Majina ya rangi uzijuazo kwa Kiswahili

Majina ya rangi uzijuazo kwa Kiswahili

Red = Nyekundu
Green = Kijani, Chanikiwiti
 
Mmmh nakumbuka km bibi aliniambia chanikiwiti ni kijani ile ya mwajuma yuleeeee!!!!!
 
wee kweli kituko hahahhaaa-bolded words
rangi nyingi sijui kiswahili chake kwakweli...shida tupu na huu uswahili
lugha haijitoshelezi labda mtu wa BAKITA ateremshe desa hapa

Samawati ni kiswahili au kiarabu? Maana samawati maana yake ni mbingu na neno samawati limetajwa sana kwenye Quraan
 
Sawati ni mbingu kweli kwa kiarabu but mbingu huwa inarangi ya blue ndio maana kiswahili walitumia neno hilo
 
Amavubi hapo sasa? Biblia ina majina ya rangi adi unashangaa kama zipo dunia ya sasa
 
Last edited by a moderator:
Samawati = blue
Hudhurungi = grey (kijivu???)
Kahawia = brown
Zambarau = purple
Rangi ya fedha = silver
Pinki = pink
Hope my memory card is still in place.

Green - kijani
orange - hudhurungi (siyo grey)
grey - kijivu
yellow - manjano
white - nyeupe
gold - dhahabu
red - nyekundu

kuna rangi inaitwa "chanikiwiti" sikumbuki ni rangi gani kwa kizungu
 
hudhurungi = light brown (Mfano rangi ya mkate)
 
Green - kijani
orange - hudhurungi (siyo grey)
grey - kijivu
yellow - manjano
white - nyeupe
gold - dhahabu
red - nyekundu

kuna rangi inaitwa "chanikiwiti" sikumbuki ni rangi gani kwa kizungu

hivi dhahabu haina rangi ya kujitosheleza ki maelezo, hivi na udongo una rangi gani?
 
Green - kijani
orange - hudhurungi (siyo grey)
grey - kijivu
yellow - manjano
white - nyeupe
gold - dhahabu
red - nyekundu

kuna rangi inaitwa "chanikiwiti" sikumbuki ni rangi gani kwa kizungu

Chanikiwiki sio sky blue?

Hudhurungi ni Orange??? Nadhani hapana??
 
Kiswahili ni lugha ya Kibantu, na lugha (nyingi) za Kibantu, kwa asili, zinaelekea kuwa na maneno matatu tu yanayoeleza dhana ya rangi:
1. Rangi nyeupe,
2. Rangi nyeusi, na
3. Rangi nyekundu.

Kama unazungumza lugha mojawapo ya Kibantu, jaribu kutafuta majina ya rangi, na utakutana na maneno ya rangi hizi tatu tu.

Katika Kiswahili, maneno mengine yanayotaja rangi tumekuwa tukiyapata kwa: (i) kutohoa kutoka lugha nyingine, kama vile Kiarabu na Kiingereza, na (ii) kwa kutumia analojia, yaani, kufananisha rangi husika na ile ya kitu fulani (kama vile chungwa, kahawa, zambarau, majani, udongo, ugoro, damu ya mzee, n.k.).

Kwa maneno yenye asili ya Kibantu, utaona kuwa maneno hayo yanaoana vizuri na sarufi ya lugha ya Kiswahili kwani yanatokea kama vivumishi vya kawaida tu vya neno 'rangi' (tazama <rangi nyeupe>, <rangi nyeusi>, <rangi nyekundu>; linganisha na <rangi nzuri>, <rangi mbaya>, <rangi nyingi>).

Lakini kwa maneno yanayoeleza rangi ambayo yametoholewa au yanatumia utaratibu wa analojia, utaona kuwa tunahitaji kutumia kihusishi <ya> ili kuhusisha 'rangi fulani' na 'kitu fulani', kama vile:
4. Rangi ya bluu (na sio rangi bluu),
5. Rangi ya kijani (na sio rangi kijani),
6. Rangi ya zambarau (na sio rangi zambarau),
7. Rangi ya samawati (na sio rangi samawati) n.k.

Kwa wazungumzaji tulio wengi, kanuni hizi (za kutumia au kutotumia <ya>) tunazijua lakini hatujui kwamba tunazijua! Kwa wanaojifunza Kiswahili ukubwani, inawabidi wajifunze kanuni zote hizi. Utawasikia wengine wakisema <Hii nguo ina rangi ya nyekundu.>.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom