Siasa za mbeya: Tulia na Sugu wote wanajikomba kwa CCM ili kushinda 2025

uwe hodari

JF-Expert Member
Dec 16, 2022
3,999
8,387
Sugu aliahidiwa na viongozi wa CCM kuwa atapewa jimbo la Mbeya mjini kwa kuwa akiyekuwepo tulia ni Pro-Magufuli na hawa hawatakiwi bungeni 2025.

Unaweza ukaona hadi Rais, makamo wa CCM na wengine walihudhuria kwenye shughuli ya sugu isiyo kuwa na umuhimu pmj na kusamehewa baadhi ya kodi kwenye hotel yake mbeya.

Kuona vile Tulia naye akaanza kujikomba kwa Rais ili aaminike zaidi na asionekane kama pro Magufuli. Akamgeuka Ndugai ili aaminike zaidi.

Sasa Tulia naye ameaminika kidogo baada ya kusimama kidete kuruhusu kujadiliwa kwa kwa uuzwaji wa bandari kwa waarabu. Na akapewa na safari akapumzike uko uarabuni.

Sugu naye kwa makusudi ameskika kuunga mkono uuzaji wa bandari. Lengo ni kumwonyesha Rais kuwa yupo pamoja naye ili aaminike zaidi.

Kumbe samia ana akili lengo la kuwaweka hawa wanasiasa karibu pamoja na viongozi wengine wa upinzani ilikuwa kuhakikisha atakapoanza kutoa hii mikataba asipate upinzani kwa wanasiasa wasio CCM kwa kuwa ndani ya ccm hakuna wa kuunguruma kwa kuogopa kupoteza ubunge 2025.

Ukiangalia hawa wabunge wote wawili hakuna anayewaza maendeleo ya mbeya wanawaza matumbo yao tu.

Kutokana na hilo kumeibuka kundi linataka mbeya igawanywe iwe majimbo mjini mawili ili Sugu na tulia wote warudi bungeni 2025.

Najiuliza tu inamaana mbeya hakuna watu wengine wenye uwezo wa kuongoza ukiwaacha hawa sugu na tulia wanaoonekana wanajali maslahi yao tu?
 
Back
Top Bottom