Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,264
Napenda kutolea mifano humu jamvini. Nyani ngabu, Mziwanda, Mzee Mwanakijiji, Kibunango, Kichuguu, Bubu , Mzizi mkavu, Mbu, Visenti, MwanaFA, Masanilo, Kuntakinte, Kizimkazimkuu, Msanii, Dingiswayo, (sitawamaliza)
Changamoto kwa akina Invisible, Field Marshall, Wos, Next level, Pretty, Fidel, Allien, Sasha Fierce, Lazy dog, Game theory, na wengine wengi.
Na idadi kubwa ya watanzania tuwe na majina ya asili yetu. Tusijidanganye na majina ya magharibi nay a watakatifu na ya Mashariki ya kati. Ukarimu huanzia nyumbani.
Mziwanda hahahah.
WoS siyo jina...laiti ningeweza kukutajia jina langu la kiasili.
Mzalendo Halisi Vipi? Sii la kibantu hilo?? Lol!
Jina ni jina tu liwe la kizungu au kibantu, ilimradi liwe na maana nzuri.
Hii mada naikubali kabisa mkuu,
Umesahahau kuwa siku hizi hata kuongea kiswahili matamshi ni kama kiingereza.
Yaani mtu anatamka kiswahili kama vile kiingereza, sio hiyo tu hata kutembea miondoko ni ya kiinglish, mkuu, ndo sayansi na kutokujua(science & technology)
Ukikataa majina ya "kizungu" (ambayo mengi yana asili ya kiyahudi kwa kweli, wala si "kizungu") na kukumbatia dini za kigeni, ambazo ndizo hasa mzizi wa haya majina, utakuwa unaacha ugonjwa na kujaribu kutibu dalili.
Kama unataka mabadiliko ya msingi katika fikra anzia kwenye dini, majina yatajibadilisha yenyewe.
Mobutu aliwabadilisha Wazaire (then) wote majina kwa nguvu, kwa kuanzia na yeye mwenyewe, kutoka Joseph Mobutu kwenda Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa Za Banga, lakini ikaja gundulika zilikuwa ilikuwa ni circus trick ku distract attention kutoka issues za kiuchumi.
Juhudi za kuturudishia identity yetu kama watu kitamaduni ni lazima ziende sawa na juhudi za kuinua watu kiuchumi, ama sivyo itakuwa sawa na mambo ya Mobutu.
Mi hata sijui la kwangu asili yake ni wapi......ivo ivo tu
hata mabrotherman wana style hii.hii staili wanayo masistaduu zaidi mkuu
Vingapi mlivyoiga toka uzunguni? Halafu leo majina yawe tija.Pretty,
No!! No!!
Nchi nyigine lazima mtoto upewe jina linalokubalika na jamii yao!
Lini umeenda Sweden ukakuta jina Zawadi?? Au China au japan ukakuta jina la kiswahili??
Taabu kubwa ya Afrika tunaiga kila kitu na kudharau vya kwetu!
Why can't we name our own children African names?? Why Europen names??