Majipu Arusha Technical Colege

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,522
7,030
Lini Dr. Magufuli rais wetu mpendwa utaitembelea chuo cha ufundi Arusha? Kuna ufisadi wa kutisha. Mkuu wa chuo ana PhD feki, amenunua vyombo vya serikali ikiwamo Takukuru. Jengo la km Tshs. 3 Billion lajengwa kwa Tshs. 7 Billion. Mkuu wake Dr.(feki) Richard J. Masika adai hakuna wa kumgusa serikalini. Ameinunua bodi yote. Amefukuza viongozi wa academic staff association na wa THTU. Serikali ituambie atawatesa hawa wasomi na kuiibia serikali mpaka lini?
 
Taarifa yako hebu ipe nyama sawa sawa. Kuna mengi hayapo vizuri. Vinginevyo itakuwa majungu.
 
Kwa ufupi ni kwamba chuo hiki kimekuwa kikituhumiwa kwa muda mrefu kuhusu ufisadi katika maeneo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa ghorofa tatu, kufukuza viongozi wa jumuiya ya kitaaluma (academic staff association), viongozi wa THTU, mkuu wa chuo kuitumia bodi kwa maslahi yake, mwenyekiti wa bodi kukaa muda mrefu pamoja na kwamba hana sifa kuiongoza taasisi kubwa km hii. nafasi za kazi kwa upendeleo wa kikabila. mambo mengi yameandikiwa ofisi mbalimbali za serikali tangia mwaka 2012. wafanyakazi walishabahatika kuandika kupitia gazeti la raia mwema. baadaye tunaambiwa mkuu wa chuo (Dr. Richard Masika) amemnunua mhariri mtendaji wa gazeti hilo na baada ya hapo kweli mhariri alikataa kuandika tuhuma hizo za kifisadi pamoja na kwamba zimejaa ushahidi. wafanyakazi tumekosa pa kupaza sauti zetu. Tunamuomba Mh. Rais kupitia jukwaa hili atume timu yake kufuatilia ukweli hatimaye asaidie kutumbua haya majipu.
 
Majungu majungu wacha kumtuhumu bure baba Wa watu Dr.Masika ni mchapakaz na anajituma ..Utakua na maslah binafsi tu ww
 
Majungu majungu wacha kumtuhumu bure baba Wa watu Dr.Masika ni mchapakaz na anajituma ..Utakua na maslah binafsi tu ww
Yawezekana anajituma na kuchapakazi katika ufisadi. Wapo wengi wana sifa kedekede lakini kwa kupiga madili ndio wenyewe. Mzee wahenga walilonga, uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti. Huyu Bwana anamtuhumu Dk. Masika kwa kufisidi. Hili jukwaa lina watu wengi wanapitia. Unaweza kumtetea mtu kesho akatumbuliwa, sijui utasemaje.
Natumai taarifa zake zimefika na wahusika wameziona. Kama kuna watu wanaweza kufunguka zaidi itasaidia sana kuweza kufichua uovu wa hapo chuoni kwa kuwa sote tunajua serikali iliyopita jinsi ilivyokuwa. Tuliimbishwa sana uzuri wake lakini movie inayoendelea hatujui nani atasalimika.
 
Back
Top Bottom