Majimoto wanavyodhibiti wadudu waharibifu wa mazao

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
ZwB5B7

Majimoto wakishambulia faurongo kwenye embe

SEKTA ya kilimo kama zilivyo sekta zingine nchini, imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo magonjwa na wadudu wanaoshambulia mazao na kuwafanya wakulima kupata mavuno machache tofauti na matarajio yao.

Mazao kama ya embe, korosho na machungwa yamekuwa yakishambuliwa na wadudu na magonjwa mbalimbali, jambo ambalo linaelezwa kuwakosesha wakulima soko la uhakika hasa nje ya nchi baada ya wakulima kulazimika kutumia dawa zenye sumu kupambana na magonjwa au kuua wadudu waharibifu (visumbufu vya mazao).

Dawa hizo zinaelezwa kutokuwa rafiki kwa mazingira na kwa afya ya binadamu. Hata hivyo, suluhu ya visumbufu hivyo vya mazao (wadudu waharibifu) unaonekana kupatiwa suluhisho kutokana na utafiti wa miaka kadhaa wa Profesa Maulid Mwatawala wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha SUA juu ya matumizi ya mdudu anayejulikana kwa jina la kitaalamu kama oecophylla longinoda au majimoto kwa lugha ya kiswahili.

Mdudu majimoto ambaye aligunduliwa kwenye miaka ya 1930 kupitia tafiti za kibayolojia, katika nchi za kusini mashariki mwa bara la Asia na Australia, alianza kufanyiwa utafiti hapa nchini mwaka 2011 chini ya usimamizi wa Profesa Mwatawala wa Chuo Kikuu cha SUA kabla ya kuanza rasmi kupandikizwa kwenye mazao ya korosho, maembe na michungwa mwaka 2012. Tafiti katika sehemu mbali mbali za China na Asia ya Kusini zimeonesha kuwa majimoto ana uwezo wa kudhibiti visumbufu vya mazao zaidi ya 50 katika mazao mbali mbali.

Kwa mujibu wa mtafiti mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Nassor Abdallah, miongoni kwa visumbufu vinavyoweza kudhibitiwa na majimoto ni mbu wa mikorosho (helopeltis species), wadudu aina ya coreid bug wa kwenye mikorosho, minazi na miembe.

Nassor ambaye alikuwa akizungumza na kundi la waandishi wa habari waliokuwa katika mafunzo ya uandishi wa habari za kilimo na lishe yaliyoandaliwa na taasisi ya iAGRI mjini Morogoro hivi karibuni chini ya mkufunzi Ndimara Tegambwage, anasema wadudu waharibifu wengine wanaouliwa na majimoto ni vithiripi (thrips) kwenye miembe na mikorosho, nzi waharibifu wa matunda (fruit flies) kwenye miembe na michungwa.

Wadudu wengine wanauliwa na majimoto ni kifaurongo (mango seed weevils) kwenye maembe, visumbufu vya zao la kakao, visumbufu vya mazao ya msituni kama Mahogany na Mkaratusi na pia wadudu hatari kama nyoka hawawezi kusogelea katika zao lolote linalolindwa kwa kutumia majimoto,anasema.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Kitengo cha utafiti wa kudhibiti wadudu waharibifu wa mikorosho, miembe na michungwa kwa kutumia majimoto wa Chuo Kikuu cha SUA, Profesa Maulid Mwatawala, Nassor anasema kuna aina mbili za majimoto ambao ni oecophylla longinoda anayepatikana katika nchi za tropiki hususan Afrika na oecophylla smaragdina anayepatikana katika nchi za bara la Asia pamoja na Australia.

Anasema malkia wa majimoto aliyepandwa amekuwa akipatikana katika mashamba na miti zaidi katika majira ya mvua hasa miezi ya Desemba ambapo huchukuliwa na kupelekwa maabara kwa ajili ya utafiti wa kibayolojia.

Majimoto wanaishi kwenye viota na kwa kawaida hupatikana katika miti ya msituni, lakini pia katika miti mbalimbali ya matunda kama miembe, michungwa, mistafeli, kahawa, kakao, mikorosho, miti ya msituni na huishi kwa kutegemea sukari kama chanzo chao cha nguvu na wadudu wadogo wadogo kama chanzo cha protini,anasema.

Anasema koloni (ukoo) la majimoto linaweza kuwa kubwa sana lenye viota zaidi ya 100 kupitia aina mbali mbali ya mimea na kwamba koloni moja la majimoto wa Afrika linaundwa na malkia mmoja na wafanyakazi wasiopungua nusu milioni au zaidi.

Hata hivyo, tafiti zilizofanyika katika nchi za Australia na Asia ya Kusini Mashariki zimeonesha kuwa koloni moja linaweza kuwa na malkia zaidi ya mmoja, huku koloni la majimoto likiwa limegawanyika na limekuwa likiundwa katika makundi makubwa matatu,anasema.

Anasema kwa majimoto wa ukanda wa tropiki barani Afrika, kila koloni linaanzishwa na malkia mmoja aliyepandwa ambaye kwa mara ya kwanza hutaga mayai yake juu ya majani na kuyalinda mpaka anapototoa na kuwa wafanyakazi waliokomaa na kuanza kutengeneza viota.

Baada ya kupandwa na kurudi kuanzisha koloni, malkia hutumia akiba ya protini aliyohifadhi mwilini mwake baada ya kupandwa kwa ajili ya kujikimu kwa chakula na huendelea kutaga mayai zaidi katika uhai wake wote bila kuhitaji kupandwa tena,anasema.

Nassor anasema kama malkia aliyepandwa atatunzwa na kupatiwa huduma nzuri kwenye nyumba maalum za kuwalea (screen house), anaweza kuwa na koloni kubwa ambalo litaweza kudhibiti visumbufu vya mazao katika kipindi cha ndani ya miezi sita.

Anasema watafiti humkamata malkia wa majimoto aliyepandwa kwa kutumia viota vya bandia vinavyotengenezwa kwa kutumia majani ya mmea, karatasi, au kwenye mitego maalumu inayotumia mwanga kuvuta wadudu mara baada ya kupandiwa na dume. Katika kupandiana huko, majimoto (jike na dume) huruka juu angani na baada ya kumaliza kitendo hicho dume hufa na malkia hungoka mbawa na kuwa tayari kwa ajili ya kutaga.

Malkia ana uwezo wa kutaga hadi mayai mia moja kwa siku. Malkia baada ya kukamatwa huhifadhiwa maabara/nyumba maalum za kuwalea kwa ajili ya kupatiwa huduma na baada ya siku mbili hadi tatu tangu kupandwa huanza kutaga huku wafanyakazi wakianza kuchomoza ndani ya kipindi kisichozidi siku thelathini,anasema.

Anasema malkia hukitunza kizazi cha kwanza kwa kukipatia huduma zote muhimu za chakula na katika kipindi hicho, malkia hupoteza hadi asilimia sitini ya uzito wake hadi hapo wafanyakazi wa kwanza watakapoweza kuhudumia kizazi kipya pamoja na malkia mwenyewe.

Vile vile, majimoto wanaweza kupandikizwa kwenye shamba la miti ya matunda kwa kuvuna na kupandikiza koloni (ukoo) la majimoto kutoka kwenye chanzo (mti wa porini au mti mwingine wowote wa matunda).

Kwa kutumia njia hii, hatua ya kwanza ni kukitambua kiota kinachobeba malkia na baada ya kumpata malkia, hatua inayofuata ni kuvuna kiota hicho na kukitunza kwenye mfuko wa rambo kabla ya kuendelea kuvuna viota vingine katika koloni hilo na kuvitunza pia kwenye mifuko mingine ya rambo kwa ajili ya kubebwa na kupandikizwa kwenye shamba husika, mfuko mmoja wa rambo unaweza kubeba viota vinne hadi sita kulingana na ukubwa wa viota hivyo,anasema.

SEKTA ya kilimo kama zilivyo sekta zingine nchini, imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo magonjwa na wadudu wanaoshambulia mazao na kuwafanya wakulima kupata mavuno machache tofauti na matarajio yao.

Mazao kama ya embe, korosho na machungwa yamekuwa yakishambuliwa na wadudu na magonjwa mbalimbali, jambo ambalo linaelezwa kuwakosesha wakulima soko la uhakika hasa nje ya nchi baada ya wakulima kulazimika kutumia dawa zenye sumu kupambana na magonjwa au kuua wadudu waharibifu (visumbufu vya mazao).

Dawa hizo zinaelezwa kutokuwa rafiki kwa mazingira na kwa afya ya binadamu. Hata hivyo, suluhu ya visumbufu hivyo vya mazao (wadudu waharibifu) unaonekana kupatiwa suluhisho kutokana na utafiti wa miaka kadhaa wa Profesa Maulid Mwatawala wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha SUA juu ya matumizi ya mdudu anayejulikana kwa jina la kitaalamu kama oecophylla longinoda au majimoto kwa lugha ya kiswahili.

Mdudu majimoto ambaye aligunduliwa kwenye miaka ya 1930 kupitia tafiti za kibayolojia, katika nchi za kusini mashariki mwa bara la Asia na Australia, alianza kufanyiwa utafiti hapa nchini mwaka 2011 chini ya usimamizi wa Profesa Mwatawala wa Chuo Kikuu cha SUA kabla ya kuanza rasmi kupandikizwa kwenye mazao ya korosho, maembe na michungwa mwaka 2012. Tafiti katika sehemu mbali mbali za China na Asia ya Kusini zimeonesha kuwa majimoto ana uwezo wa kudhibiti visumbufu vya mazao zaidi ya 50 katika mazao mbali mbali.

Kwa mujibu wa mtafiti mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Nassor Abdallah, miongoni kwa visumbufu vinavyoweza kudhibitiwa na majimoto ni mbu wa mikorosho (helopeltis species), wadudu aina ya coreid bug wa kwenye mikorosho, minazi na miembe.

Nassor ambaye alikuwa akizungumza na kundi la waandishi wa habari waliokuwa katika mafunzo ya uandishi wa habari za kilimo na lishe yaliyoandaliwa na taasisi ya iAGRI mjini Morogoro hivi karibuni chini ya mkufunzi Ndimara Tegambwage, anasema wadudu waharibifu wengine wanaouliwa na majimoto ni vithiripi (thrips) kwenye miembe na mikorosho, nzi waharibifu wa matunda (fruit flies) kwenye miembe na michungwa.

Wadudu wengine wanauliwa na majimoto ni kifaurongo (mango seed weevils) kwenye maembe, visumbufu vya zao la kakao, visumbufu vya mazao ya msituni kama Mahogany na Mkaratusi na pia wadudu hatari kama nyoka hawawezi kusogelea katika zao lolote linalolindwa kwa kutumia majimoto,anasema.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Kitengo cha utafiti wa kudhibiti wadudu waharibifu wa mikorosho, miembe na michungwa kwa kutumia majimoto wa Chuo Kikuu cha SUA, Profesa Maulid Mwatawala, Nassor anasema kuna aina mbili za majimoto ambao ni oecophylla longinoda anayepatikana katika nchi za tropiki hususan Afrika na oecophylla smaragdina anayepatikana katika nchi za bara la Asia pamoja na Australia.

Anasema malkia wa majimoto aliyepandwa amekuwa akipatikana katika mashamba na miti zaidi katika majira ya mvua hasa miezi ya Desemba ambapo huchukuliwa na kupelekwa maabara kwa ajili ya utafiti wa kibayolojia. Majimoto wanaishi kwenye viota na kwa kawaida hupatikana katika miti ya msituni, lakini pia katika miti mbalimbali ya matunda kama miembe, michungwa, mistafeli, kahawa, kakao, mikorosho, miti ya msituni na huishi kwa kutegemea sukari kama chanzo chao cha nguvu na wadudu wadogo wadogo kama chanzo cha protini,anasema.

Anasema koloni (ukoo) la majimoto linaweza kuwa kubwa sana lenye viota zaidi ya 100 kupitia aina mbali mbali ya mimea na kwamba koloni moja la majimoto wa Afrika linaundwa na malkia mmoja na wafanyakazi wasiopungua nusu milioni au zaidi.

Hata hivyo, tafiti zilizofanyika katika nchi za Australia na Asia ya Kusini Mashariki zimeonesha kuwa koloni moja linaweza kuwa na malkia zaidi ya mmoja, huku koloni la majimoto likiwa limegawanyika na limekuwa likiundwa katika makundi makubwa matatu,anasema.

Anasema kwa majimoto wa ukanda wa tropiki barani Afrika, kila koloni linaanzishwa na malkia mmoja aliyepandwa ambaye kwa mara ya kwanza hutaga mayai yake juu ya majani na kuyalinda mpaka anapototoa na kuwa wafanyakazi waliokomaa na kuanza kutengeneza viota.

Baada ya kupandwa na kurudi kuanzisha koloni, malkia hutumia akiba ya protini aliyohifadhi mwilini mwake baada ya kupandwa kwa ajili ya kujikimu kwa chakula na huendelea kutaga mayai zaidi katika uhai wake wote bila kuhitaji kupandwa tena,anasema.

Nassor anasema kama malkia aliyepandwa atatunzwa na kupatiwa huduma nzuri kwenye nyumba maalum za kuwalea (screen house), anaweza kuwa na koloni kubwa ambalo litaweza kudhibiti visumbufu vya mazao katika kipindi cha ndani ya miezi sita.

Anasema watafiti humkamata malkia wa majimoto aliyepandwa kwa kutumia viota vya bandia vinavyotengenezwa kwa kutumia majani ya mmea, karatasi, au kwenye mitego maalumu inayotumia mwanga kuvuta wadudu mara baada ya kupandiwa na dume. Katika kupandiana huko, majimoto (jike na dume) huruka juu angani na baada ya kumaliza kitendo hicho dume hufa na malkia hungoka mbawa na kuwa tayari kwa ajili ya kutaga.

Malkia ana uwezo wa kutaga hadi mayai mia moja kwa siku. Malkia baada ya kukamatwa huhifadhiwa maabara/nyumba maalum za kuwalea kwa ajili ya kupatiwa huduma na baada ya siku mbili hadi tatu tangu kupandwa huanza kutaga huku wafanyakazi wakianza kuchomoza ndani ya kipindi kisichozidi siku thelathini,anasema.

Anasema malkia hukitunza kizazi cha kwanza kwa kukipatia huduma zote muhimu za chakula na katika kipindi hicho, malkia hupoteza hadi asilimia sitini ya uzito wake hadi hapo wafanyakazi wa kwanza watakapoweza kuhudumia kizazi kipya pamoja na malkia mwenyewe.

Vile vile, majimoto wanaweza kupandikizwa kwenye shamba la miti ya matunda kwa kuvuna na kupandikiza koloni (ukoo) la majimoto kutoka kwenye chanzo (mti wa porini au mti mwingine wowote wa matunda).

Kwa kutumia njia hii, hatua ya kwanza ni kukitambua kiota kinachobeba malkia na baada ya kumpata malkia, hatua inayofuata ni kuvuna kiota hicho na kukitunza kwenye mfuko wa rambo kabla ya kuendelea kuvuna viota vingine katika koloni hilo na kuvitunza pia kwenye mifuko mingine ya rambo kwa ajili ya kubebwa na kupandikizwa kwenye shamba husika, mfuko mmoja wa rambo unaweza kubeba viota vinne hadi sita kulingana na ukubwa wa viota hivyo,anasema.

Anasema majimoto hupendelea kula vyakula vyenye protini kama vile samaki na sukari, hivyo anapofikishwa kwenye nyumba za kuwalea, watafiti humtunza kwa kumpatia vyakula hivyo pamoja na sukari iliyoyeyushwa ambayo hupewa kwenye pamba iliyoloweshwa.

Endapo malkia atatunzwa na kupatiwa huduma nzuri, anaweza kutaga mayai mengi na kuanguliwa na baada ya miezi sita tangu kufikishwa maabara anaweza huchukuliwa na kupelekwa shambani kwa ajili ya kuanza kazi za kudhibiti visumbufu vya mazao,anasema.

Baada ya kufikishwa shambani wakiwa katika viota, hupandikizwa kwenye mmea ulioanza kutoa maua au majani mapya ambao kwa mujibu wa Nassor ndio hupendwa zaidi na wadudu waharibifu kutokana na sukari ambayo imekuwa ikipatikana kwenye maua na kwamba kiota kimoja hubeba majimoto zaidi ya 3000 kutegemeana na ukubwa wa kiota.

Kwa kawaida, malkia ana urefu wa karibu mm 20-25, na rangi yao kwa kawaida ni ya kijani au rangi ya udongo, kazi ya malkia ni kutaga tu na kwa kupandwa mara moja na dume na anakuwa na uwezo wa kuendelea kutaga mamilioni ya mayai katika uhai wake na kuweza kuishi hadi miaka 30 lakini wafanyakazi wanaishi kati ya mwaka mmoja hadi mitatu,anasema. Anasema wafanyakazi wadogo wanakuwa na urefu wa milimita tano hadi sita ambao huishi ndani ya kiota na kazi yao ni kulinda na kuangalia kizazi kipya huku wafanyakazi wakubwa wanaofikia urefu wa milimita 8 hadi 10, kazi yao kubwa ikiwa ni kutafuta chakula, kulinda, kudumisha na kupanua koloni.

Nassor anasema majimoto wamekuwa wakiishi katika makoloni kama watu wanavyoishi katika nchi na kwamba kila koloni huchukua miti kadhaa kama kila nchi inavyokuwa na miji kadhaa. Kwa mfano koloni linalochukua miti minane ni kama nchi moja yenye miji minane, mti na viota 21 ni mti mkubwa kama mji mkuu wa nchi, kila koloni kwenye mti lina viota vingi ni kama kila mji wenye wilaya nyingi, kila kiota kinabeba majimoto wengi mithili ya wilaya yenye watu wengi,anasema.

Nassor anasema utafiti umebaini kuwa tabia kuu za majimoto ni kuwa kila koloni linadhibitiwa na malkia mmoja, kama nchi inavyodhibitiwa na rais au waziri mkuu mmoja na kwamba katika koloni la majimoto, wenyewe wanakuwa ni marafiki kwa kila mmoja, wanatafuta chakula pamoja, wanawasiliana kati yao, wanalinda koloni lao na kuangalia kizazi hivyo ni sawa na watu ambao wanaishi ndani ya nchi moja (raia).

Kwa mujibu wa Nassor, koo moja ya majimoto haiwezi kuishi na koo nyingine kwenye mti mmoja na ikitokea koo mbili tofauti kukutana hupigana mpaka koo moja ife. Vita mara nyingi huanza pale koloni moja linapoingia kwenye makazi ya koloni jingine na kufananisha sawa na watu waliotekwa wakati wa kuvuka mpaka wa nchi bila ya hati ya kusafiria.

Pia Nassor anasema, majimoto wa koo moja hupandiana wenyewe kwa wenyewe wanaporuka na wanaporudi malkia huanzisha koo nyingine ambayo haiwezi tena kuwa rafiki na koo waliyozaliwa.

Anasema taaluma ya matumizi ya majomoto katika kudhibiti visumbufu vya mikorosho, michungwa na miembe imeanza kueleweka, kukubalika na kuigwa na mtu mmoja mmoja pamoja na vikundi.

Kwa upande wa zao la korosho, kikundi cha Masasi High Quality Farmers Products kilichoanzishwa mwaka 2007 kwa kuwashirikisha wakulima 840 kutoka vyama tofauti vya kilimo hai (organic farming) wa zao la korosho kutoka vijiji sita wilayani humo ambavyo ni Chiungutwa, Maugura, Temeke, Mpindimbi, Mwena, na Chakama vimeweza kuiga teknolojia hii na faida zimeonekana, anasema na kuongeza: Kundi hilo limekuwa likiendelea vizuri na kutokana na mafanikio waliyoyapata, wakulima zaidi wamekuwa wakijiungana na hadi kufikia mwaka 2013 lilikuwa na wanachama 1589 kutoka vijiji 12.

Nassor anasema kwa upande wa michungwa wakulima zaidi ya 20 kutoka kijiji cha Semngano wilayani Muheza, Tanga tayari wameanza kutumia taaluma hii kwa kuingiza majimoto katika michungwa yao na tayari wameona na kufurahia faida za majimoto kwenye mashamba yao.

Taaluma hii inazidi kuenea siku hadi siku kwa njia ya mkulima mmoja mmoja kuiga kutoka kwa mkulima mwingine. Kwa zao la maembe tayari wakulima wasiopungua watano wameiga taaluma hii huko Kibaha na kundi la wakulima 20 wanaopatikana Mkuranga wilayani Pwani inaelezwa kuwa w
HabariLeoaliomba kupatiwa mafunzo juu ya matumizi ya majimoto kudhibiti wadudu waharibifu wa maembe.

Anasema kundi hilo la wakulima 20 lilipatiwa mafunzo hayo na tayari kila mmoja amepandikiza majimoto kwenye mashamba yake na kwamba wanaendelea kuisambaza taaluma hiyo kwa wakulima wengine.

Nassor anasema matokeo ya utafiti wa majimoto yameonesha kuwa yana faida kubwa kwa wakulima hasa wanaofanya biashara ya kusafirisha nje ya nchi mazao kama ya korosho, embe na machungwa kwa sababu mataifa mengi ya nje yanapendelea mazao yasiyozalishwa kwa kutumia dawa aina yoyote yenye kemikali na kwamba gharama yake ni ndogo kulinganisha na mkulima anayelima kwa kutumia dawa zenye kemikali katika kuzuia wadudu waharibifu.

Gharama

Nassor anasema katika utafiti walioufanya, mkulima anayelima kisasa hekta moja ya zao la korosho lenye miti 70 alitumia gharama ya Sh. 846,650 kupandikiza majimoto, ukilinganisha na gharama za madawa zinazofikia Sh 1,225,350 kwa eneo hilo hilo la hekta moja.

Kwa upande wa maembe ambayo yalipandwa kwa nafasi ya mita 10 baina ya mwembe na mwembe, na kuchukua idadi ya miti 100 kwa hekta, gharama za kupandikiza majimoto zilikuwa Sh 404,400 kwa hekta na gharama za madawa zilikua Sh 1,092,000 kwa hekta.

Hata hivyo, gharama hizi zinatofautiana kutokana na masafa ambayo majimoto wa kupandikiza hufuatwa kutoka kwenye shamba wanalopatikana,anasema.

Nassor anaendelea kusema kuwa zao lililotunzwa kwa kutumia majimoto kwa mfano embe linaweza kuwa na doti nyeusi kutokana na tindikali inayotokana na majimoto.

Matokeo yaliyofanyika nchini Australia yameonesha kuwa kuna uhusiano mkubwa wa alama nyeusi (dotidoti) zinazosababishwa na majimoto na ubora wa ndani (kiwango cha sukari), embe haiozi haraka na vile vile alama hizo zinaweza kutumika kama kiashiria cha tunda salama na bora zaidi,anasema.

Hata hivyo, Mtafiti Nassor anaelezea changamoto kubwa ya matumizi ya majimoto ni pamoja na kushambuliwa na wadudu wengine kama vile sisimizi ambao hata hivyo hudhibitiwa kwa kupaka gundi chini ya mti unaolindwa na majimoto na kuzuia wadudu wa aina hiyo kupanda kwenye miti.

Njia nyingine ya kukabiliana na changamoto hiyo ni pamoja na kutumia chambo chenye sumu ambayo inakubalika katika kilimo hai (organic farming) kama spinosad. Kwa upande wake Saverina Tiba ambaye ni mfanyakazi msaidizi idara ya utafiti wa majimoto, anasema changamoto nyingine wakati majimoto wanapolelewa kwenye nyumba maalumu ni mashambulizi dhidi ya buibui.

Aidha Nassor anasema baadhi ya wakulima ambao hawajapata elimu sahihi ya matumizi ya majimoto, hudaiwa kuwa na hofu ya kungatwa wakati wa mavuno, lakini anasema hakuna madhara yoyote ambayo huweza kuyapata endapo utangatwa na maumivu yanayotoka na kungatwa ni ya muda mfupi tu. Anasema wakati wa mavuno mkulima anaweza kutumia samaki kwa kuweka chini ya mmea unaovunwa ambapo majimoto huvutiwa na harufu ya samaki na hushuka chini na kuanza kumla samaki huyo na kutoa nafasi kwa mvunaji kuendelea na kazi yake bila kushambuliwa sana.

Njia nyingine ni kupaka poda au majivu mikononi ambayo pia harufu yake humzuia majimoto asiweze kukungata au pia mkulima anaweza kutumia vazi maalum la kujikinga na kungatwa ambalo sio la gha
HabariLeorama kubwa,anasema.

Mtafiti Nassor anatoa ushauri kwa wakulima kote nchini kutumia teknolojia hiyo ya majimoto kudhibiti visumbufu vya mazao na kupata soko la uhakika la mazao yao nje ya nchi kutokana na walaji wengi kupendelea mazao yaliyolimwa kwa misingi ya kilimo hai (organic farming) kwa lengo la kulinda afya zao badala ya mazao yaliyolimwa kwa kutumia dawa za sumu ambazo zinaharibu mazingira, kuua viumbe visivyokusudiwa pamoja na kuhatarisha afya ya mwanadamu.

Chanzo: HabariLeo

Anasema majimoto hupendelea kula vyakula vyenye protini kama vile samaki na sukari, hivyo anapofikishwa kwenye nyumba za kuwalea, watafiti humtunza kwa kumpatia vyakula hivyo pamoja na sukari iliyoyeyushwa ambayo hupewa kwenye pamba iliyoloweshwa.

Endapo malkia atatunzwa na kupatiwa huduma nzuri, anaweza kutaga mayai mengi na kuanguliwa na baada ya miezi sita tangu kufikishwa maabara anaweza huchukuliwa na kupelekwa shambani kwa ajili ya kuanza kazi za kudhibiti visumbufu vya mazao,anasema.

Baada ya kufikishwa shambani wakiwa katika viota, hupandikizwa kwenye mmea ulioanza kutoa maua au majani mapya ambao kwa mujibu wa Nassor ndio hupendwa zaidi na wadudu waharibifu kutokana na sukari ambayo imekuwa ikipatikana kwenye maua na kwamba kiota kimoja hubeba majimoto zaidi ya 3000 kutegemeana na ukubwa wa kiota.

Kwa kawaida, malkia ana urefu wa karibu mm 20-25, na rangi yao kwa kawaida ni ya kijani au rangi ya udongo, kazi ya malkia ni kutaga tu na kwa kupandwa mara moja na dume na anakuwa na uwezo wa kuendelea kutaga mamilioni ya mayai katika uhai wake na kuweza kuishi hadi miaka 30 lakini wafanyakazi wanaishi kati ya mwaka mmoja hadi mitatu,anasema. Anasema wafanyakazi wadogo wanakuwa na urefu wa milimita tano hadi sita ambao huishi ndani ya kiota na kazi yao ni kulinda na kuangalia kizazi kipya huku wafanyakazi wakubwa wanaofikia urefu wa milimita 8 hadi 10, kazi yao kubwa ikiwa ni kutafuta chakula, kulinda, kudumisha na kupanua koloni.

Nassor anasema majimoto wamekuwa wakiishi katika makoloni kama watu wanavyoishi katika nchi na kwamba kila koloni huchukua miti kadhaa kama kila nchi inavyokuwa na miji kadhaa. Kwa mfano koloni linalochukua miti minane ni kama nchi moja yenye miji minane, mti na viota 21 ni mti mkubwa kama mji mkuu wa nchi, kila koloni kwenye mti lina viota vingi ni kama kila mji wenye wilaya nyingi, kila kiota kinabeba majimoto wengi mithili ya wilaya yenye watu wengi,anasema.

Nassor anasema utafiti umebaini kuwa tabia kuu za majimoto ni kuwa kila koloni linadhibitiwa na malkia mmoja, kama nchi inavyodhibitiwa na rais au waziri mkuu mmoja na kwamba katika koloni la majimoto, wenyewe wanakuwa ni marafiki kwa kila mmoja, wanatafuta chakula pamoja, wanawasiliana kati yao, wanalinda koloni lao na kuangalia kizazi hivyo ni sawa na watu ambao wanaishi ndani ya nchi moja (raia).

Kwa mujibu wa Nassor, koo moja ya majimoto haiwezi kuishi na koo nyingine kwenye mti mmoja na ikitokea koo mbili tofauti kukutana hupigana mpaka koo moja ife. Vita mara nyingi huanza pale koloni moja linapoingia kwenye makazi ya koloni jingine na kufananisha sawa na watu waliotekwa wakati wa kuvuka mpaka wa nchi bila ya hati ya kusafiria.

Pia Nassor anasema, majimoto wa koo moja hupandiana wenyewe kwa wenyewe wanaporuka na wanaporudi malkia huanzisha koo nyingine ambayo haiwezi tena kuwa rafiki na koo waliyozaliwa.

Anasema taaluma ya matumizi ya majomoto katika kudhibiti visumbufu vya mikorosho, michungwa na miembe imeanza kueleweka, kukubalika na kuigwa na mtu mmoja mmoja pamoja na vikundi.

Kwa upande wa zao la korosho, kikundi cha Masasi High Quality Farmers Products kilichoanzishwa mwaka 2007 kwa kuwashirikisha wakulima 840 kutoka vyama tofauti vya kilimo hai (organic farming) wa zao la korosho kutoka vijiji sita wilayani humo ambavyo ni Chiungutwa, Maugura, Temeke, Mpindimbi, Mwena, na Chakama vimeweza kuiga teknolojia hii na faida zimeonekana, anasema na kuongeza: Kundi hilo limekuwa likiendelea vizuri na kutokana na mafanikio waliyoyapata, wakulima zaidi wamekuwa wakijiungana na hadi kufikia mwaka 2013 lilikuwa na wanachama 1589 kutoka vijiji 12.

Nassor anasema kwa upande wa michungwa wakulima zaidi ya 20 kutoka kijiji cha Semngano wilayani Muheza, Tanga tayari wameanza kutumia taaluma hii kwa kuingiza majimoto katika michungwa yao na tayari wameona na kufurahia faida za majimoto kwenye mashamba yao.

Taaluma hii inazidi kuenea siku hadi siku kwa njia ya mkulima mmoja mmoja kuiga kutoka kwa mkulima mwingine. Kwa zao la maembe tayari wakulima wasiopungua watano wameiga taaluma hii huko Kibaha na kundi la wakulima 20 wanaopatikana Mkuranga wilayani Pwani inaelezwa kuwa waliomba kupatiwa mafunzo juu ya matumizi ya majimoto kudhibiti wadudu waharibifu wa maembe.

Anasema kundi hilo la wakulima 20 lilipatiwa mafunzo hayo na tayari kila mmoja amepandikiza majimoto kwenye mashamba yake na kwamba wanaendelea kuisambaza taaluma hiyo kwa wakulima wengine.

Nassor anasema matokeo ya utafiti wa majimoto yameonesha kuwa yana faida kubwa kwa wakulima hasa wanaofanya biashara ya kusafirisha nje ya nchi mazao kama ya korosho, embe na machungwa kwa sababu mataifa mengi ya nje yanapendelea mazao yasiyozalishwa kwa kutumia dawa aina yoyote yenye kemikali na kwamba gharama yake ni ndogo kulinganisha na mkulima anayelima kwa kutumia dawa zenye kemikali katika kuzuia wadudu waharibifu.

Gharama

Nassor anasema katika utafiti walioufanya, mkulima anayelima kisasa hekta moja ya zao la korosho lenye miti 70 alitumia gharama ya Sh. 846,650 kupandikiza majimoto, ukilinganisha na gharama za madawa zinazofikia Sh 1,225,350 kwa eneo hilo hilo la hekta moja.

Kwa upande wa maembe ambayo yalipandwa kwa nafasi ya mita 10 baina ya mwembe na mwembe, na kuchukua idadi ya miti 100 kwa hekta, gharama za kupandikiza majimoto zilikuwa Sh 404,400 kwa hekta na gharama za madawa zilikua Sh 1,092,000 kwa hekta.

Hata hivyo, gharama hizi zinatofautiana kutokana na masafa ambayo majimoto wa kupandikiza hufuatwa kutoka kwenye shamba wanalopatikana,anasema.

Nassor anaendelea kusema kuwa zao lililotunzwa kwa kutumia majimoto kwa mfano embe linaweza kuwa na doti nyeusi kutokana na tindikali inayotokana na majimoto.

Matokeo yaliyofanyika nchini Australia yameonesha kuwa kuna uhusiano mkubwa wa alama nyeusi (dotidoti) zinazosababishwa na majimoto na ubora wa ndani (kiwango cha sukari), embe haiozi haraka na vile vile alama hizo zinaweza kutumika kama kiashiria cha tunda salama na bora zaidi,anasema.

Hata hivyo, Mtafiti Nassor anaelezea changamoto kubwa ya matumizi ya majimoto ni pamoja na kushambuliwa na wadudu wengine kama vile sisimizi ambao hata hivyo hudhibitiwa kwa kupaka gundi chini ya mti unaolindwa na majimoto na kuzuia wadudu wa aina hiyo kupanda kwenye miti.

Njia nyingine ya kukabiliana na changamoto hiyo ni pamoja na kutumia chambo chenye sumu ambayo inakubalika katika kilimo hai (organic farming) kama spinosad. Kwa upande wake Saverina Tiba ambaye ni mfanyakazi msaidizi idara ya utafiti wa majimoto, anasema changamoto nyingine wakati majimoto wanapolelewa kwenye nyumba maalumu ni mashambulizi dhidi ya buibui.

Aidha Nassor anasema baadhi ya wakulima ambao hawajapata elimu sahihi ya matumizi ya majimoto, hudaiwa kuwa na hofu ya kungatwa wakati wa mavuno, lakini anasema hakuna madhara yoyote ambayo huweza kuyapata endapo utangatwa na maumivu yanayotoka na kungatwa ni ya muda mfupi tu. Anasema wakati wa mavuno mkulima anaweza kutumia samaki kwa kuweka chini ya mmea unaovunwa ambapo majimoto huvutiwa na harufu ya samaki na hushuka chini na kuanza kumla samaki huyo na kutoa nafasi kwa mvunaji kuendelea na kazi yake bila kushambuliwa sana.

Njia nyingine ni kupaka poda au majivu mikononi ambayo pia harufu yake humzuia majimoto asiweze kukungata au pia mkulima anaweza kutumia vazi maalum la kujikinga na kungatwa ambalo sio la gharama kubwa,anasema.

Mtafiti Nassor anatoa ushauri kwa wakulima kote nchini kutumia teknolojia hiyo ya majimoto kudhibiti visumbufu vya mazao na kupata soko la uhakika la mazao yao nje ya nchi kutokana na walaji wengi kupendelea mazao yaliyolimwa kwa misingi ya kilimo hai (organic farming) kwa lengo la kulinda afya zao badala ya mazao yaliyolimwa kwa kutumia dawa za sumu ambazo zinaharibu mazingira, kuua viumbe visivyokusudiwa pamoja na kuhatarisha afya ya mwanadamu.

Chanzo: HabariLeo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom