Uchaguzi 2020 Majimbo haya yanatakiwa kwa gharama yoyote na CCM

1. Kawe: Namuonea huruma sana Halima Mdee (Gwajima hapendwi lakini ndio mbunge mtarajiwa)

2. Vunjo: Kimei sio mwanasiasa ila alienda pale kwa kuelekezwa tu upinzani unapitaje?

3. Moshi Mjini: Jimbo kongwe la upinzani. Mwenye jimbo lake kafa(Ndessamburo) upinzani unapitia wapi?

4. Hai: Mbowe ni kama kashatolewa lakini kwa sababu mpira ni dk 90 anaona bora amalize tu

5. Arusha Mjini: Maskini Lema anapambana na aliekuwa Rais wa mkoa wake anajua kila kitu kuhusu Arusha.

6. Iringa Mjini: Msigwa amekuwa mwiba sana bungeni kwahiyo anatakiwa asirudi kwa vyovyote vile.

7. Mbeya Mjini: Sugu anapambana na Naibu Spika. Kiutawala tu bungeni nani mkubwa?

8. Tarime zote(Vijijini na Mjini) si rahisi lakini ni lazima wapinzani waachie hata kwa nguvu.

9. Kigoma mjini: ZZK ni mfame pale lakini anatakiwa mtu mpole wa kupiga makofi tu bungeni na kuimba mapambio.

Wapinzani watapita wasiojua kuongea sana na vijimbo vidogo vidogo tu.

Wekeni alama uzi huu halafu baada ya tarehe 28 mtaniambia kuwa mimi sio muongo. Mimi sina chama ila ukweli ndio huo.

Utabili wako umetimia mkuu
 
Back
Top Bottom