Majina ya magereza yana maana yoyote?

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,730
1,201
Habari za wikend wadau,huwa najiuliza kama majina ya magereza yetu hapa nchini kama yana maana yeyote,mfano utokapo morogoro kwenda Dodoma,kabla ya kufika Dumila,ukiwa maeneo ya WAMI-DAKAWA,hapa kuna magereza kadhaa,ila kuna gereza linaitwa GEREZA LA MTEGO WA SIMBA.....ni gereza kuubwa sana linajihusiha na masuala ya KILIMO(kama ilivyo kwa magereza meengi ya mkoani morogoro),sijajua sababu ya kupewa jina hili,nawe tupia jina la gereza unalolijua na utuambie huenda lina maana......
Siku njema wadau
 
Magereza mengi nijuavyo mimi yalijengwa enzi za ukoloni hivyo yalipewa majina ya maeneo husika kama, Gereza Ukonga - Ukonga, Gereza Songwe - Songwe, Gereza Mugumu - Mugumu Mara n.k
 
Pia maeneo hayo hayo ya DAKAWA kuna GEREZA LA VIJANA LA MBIGIRI,,,,nachojua mimi mbigiri ni aina ya majani ambayo hutoa miba mikali sana,,,,,,,
 
Magereza mengi nijuavyo mimi yalijengwa enzi za ukoloni hivyo yalipewa majina ya maeneo husika kama, Gereza Ukonga - Ukonga, Gereza Songwe - Songwe, Gereza Mugumu - Mugumu Mara n.k

swadakta mzee wa rula,,,,hilo halina shaka,,,,ila sasa mengine yana majina tata sana,,,,mfano huo wa MTEGO WA SIMBA,wakat eneo lile linaitwa DAKAWA,,,yaan ile uniqueness,,,,,au mbigiri,nalo lipo hapohapo
 
jina la kitu ni historia fulani. mtego wa simba, lazima wenyeji waliwahi kutega simba hapo na wakampata. kuanzia hapo likajulikana hivyo
 
Gereza la maweni tanga.
Gereza la maweni Tanga jina limetokana na mandhari ya eneo lenyewe limezungukwa na mawe makubwa.
 
Gereza la maweni tanga.
Gereza la maweni Tanga jina limetokana na mandhari ya eneo lenyewe limezungukwa na mawe
makubwa.
asante sana mdau kwa jibu murua ndo nilikua nahitaji kujua kitu kama hiki
 
Isupilo-Mafinga,Kigongoni-Bagamoyo,Bwawani-Bagamoyo.Kisongo-Arusha!!!
 
Isanga-dodoma,segerea-dar!keko-dar,haya yanachukua majina ya maeneo yalipo!
 
Back
Top Bottom