Tunategemea wilaya ndio yawe majimbo ili kila jimbo ligombewe na mwanaume na mwanamke ili moja kuondia viti maalum, pili kupata 50-50% ya uwiano. Pili kuondoa by election iwapo mbunge atafariki atabaki mmoja kuondoa gharama za by election. Hivyo majimbo yatakuwa re defined kwa muundo wa wilaya kwenye katiba mpya na kila chama kitasimamisha wagombe wawili kwa wilaya zilizopo x 2 ni idadi ndogo kuliko idadi ya wabunge iliyopo
Mwigulu, huu utaratibu wa kuwa na mgombea mwenza unanipa shida sana, I don't know how much thought went into it lakini naamini haitachukuwa muda mrefu tutajikuta tunakaa chini na kuangalia tena upya mfumo wa bunge (kama utapitishwa).
Kwanza, najiuliza, mfumo wa mbunge-mwenza utaleta manufaa gani hasa kwa mwananchi wa kawaida tofauti na mfumo wa mgombe mmoja? Na kama tunasema ni kwa ajili ya kuwa na wabunge wanawake maana yake tunakubali kuwa wanawake wa Tanzania hawana uwezo wa kugombea bila ya kubebwa! This is a set back kwa wale wale wanaopigana na mfumo dume. Hivi hakuna namna nyingine yenye staha ya kuongeza uwakilishi wa wanawake bila ya huu wa mbeleko? Mbona Rwanda wameweza, sisi tunashindwa vipi?
Labda niongeze, kwasasa hivi uwakilishi wa wanawake bungeni ni 30%. In theory inaonekana tumepiga hatua. Lakini hebu tujiulize, wanawake wa Tanzania wamepata unafuu gani wa maisha kutokana na ongezeko hili la uwakilishi bungeni? Mfano mdogo tu, kwenye wards wa kujifungulia, kuna tofauti yoyote itokanayo na ongezeko la wanawake bungeni? Vipi sheria ambazo wanawake - nje ya bunge- wamekuwa wanazilalamikia, zimebadilishwa tangu wabunge wanawake waongezeke bungeni? mfano sheria ya mirathi, kuna tofauti yoyote? Domestic violence against girls/women, kuna unafuu wowote?
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba tusigeuze bunge kuwa x'mas tree, kwamba watu wanakwenda bungeni ili kupendezesha muonekano. Tujikite kwenye uwezo. Kama mtu ana uwezo, ana uwezo. Na kama hana, maana yake hana. Kuwa number mbili hakumfanyi mtu asiye na uwezo akawa nao! We really have to be realistic about this otherwise tutajikuta tunapeleka resources kwenye mambo yasiyo na tija. Pia, sidhani kama ni mfano mzuri (role model) kwa girls kuona mama zao wanapata nyadhifa kwa sababu tu gender!
Pili, Jambo moja ambalo kila mwanadamu ana uhakika nalo ni 'kifo'. Kila mtu atakufa -kwa hakika. Sasa sijui how effective huu utaratibu wa wagombea wawili kwenye mambo ya vifo? Hivi ikitokewa wawakilishi wote wawili wakafa kwa pamoja inakuwaje? Au kama amefuka mmojawapo, huyo mwingine aliyebakia ataongoza bila ya kuwa na 'mwenza'? Na kama atateuliwa mtu mwingine kuungana naye, ni utaratibu gani utakaotumika kumpata replacement wa marehemu ambao hautakuwa wa gharama kama iliyosasa? Kama upo utaratibu wa namna hiyo - usiokuwa wa gharama kubwa - ni kwanini kuingia gharama ya kuwa na wawakilishi wa wawili in the first place?
Mpaka hapa nadhani unaweza kuona kuwa hii theory is foundamentally flawed.
Sijui kama katiba mpya itaruhusu mgombea binafsi katika ngazi ya ubunge, lakini kama hakuna mabadiliko ni kwamba mbunge lazima awe mwanachama wa chama cha siasa. Kama ndivyo, tafsiri yake ni kuwa wananchi wanapomchagua mbunge maana yake wamekubaliana -si tu na uwezo wa mgombea peke yake - bali pia, watakuwa wamechagua sera za chama anachowakilisha. Kwa maana hiyo, (maoni yangu) ikitokea kifo, chama cha marehemu kiruhusiwe (kisheria) kuteua replacement bila ya kuwa na uchaguzi. Kwangu mimi hii ni sensible way kama kweli tunataka kuwa na 'lean' legislative branch.
Tatu, unapokuwa na wabunge wawili kwenye jimbo moja, chain of command inakuje? Na nani anafanya nini? Ikitokea mmoja wa hao 'double' anafanya kazi chini ya viwango, wananchi wanaweza kumuondoa yeye peke yake, au ataondelewa na mwenziwe? Nasema hivi kwa sababu moja ya mambo yanayotajwa na wananchi wakati huu wa kukusanya maoni ya katiba mpya, ni mamlaka ya wapiga kura kumuondoa mbunge mzembe. Tumeona matatizo kwenye mawizara (Waziri vs Naibu wake), kwenye ngazi ya ubunge how do you handle things (a) kama wawili hawa hawaonani eye to eye na (b) mmoja hafanyi kazi kama inavyotakiwa. Unamuondoa mmoja au wote wawili? Na kama unamuondoa mmoja, again, huyo aliyebaki atawakilisha jimbo peke yake au atateuliwa replacement wa yule mzembe?
Nne, kugeuza Wilaya kuwa jimbo nako kuna walakini. Hatuna uwiano mzuri kati Wilaya na Wilaya; hapa naongea watu, geography, mahitaji, etc. Mfano Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam haziwezi kuwa sawa na Wilaya za mkoa wa Katavi. Au Wilaya za Mkoa wa Mwanza haziwezi kuwa sawa na Wilaya zilizoko Pemba. Kwa maana hiyo, ile 'haki' ya equal representation inakuwa imeminywa kwa baadhi ya jamii sababu variables zilizotumika kupata jimbo zimepewa uzito unaolingana japo mazingira ni tofauti.
Kwangu mimi sidhani kama Wilaya ni njia nzuri ya kupata jimbo. Tunatakiwa tuwe na vipengele vingine ili kutoa haki sawa kwa kila eneo. Na maadam tunaandika katiba mpya, basi tuangalie hili beyond politcs, tumalizane na habari ya majimbo mapya kila kukicha kwa kuweka 'permanent' framework.