Uchaguzi 2020 Majigambo ya Wana-CCM kuwa Wapinzani hawataambulia chochote: Napata hisi watapa pata pigo kubwa na takatifu litalofuta kabisa ndoto zao na tegemeo lao

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Hivi sasa ni kawaida kusoma au kusikia maoni ya wana-CCM kuwa wapinzani katika uchaguzi mkuu wa baadae mwaka huu hawatapata chochote huku wakiwalenga zaidi CHADEMA na kwa kiasi fulani ACT-Wazalendo.

Kuhusu NCCR, kila mwenye akili anaelewa nini kinaendelea na ndio maana huwasikia wakiishambulia NCCR wala kusema itakufa kama wasemavyo kuhusu CHADEMA kuwa inakwenda kufa.

Binafsi, hisia zangu zinaniambia hawa watu wanaweza kupata pigo kubwa sana litakoloondoa kabisa matumaini yao na tukawa na mwanzo wa mabadiliko makubwa tofauti na wao wanavyoamini.

Ukweli ni kwamba,wenzetu hawa majigambo yao yanatokana na kuamini katika nguvu za mtu mmoja ambae wanasahau nae ni binadamu tu kama wengine na wanasahau kabisa hakuna aijue kesho.

CCM hawa majigambo yao hayana tofauti na majigambo ya washabiki wa club ya soka ambao kiburi chao msingi wake ni timu yao kuwa na mfadhili anaefanikisha mafanikio ya club yao na ambae akiamua tu kujitoa,club hiyo ndani ya muda mfupi inarudi ground zero kwasababu ilitegemea mtu mmoja pasipo kujiongeza(kuwa na Plan B).

CCM hii ya leo ambayo wafuasi wake wanajipiza kushinda uchaguzi huku wakisema upinzani unakwenda kushindwa vibaya na kwamba hawatapata mbunge hata mmoja(wakiwalenga zaidi CHADEMA),hawajawekeza kabisa kwa wananchi wa kawaida zaidi ya kutegemea mbinu hizi wanazotumia na kama walivyofanya mwaka jana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Tegemeo la hawa wenzetu ni mtu mmoja kuwabeba na ikitokea mtu huyo hayupo kwasababu yoyote ile,hakika wanakwenda kuanguka vibaya sana kwani sidhani kama hata wana Plan B zaidi ya kutegemea nguvu za mtu huyo mwenye roho ngumu ambae nae ni binadamu tu kama mimi na wewe na ambae nae haijui kesho yake.

Majigambo ya wenzetu hawa hayana tofauti sana na yale waliokuwa nayo wana-Simba ya kuifunga Yanga wakasahau mpira unadunda na kilichotokea hawakuamini pale walipotandikwa moja bila majibu(nimelazimika kutoa mfano huu ili nieleweke hivyo watani mtanisamehe).

Hivyo,nawashauri wenzetu hawa waache kumtegemea mwanadamu kuwa atawavusha bali nawashauri wamuombe Mungu huyo mtu ambae ni tegemeo ili lolote lisilo jema likatokea vinginevyo wanakwenda kupata anguko baya sana.

Miezi mitano kuanzia sasa mpaka siku ya uchaguzi bado ni muda mrefu sana kibinadamu hivyo tusijisahau sana kwani hakuna mwanadamu aijue kesho hivyo msiwekeza kwa mwanadamu mwenzenu kama cha cha siasa bali mjikite kuwa karibu na wananchi ili yoyote akisimama kwa kofia ya chama chenu, chama kimbebea kwasababu mmefanya yale wananchi wayatakayo na si kutegemea binadamu ambae hana uhakika hata wa kesho yake.

Na jambo la mwisho ni kuwa,huyo mnaemtegemea kuwababe muda wake ukaisha huku mkiwa mmesahau shida na matatizo ya wananchi na ikatokea atakaemrithi asiwe na hulka kama zake,mmejiuliza nini kitawapata?


Kazi kwenu.
 
Mtabiri mkuu wa JF katoa unajimu adhimu juu ya kitakachotokea Kama Lwakatare atamwaga mboga, tusubiri mboga imwagwe ili ule msemo unaosema mtu mzima akivuliwa nguo huchutama utakapotimia
 
Back
Top Bottom