MAJIRA: NCCR waibomoa CHADEMA

MAJIRA: NCCR waibomoa CHADEMA

Kama CHADEMA INAWEZA KUPOKONYWA wanachama 220 kwa kahama tu hii ni kwamba chadema itakuwa na wanachama wengi zaidi ya vyama vingine.
 
haya yote ndio siasa kwa hiyo hakuna cha kushangaa.
siasa ni ushawishi
siasa ni nguvu
siasa ni majadiliano na muafaka..........
 
Hakuna hata nyinyiem mmoja? Kweli kazi ya kukibomoa CHADEMA Kisandu anaijua. Yaani hotuba iliwagusa wanachama wa CDM tu, hakuna UDP, TLP!!!
 
Ndio kazi alotumwa Mbatia baada ya kupewa ubunge wa viti masking. Tulitegemea hilo. Another ccmb.
 
Hivi inakuwaje watu 200 ni kuzoa? mi nilifikiri labda imezoa watu 1000 n akuendelea kumbe watu 200 tu
 
CHADEMA wala msitukane sana katika hili, maana huo ndio mchezo wenu wa kawaida. Mwaka 2007 mlichukua sana wanachama wa NCCR mkiwambia kuwa vyama vimeungana na wote inabidi wahamie kwenu. Pili, mlipitisha uzushi mikoani kwamba NCCR imefutiwa usajili. Tatu, mmewachukua viongozi wengi wa kitaifa wa NCCR kwa lengo la kutumaliza. Mlimchukua muasisi wa chama Mabere Marando, Mkamchukua Marehemu Chacha Wangwe, mkamkwapua Prof. Mwesiga Baregu, Mhe. Tundu Lissu, Mhe. John Mnyika, Mhe. Chiku Abwao, Mhe. Joseph Selasini, na wengine wengi. Hivi juzi tu mkamchukua aliyekuwa naibu katibu Mkuu Laurent Tara.
Yale yale, ya mkuki kwa nguruwe ...?
 
kisandu acha kupotosha umma mkutano ulikuwa na watu hata thelathini hawafiki
 
Chama Cha NCCR-Mageuzi, juzi kimeuteka mji wa Kahama, mkoani Shinyanga na kufanikiwa kuzoa wanachama wapya 220 kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wanachama hao walijiunga na Chama hicho katika mkutano wa hadhara ambao ni mwendelezo wa operesheni ya "Uzalendo amka Kahama" uliofanyika katika Kata za Basoka na Mwendakulima.

Operesheni hiyo imelenga kuwazindua wakazi wa kahama wajue misingi ya kudai haki zao bila kupoteza uhai wao, kujihadhari na baadhi ya wanasiasa ambao wako tayari kusababisha machafuko ili wafanikishe malengo yao.

Akihutubia Mkutano huo, katibu wa Habari na Uenezi wa Chama hicho Taifa, Kitengo cha Vijana, Bw.Deogratius Kisandu aliwataka vijana wasikubali kutumika kisiasa kwa manufaa ya vyama bali watangulize masilahi ya Taifa.

Alisema wanachama hao kutoka CHADEMA, waliamua kukihama chama hicho kutokana na mwenendo usioridhisha ambapo kati ya wanachama hao 98 wametokea katika Kata hizo ambapo 122 wametokea Mjini Kahama.
It is so interesting,yaani hata CCM mmoja hawakumpata,kwa hiyo lengo lao ni kubomoa CHADEMA sio CCM.Mimi nilidhani kama lengo ni kutwaa nchi basi target ingekuwa ni CCM na sio kujivuna kwa kuibomoa CHADEMA,ili iweje?miyopic thinking.
 
Chama Cha NCCR-Mageuzi, juzi kimeuteka mji wa Kahama, mkoani Shinyanga na kufanikiwa kuzoa wanachama wapya 220 kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wanachama hao walijiunga na Chama hicho katika mkutano wa hadhara ambao ni mwendelezo wa operesheni ya "Uzalendo amka Kahama" uliofanyika katika Kata za Basoka na Mwendakulima.

Operesheni hiyo imelenga kuwazindua wakazi wa kahama wajue misingi ya kudai haki zao bila kupoteza uhai wao, kujihadhari na baadhi ya wanasiasa ambao wako tayari kusababisha machafuko ili wafanikishe malengo yao.

Akihutubia Mkutano huo, katibu wa Habari na Uenezi wa Chama hicho Taifa, Kitengo cha Vijana, Bw.Deogratius Kisandu aliwataka vijana wasikubali kutumika kisiasa kwa manufaa ya vyama bali watangulize masilahi ya Taifa.

Alisema wanachama hao kutoka CHADEMA, waliamua kukihama chama hicho kutokana na mwenendo usioridhisha ambapo kati ya wanachama hao 98 wametokea katika Kata hizo ambapo 122 wametokea Mjini Kahama.

We kweli farasi kama Id yako ilivyo yaani ina maana wooote hao 200 sijui wametoka Chadema tu hamna waliotoka ccm,nccr mageuzi au chama chochote isipokuwa Chadema?

Hamtalala mwaka huu make usingizi hampati kila wakati ni kuwafikiria Chadema tu safari hii hadi mbebe mimba tu hamponi make sasa hamfanyi kazi zenu ni kuwachochea Chadema kuwasingizia ugaidi,mtafanya yoooote mwisho mtaacha tu
 
Chama Cha NCCR-Mageuzi, juzi kimeuteka mji wa Kahama, mkoani Shinyanga na kufanikiwa kuzoa wanachama wapya 220 kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wanachama hao walijiunga na Chama hicho katika mkutano wa hadhara ambao ni mwendelezo wa operesheni ya "Uzalendo amka Kahama" uliofanyika katika Kata za Basoka na Mwendakulima.

Operesheni hiyo imelenga kuwazindua wakazi wa kahama wajue misingi ya kudai haki zao bila kupoteza uhai wao, kujihadhari na baadhi ya wanasiasa ambao wako tayari kusababisha machafuko ili wafanikishe malengo yao.

Akihutubia Mkutano huo, katibu wa Habari na Uenezi wa Chama hicho Taifa, Kitengo cha Vijana, Bw.Deogratius Kisandu aliwataka vijana wasikubali kutumika kisiasa kwa manufaa ya vyama bali watangulize masilahi ya Taifa.

Alisema wanachama hao kutoka CHADEMA, waliamua kukihama chama hicho kutokana na mwenendo usioridhisha ambapo kati ya wanachama hao 98 wametokea katika Kata hizo ambapo 122 wametokea Mjini Kahama.
Sijawahi kusikia kitu kama hiki, kumbe KAHAMA yote ni CHADEMA! Haki ya Mungu, kama hivyo CDM wamefanya kazi maana ni chama pekee mahali hapo, sasa NCCR ni ya pili. Kifupi haiji kichwani kuwa waliojiunga na NCCR wametoka wote CHADEMA, kuna marafiki zangu 35 nawajua walikuwa CCM na wengi walikuwa hawana Chama chochote kati ya hao waliojiunga. Kauli ya kuzuia vijana kutumika kisiasa inachekesha maana hata huyo aliyetoa kauli hiyo anatumika kisiasa na amekuwa hapo kisiasa, hivyo kuna ubaya gani vijana kutumika kisiasa? Kuna wakati tuwe wakweli jamani, kila mtu anatumika kisiasa ili kufanikisha malengo ya kisiasa yaani ya kuchukua dola na kuendeleza nchi, ni kutokuelewa maana ya haya yote kwa kiongozi kusema vijana wasitumike kiisiasa, ni nani atawatumia kiuchumi bila kufikia malengo ya kisiasa?
 
Hakuna hata nyinyiem mmoja? Kweli kazi ya kukibomoa CHADEMA Kisandu anaijua. Yaani hotuba iliwagusa wanachama wa CDM tu, hakuna UDP, TLP!!!

:nono: Inawezekana alipofika alitangaza kuwa yeye yuko pale kwa ajili ya kuchukua wafuasi wa CDM na wala hana shida, na tena hataki wafuasi wa vyama vingine kwani tayari ni ndugu na wanafanya kazi pamoja. Alitangaza adui wao ni mmoja tu anayepaswa kushughulikiwa naye ni CDM. Yamkini ndiyo maana alivuna hao watu. :nono:
 
Kwa hiyo nccr wanawataka kuwakomboa watanzania kutoka kwa nani? au sielewi maana ya ukombozi? Je hiyo kata wanachama ni chadema tu hakuna vyama vingine?

Mkuu sasa hiyo si ndo ile njia ya mwongo ni fupi? Afu sikujua ukombozi kutoka mikononi mwa CHADEMA kumbe siku hizi CHADEMA ndo wenye dola kwi kwi...
 
Uongo mbaya sana,niko hapa Kagongwa kata Isagehe wilaya ya Kahama,huyu bwana anamkutano ,watu hawafiki 20,wengi ni watoto.Sasa hao 220 walitoka wapi?nina uhakika,NCCR hawana wanachama wanaofika 200 katka wilaya hii.Nimejaribu kuchukua picha lakini wamenizonga.
 
Ha ha ha! Kweli Uongo mbaya, watoto wamekuzonga hawataki kupigwa picha!
 
Sijawahi kusikia kitu kama hiki, kumbe KAHAMA yote ni CHADEMA! Haki ya Mungu, kama hivyo CDM wamefanya kazi maana ni chama pekee mahali hapo, sasa NCCR ni ya pili. Kifupi haiji kichwani kuwa waliojiunga na NCCR wametoka wote CHADEMA, kuna marafiki zangu 35 nawajua walikuwa CCM na wengi walikuwa hawana Chama chochote kati ya hao waliojiunga. Kauli ya kuzuia vijana kutumika kisiasa inachekesha maana hata huyo aliyetoa kauli hiyo anatumika kisiasa na amekuwa hapo kisiasa, hivyo kuna ubaya gani vijana kutumika kisiasa? Kuna wakati tuwe wakweli jamani, kila mtu anatumika kisiasa ili kufanikisha malengo ya kisiasa yaani ya kuchukua dola na kuendeleza nchi, ni kutokuelewa maana ya haya yote kwa kiongozi kusema vijana wasitumike kiisiasa, ni nani atawatumia kiuchumi bila kufikia malengo ya kisiasa?
Asante kwa kuthibitisha kwamba kweli kuna wanachama wapya wamejuinga na NCCR hapo Kahama.

Nadhani kutumika kisiasa kunakotajwa na Kisandu, ni pale ambapo watu fulani kwa maslahi yao binafsi ndani ya siasa, wanawatumia vijana hata kufanya mambo maovu. Chukulia mfano wa sakata la Bukoba Boy, kuna vijana wametumika ndivyo sivyo. Mmoja wao yuko lupango sasa, waliomtumia kufanikisha mambo yao hawajamwekea hata wakili wa kumtetea.
 
Back
Top Bottom