajui kaka/ baba wa watu kabeba nin. Pengine wanaona hana hela lakini hawajui hela inapatokana duniani. Leo wanamcheka kesho watapatwa na shida na pengine watashindwa ata sehemu ya kukopa hale mwisho wa siku watakuja kwakwo. Mbona kwenye jamii yanatokea sanaa tu. Mtu anakipato kikubwa na akipata shida anaenda kwa mwenye kipata kidogo. Ushauri wangu ni " sikiliza moyo wako unataka nini"
 
mbona mimi naenda kwa mupenzi nikiwa na kanda2 tena zimechoka mbaya usipime yani ila mwenyewe tu ananipenda nilivyo.
 
as long as unampenda wacheke mpaka waache wenyewe,huwezi kuwaridhisha binadamu hata siku moja....
 
Mara zote mnatuona wanawake wachafu......huyo ni mwanaume na aliyeleta malalamiko ni mwanamke........
Hapana sijawahi waona wanawake wachafu,lkn hii imezidi dada yaani hadi ndala zimekatika ehehehehe
 
Dawa ni kuwafungia vioo.

Mwishoni watakuja jiona wapumbavu
 
Back
Top Bottom