Chama Cha NCCR-Mageuzi, juzi kimeuteka mji wa Kahama, mkoani Shinyanga na kufanikiwa kuzoa wanachama wapya 220 kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wanachama hao walijiunga na Chama hicho katika mkutano wa hadhara ambao ni mwendelezo wa operesheni ya "Uzalendo amka Kahama" uliofanyika katika Kata za Basoka na Mwendakulima.
Operesheni hiyo imelenga kuwazindua wakazi wa kahama wajue misingi ya kudai haki zao bila kupoteza uhai wao, kujihadhari na baadhi ya wanasiasa ambao wako tayari kusababisha machafuko ili wafanikishe malengo yao.
Akihutubia Mkutano huo, katibu wa Habari na Uenezi wa Chama hicho Taifa, Kitengo cha Vijana, Bw.Deogratius Kisandu aliwataka vijana wasikubali kutumika kisiasa kwa manufaa ya vyama bali watangulize masilahi ya Taifa.
Alisema wanachama hao kutoka CHADEMA, waliamua kukihama chama hicho kutokana na mwenendo usioridhisha ambapo kati ya wanachama hao 98 wametokea katika Kata hizo ambapo 122 wametokea Mjini Kahama.