Majini & Mapepo πŸ‘»πŸ€”

Kwanza nikupongeze kwa kuibua maswali haya. Haya ni maswali ya msingi katika falsafa ya dini, na hata wanatheolojia, wanafalsafa na wanazuoni wa dini wameyajadili kwa karne nyingi.
Shukran sana
karibu kwenye mjadala mkuu
Kujua jambo kabla halijatokea si sawa na kulisababisha, nakubali

Lakini huu mfano wa rafiki uliouweka hauendani na hoja hii

Kumbuka Mungu anajinasibu kuwa yeye ni muumbaji wa kila kitu
Nadhani nikisema muumbaji wa kila kitu unaelewa ninachomaanisha, si ndiyo mkuu?

Kwa hiyo, si kwamba Mungu alijua tu kila kitu kitakachotokea kama ulivyosema kwenye mfano wa rafiki, bali yeye ndiye muumbaji wa hayo yote
kwa mantiki hiyo angeweza kuzuia
Yes, sasa swali linakuja, kwa nini Mungu aumbe viumbe wenye uwezo wa kutenda maovu?

Kwa nini asingewaumba viumbe ambao hawana kabisa huo udhaifu wa kutenda maovu?

Kumbuka Mungu ndiye muumbaji wa kila kitu
Kwanini mwanadamu awajibike kwa udhaifu alioumbwa nao?
Shetani mwenyewe anasema hakuwa na mamlaka ya kuwalazimisha wanadamu kufanya maovu, bali yeye anachofanya ni kuwaita na wao wanaitika

Kwa nini Mungu amuache Shetani aendelee kuishi huku akijua wazi kwamba ataendelea kuwarubuni wanadamu na kuwafanya waanguke dhambini?

Cha kushangaza zaidi Mungu aliwaangamiza watu wa Sodoma na Gomora, lakini akamwacha Shetani, ambaye ndiye chanzo I mean mdanganyifu

Hapa hata siongei sana Shetani alipaswa kuuwa mapema kabisa sioni mantiki ya kumuacha aishi

Sijawahi kuelewa yaani
Kwa nini mwanadamu aadhibiwe kwa makosa yake wakati yeye ndiye aliyeumbwa akiwa na matamanio, wivu na madhaifu mengine kibao?

Kosa lake hasa liko wapi ikiwa hakujiumba mwenyewe wala hakuchagua kuwa na hizo tabia na madhaifu?

Kwa nini Mungu asingemuumba mwanadamu akiwa mkamilifu, asiye na matamanio yanayovuka mipaka
wivu na mielekeo ya kutenda maovu?

Yaani Why Why nashindwa kuelewa

Kulikua na haja gani ya kuumba vitu complicated mkuu?
Na uwezekano wa kuumba vitu straight upo?
Yaani kama haya majanga ndio kabisaaa nashangazwa na namna Mungu anaacha dunia iwe uwanja wa fujo na mabalaa je anafurahia
Hakuna majini hakuna mapepo
Ukitaka unaweza kuvitengeneza kwenye akili yako
Kama una amini vipo weka ushahidi
Hizi dini nazo ni za wapiga dili tu mie hata siziamini nimetumia bible kukujibu kwa sababu mada inahusu hivyo vitabu vitakatifu kama msemavyo

Na pia ujue Qur'an ni copy end paste ya bibilia agano la kale
Kwa hiyo, tusichanganye mafundisho haya.

Kuwa na maswali kuhusu Mungu si kosa. Hata watu wa imani wamekuwa wakiuliza maswali hayo. Lakini pia hatupaswi kudhani kwamba kwa sababu hatujaelewa sababu ya jambo fulani, basi jambo hilo halina sababu.
Sababu kama zipo ziainishe nipo tayari kujifunza mkuu
Ingekua bora tungeumbwa kwa ukamilifu Yes kuliko hizi songombingu

Kwako Jagina

Alooo nimetumia muda kuandika nandika nafuta naandika nafuta πŸ™ŒπŸΌπŸ™ŒπŸΌπŸ™ŒπŸΌ
 
1.Mungu aliumba malaika ili wawe waangalizi wa uumbaji wake, shetani ni malaika mmojawapo baadaye akaasi.kunamechanism ya kupambana na shetani
Shatani alitoa wapi hii tabia ?
Uasi ulitoka wapi?
 

Mkuu, nimekusoma vizuri. Maswali yako yana uzito, lakini kuna mambo kadhaa tunayopaswa kuyatofautisha.

1. Kwa nini Mungu aliumba mwanadamu mwenye matamanio na uwezo wa kufanya maovu?

Katika Uislamu, kuwa na matamanio si dhambi. Matamanio ni sehemu ya maumbile ya mwanadamu. Tatizo si kuwa na matamanio, bali ni namna mtu anavyoyatumia. Kwa mfano, hasira si dhambi yenyewe, lakini kumdhulumu mtu kwa sababu ya hasira ni kosa.

Mungu ametupa akili, dhamiri na uwezo wa kuchagua. Qur'an 91:7–10 inaeleza nafsi ya mwanadamu na uwezo wake wa kutambua uovu na uchamungu.

2. Kwa nini Mungu hakumuumba mwanadamu mkamilifu asiyeweza kutenda maovu?

Mungu angeweza kuumba viumbe wasiomuasi. Qur'an 66:6 inasema malaika hawamuasi Mungu. Lakini mwanadamu ameumbwa akiwa na uwezo wa kuchagua. Hapo ndipo maana ya mtihani, uwajibikaji na uchaguzi wa mema inapopatikana.

3. Kwa nini Mungu hakumuangamiza Shetani mapema?

Hili ni swali muhimu. Lakini kumbuka Shetani hana mamlaka ya kumlazimisha mwanadamu kutenda dhambi. Qur'an 14:22 inamnukuu Shetani akisema kwamba yeye aliwaita tu, nao wakaitikia. Mungu amempa muda maalumu, lakini hilo halimaanishi kwamba anakubaliana na matendo yake.

4. Kwa nini mwanadamu aadhibiwe kwa udhaifu ambao hakuchagua kuwa nao?

Hapa kuna msingi muhimu wa Uislamu: Mungu hamwadhibu mtu kwa sababu tu ana matamanio au udhaifu wa kibinadamu. Anamhukumu kwa matendo yake, kwa kuzingatia uwezo na mazingira yake.

Qur'an 2:286 inasema: "Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo."

Pia Qur'an 6:164 inasema hakuna nafsi itakayobeba dhambi ya nafsi nyingine.

5. Kuhusu majini na mapepo

Naelewa kwamba wewe huamini uwepo wao. Lakini kwa Muislamu, uwepo wa majini ni sehemu ya imani inayotokana na wahyi. Qur'an ina sura nzima inayoitwa Al-Jinn (Sura ya 72). Huo ni ushahidi wa maandiko kwa anayeukubali wahyi, ingawa ninaelewa kwamba wewe unatafuta pia ushahidi unaoweza kuthibitishwa kisayansi.

6. Kuhusu madai kwamba Qur'an ni nakala ya Biblia

Kufanana kwa baadhi ya simulizi hakuthibitishi moja kwa moja kwamba kitabu kimenakiliwa. Qur'an yenyewe inakiri kwamba Mungu aliteremsha vitabu kabla yake, lakini pia inatofautiana na Biblia katika baadhi ya mafundisho na simulizi.

Mkuu, nakubaliana nawe kwamba swali la kwa nini Mungu aliruhusu uwezekano wa uovu wakati alikuwa na uwezo wa kuuzuia ni swali kubwa la kifalsafa.

Lakini ningependa kukuuliza jambo moja: Je, kwa mtazamo wako, dunia ambayo viumbe wana uwezo wa kuchagua mema lakini pia wanaweza kuchagua mabaya haina thamani yoyote kuliko dunia ambayo hakuna kiumbe mwenye uwezo wa kufanya uchaguzi wa kimaadili?

​

 
Samahani mkuu unatumia AI kunijibu?

Nashangazwa namna ambavyo badala ya kunijibu maswali yangu ni kama unaniuliza tena

Sasa tutakuwa tunaulizana tuu bila kupeana majibu?

now nipo barabarani
Nikitulia nitakuja kukujibu
 
MUNGU Hakuumba mabaya.mabaya maana yake kwenda kinyume na mambo mema au utaratibu wa Mungu.shetani na wenzake wakawafundisha binadamu kwenda kinyume na Mungu.
Shetani na wenzake ndio wakafundisha binadamu
Haya yeye Shetani alifundishwa na nani?
 
Shetani na wenzake ndio wakafundisha binadamu
Haya yeye Shetani alifundishwa na nani?
We mdada unazungumzia asili ya vitu vyote kuna uhasi+uchanya. Na vyote ni kipimo kwako wewe binadamu kuumbwa kwa ulimwengu haikuwa kirahisi bila hata maandiko kwa mtazamoo tuu ipo nguvu kuu, unamini katika Mungu????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…