Majini & Mapepo πŸ‘»πŸ€”

Mjadala mtamu sana huu , kuna kipindi fulani nilikutana na Mama mmoja ni Shahidi wa Yehova aliniambia mengi sana, kwa sababu nina wenge la uchovu Acha kwanza nitulie nikiwa timamu nitarejea, lakini mleta uzi kumbuka tunaishi kwa kanuni ila kupatikane usawa.

 
Pamoja na kitabu binafsi Naamini katika Nguvu Kubwa na ya ajabu pamoja na chanzo cha uumbaji wa vyote ninavyoviona na ninavyovihisi.
Chanzo cha uumbaji kinaweza kuwepo ila hizi hadithi za kwenye vitabu

Watu wahataki zihojiwe kama ulivyo ni quote kua Mungu hachunguziki?
 
Kwani hujui kule kanisani mapepo huwabamiza chini bila huruma.

Kwa mfano, kuna mama mmoja hapa jirani anamakovu mwili mzima kwa sababu ya kukatwa mitama na pepo.

Yaani, pepo anakukata mtama na hajali kama utaangukia kiti ama la! πŸ₯²
Hivi wewe kwanini lakini πŸ˜…πŸ˜…
 
Una hakika kama kweli Mungu yupo?
Hicho kitabu unachotumia unaamini ni maneno yale au ni tungo za watu?
Mungu yupo ! Angalia uumbaji unaoonekane , Anga halina nguzo na limesimama, Milima, bahari wote huo ni uumbaji wa asili kuonesha kwamba kuna muumbaji ukiachana na fiction za Wanasayansi.

Ni sawa na wewe unapoenda dukani kununua simu , je hiyo simu ikiharibika si huwa unaipeleka ulipoonunua au kwa fundi ?
 
Mapepo yapo ndugu mtoa mada, na yanafanya kazi haswa, huwezi kuyaona kwa macho ya kawaida ni invisibles
 
Kwenye uumbaji ubaya alitaka uwepo au hakutaka? Maana inasound kama lili shambulio la ghafla
 
Kwahiyo, unasema Mungu hakuumba kiumbe kikiwa kibaya, bali original ya kila kiumbe ni chema

Sasa Je, Mungu hakujua kwamba viumbe hawa wema baadaye wangebadilika na kuwa waovu? Kama alijua, kwa nini hakuzuia hilo lisitokee?

Au nayo ilikuwa sehemu ya mpango wake?
 
Chanzo cha uumbaji kinaweza kuwepo ila hizi hadithi za kwenye vitabu

Watu wahataki zihojiwe kama ulivyo ni quote kua Mungu hachunguziki?
Sipingani na wewe pengine majina tuu but I think even you can sense the awareness of that super power ukitembea ,ukilala ,ukitizama anga ,viumbe na mimea kwangu huyo Muumbaji ndiye ninayemwamini. Hadithi kila mmoja ana yakwake chukua kinachofiti kwenye akili yako ninachokiamini usichkulie huu uumbaji/ chanzo kama kazi ya mtu bali nguvu na uwezo kiroho zaidi.
 
Hizo kanuni zinazoegemea upande?
 
Kwahiyo unaamini Mungu alieumba vyote hivyo ni huyo alietajwa kwenye vitabu vya dini?
 
Hapa naweza kukuelewa ni kweli kuna uwezekano dunia ina chanzo

Ila kwa hadithi za Qur’an na bible mapungufu ni mengi tena ya wazi
 
Kwani hujui kule kanisani mapepo huwabamiza chini bila huruma.

Kwa mfano, kuna mama mmoja hapa jirani anamakovu mwili mzima kwa sababu ya kukatwa mitama na pepo.

Yaani, pepo anakukata mtama na hajali kama utaangukia kiti ama la! πŸ₯²
Hii sometimes huwa ni akili yako ndio inakuendesha tu hasa kwenye hizi nyumba za ibada lakini uwepo wa mapepo wabaya upo sana, nakumbuka mwaka fulani nilienda kanisa fulani la Wanaijeria nilitajwq jina na yule Pastor bila hata kumwambia, tarehe,mwaka na mwezi wa kuzaliwa πŸ˜€ yaanj mpaka wilaya niliyozaliwa , hapo nilijiuliza sana japo haikuniletea suluhisho ya lile nililokuwa nalitaka.

Wakati mwingine Ubongo wetu hupenda sana mambo marahisi tofauti na uhalisia wa kile tunachokitaka, how come upate kazi nzuri bila kuangalia kwamba hiyo kazi ina ushindani ? Kwanini upate pesa kwa njia ya maombi tu bila kujua siri ya hiyo pesa ?

Ninachokumbuka lile kanisa niliombewa nikaruka mapepo kama yote 🀣🀣🀣 nikachana mpaka suruali yangu cadet kaliii na kiatu kikaachia sole πŸ˜‚

Mapepo wapo lakini akili za waamini wengi zimeshapumbazwa na ujinga wa hawa wakujiita Manabii maana inashangaza kila mara mapepo yanakemewa die by fire πŸ”₯ Holy spirit na blah blah kibao .

Hayo mambo ya mapepo na majini yapo kabisa na watu tushapigwa sana zongo. Nakumbuka sehemu fulani kuna dogo ni mtaalamu sana wa dua alibis viatu vyake msibani akaenda kununua misumari na dawa kwenye maduka ya dawa za asili akachanganya akasomea akatengeneza kitu ambacho hakionekani akakituma kikamtamfute aliyeiba vile viatu mbona mwizi alirudisha ?
 
Mkuu, Mimi nitawaamini hao mapepo wachafu kama wapo siku wakinikata mtama kanisani.

Aidha, nitawaamini majini siku wakinilamba vibao bila huruma, sijui muda huo nikiwa sehemu gani, labda nikiwa napita maeneo ya makaburini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…