Majina vigogo wa Unga: Naomba Ikulu inipatie niwataje bila mazingaombwe

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,379
SUALA LA MADAWA YA KULEVYA LINAIGUSA MOJA KWA MOJA CCM NA VIGOGO WAKE.

Miaka yote wahusika tunaambiwa wahusika wapo, na majina yapo Ikulu tangu JK. Sasa mnapropaganda nini. Kama tunakubaliana kusamehe basi samaki wapewe maonyo na Kula kiapo cha kuachana na hio biashara.

Tusiwasingizie dàgaa kwa kuwaficha Samaki. Majina yapo Ikulu, yatolewe hadharani. Najua fika mnaogopa kama ilivyo kwa vigogo wanaotumia majina ya watu ambao mpaka Leo mnaogopa kuwataja. Usishangae hata anayewatangaza dagaa(mateja) katumwa na Samaki(vigogo wa unga). Ili kuhadaa umma.

Nipeni Mimi Deogratius Kisandu hao samaki(wamiliki wa magodauni ya madawa ya kulevya) niwataje kuliko kuadhirisha mateja(dagaa) na wasambazaji(furu).

Tatizo sio vijana wetu, tatizo ni mfumo danganyifu, usiotaka kufanya kazi na watu wakweli.

Deogratius Nalimi Kisandu
Mtemi Kiongozi wa chama cha ACA tarajiwa.
 
Ngosha Deo,
Tatizo hutaki ushauri, ungetusikiliza na sie tunapokupa ushauri.
Kwani tatizo la madawa ya kulevya liko kwenye kutaja? Kutaja majina ndo kukomesha biashara ya mihadarati?
Narudia tena ndugu yangu. Kafanye moja kati ya haya mawili....KUFUGA au KULIMA hizi kiki si za mtu anaetarajiwa kuwa kiongozi mkuu wa chama kikuu cha siasa barani Africa....
 
Ukweli ni kwamba wahusika was dawa za kulevya hakuna hata mmoja ktk orodha ya Makonda kaweka upuuzi mtupu pale. Mbona Magufuli anayo orodha ya hata askali wanaohusika na si hao wa Makonda
 
Sioni tatizo lake pia anapaswa kupewa support na wa Tanzania wote wazalendo kwa maamuzi yake
 
SWALA LA MADAWA YA KULEVYA LINAIGUSA MOJA KWA MOJA CCM NA VIGOGO WAKE.

Miaka yote wahusika tunaambiwa wahusika wapo, na majina yapo Ikulu tangu JK. Sasa mnapropaganda nini. Kama tunakubaliana kusamehe basi samaki wapewe maonyo na Kula kiapo cha kuachana na hio biashara.

Tusiwasingizie dàgaa kwa kuwaficha Samaki. Majina yapo Ikulu, yatolewe hadharani. Najua fika mnaogopa kama ilivyo kwa vigogo wanaotumia majina ya watu ambao mpaka Leo mnaogopa kuwataja. Usishangae hata anayewatangaza dagaa(mateja) katumwa na Samaki(vigogo wa unga). Ili kuhadaa umma.

Nipeni Mimi Deogratius Kisandu hao samaki(wamiliki wa magodauni ya madawa ya kulevya) niwataje kuliko kuadhirisha mateja(dagaa) na wasambazaji(furu).

Tatizo sio vijana wetu, tatizo ni mfumo danganyifu, usiotaka kufanya kazi na watu wakweli.

Deogratius Nalimi Kisandu
Mtemi Kiongozi wa chama cha ACA tarajiwa.
It is dangerous to be right while the government is wrong... U will be digging ur own grave. Case study Jacob Juma
 
tatizo watu washazoea kumkejeli Deo, sijaona sababu concrete ya kumdhihaki kwenge huu uzi wa leo. Kaongea kitu cha msingi.. Kama Juma Pondamali Maembe ameshindwa kuwataja AMPE DEO HAYO MAJINA AYAWEKE HADHARANK
 
Kisandu yuko sawa leo
Watu msimdhihaki Kisandu kama anataka kupewa hayo majina kama kuna Mwenye ujasiri wa kumpa ampe, Mimi binafsi hata nikipewa hayo majina kitendo cha kumaliza kuyasoma nikitoka nje ndo habari yangu itaishia hapo, sasa kama kuna mtu ana uhakika na usalama wake na ana uwezo wa kuyaanika hayo majina kwanini mnamtolea matusi wakuu? Acheni stress za maisha
 
Back
Top Bottom