Majigambo ya wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majigambo ya wabunge

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Felixonfellix, May 13, 2010.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Katika jimbo fulani kuna bango linalomnadi mbunge wa sehemu hiyo hivi: Baadhi ya misaada mbalimbali niliyotoa kwa wanajimbo langu binafsi:
  1. Nilisaidia upatikanaji wa majeneza pamoja na kusafirisha marehemu toka wilaya yangu waliopata ajali ya treni huko Dodoma na kushughulikia majeruhi kwa kuwawahisha hospitali ili kupata matibabu ya haraka.
  2. Nilifanikisha uletwaji wa mwili wa marehemu Mathias Kasoso toka Dar es Salaam. Nilisaidia sana uwezekano wa usafiri wa ndege pamoja na usafiri wa gari wa kutoka uwanja wa ndege kwenda alikozikwa.
  3. Nilitoa baiskeli kwa mlemavu wa .... yenye thamani ya Tsh. 60,000 na Sh. 00,000 kumnunulia mlemavu mwingine baiskeli ya gurudumu tatu.
  4. Nilimsaidia Mama mtu mzima kupata haki zake Dodoma zilizokuwa hatarini kupotea bure
  5. Nilimsaidia Salehe na rafiki yake (Sh. 40,000) nauli ya kutoka Dar es Salaam. Walikuwa wamekwama Dar es Salaam.
  6. Niliwasafirisha vijana wawili kutoka jimboni mwangu waliokwama Dar baada ya kudanganywa waende Dar es salaam wangepatiwa ajira.
  Baada ya kutaja michango yake mingine, tangazo hilo la mbunge lilimalizia hivi: “Nina hakika nimetoa michango mingine mingi kwa wanajimbo na kwa watu wengine pia ambao hawatoki jimboni mwangu.. Nyinyi ndiyo mtanikumbusha mengine niliyoyasahau.”
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  kwa kweli hapa Padre Karugendo aliniacha hoi kwenye hiyo article yake ya kwenye Raia Mwema nikicheka sana na kusikitikia wadanganyika.
  Lakini pia hiyo ndiyo picha kamili ya wagombea ubunge wetu walivyo. Wao ni wahisani si wawakilishi.
   
Loading...