Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,997
- 20,329
Nimelazimika kujibu uzi wa mzee wangu na mwalimu wangu katika historia bwana Mohamed Said katika uzi wake huu Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya
Ndani ya uzi huo anasema kuwa "nafasi ya president wa TANU nafasi ile ilikuwa ya Chief Kidaha Makwaia lakini alikataa ndipo bahati ikamuangukia Julius Nyerere"
Mimi nimeamua kumjibu kwa kutumia andiko, Sura ya Pili, ukurasa wa 207 katika Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, kinaeleza kwa undani suala hili, nanukuu kama ifuatavyo:
"Mkataba wa Versailles ulianzisha aina mpya ya maeneo yaliyowahi kuwa ama koloni au majimbo ya nchi zilizoshindwa katika vita. Koloni zote za Ujerumani pamoja na sehemu kubwa ya majimbo ya Milki ya Osmani ya awali ziliwekwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa na kukabidhiwa kwa nchi washindi wa vita. Zilipewa hali ya pekee kama maeneo ya kudhaminiwa. Tofauti na koloni za kawaida nchi wadhamini hazikupewa mamlaka yote jinsi iliyokuwa katika koloni zao za kawaida bali zilipokea maeneo ya kudhaminiwa chini ya masharti fulani pamoja na kulinda haki kadhaa za wenyeji na KUZIANDAA nchi hizi kwa uhuru.
Hapo mwanzoni tofauti kati ya koloni na eneo la kudhaminiwa haikuwa kubwa lakini baadaye masharti ya udhamini yalikuwa muhimu. Kwa mfano hali ya Tanganyika kuwa eneo ka kudhaminiwa ilisababisha Uingereza kutokukubali walowezi wengi kuja Tanganyika. Vivyo hivyo hali ya Afrika ya Kusini Magharibi kuwa eneo la kudhaminiwa ilizuia sehemu hii kuwa jimbo la Afrika Kusini na kuwa msingi kwa uhuru wake kama nchi ya Namibia.
Jukumu la kuandaa nchi hizo kupata uhuru kwa sehemu kubwa liliratibiwa na shirika la kijasusi la kanisa Katoliki la Jesuiti kwa ustadi mkubwa bila baadhi ya makoloni kujua, lakini lilikumbana na kikinza kutoka katika shirika la kijasusi la Fabian Sociaty lililokuwa linamilikiwa na Umalkia wa Kiingereza ambalo nalo lilikuwa na jukumu la kuratibu uhuru wa Afrika katika makoloni ya Uingereza, mgogoro huo ulikuzwa kwakuwa Anglikana nao tayari walikuwa wameanza kumuandaa Chifu David Kidaha Makwaia kukabidhiwa uhuru na kuwa rais wa kwanza Tanganyika, maandalizi yote yakiratibiwa kupitia taasisi yao ya Fabian Sociaty iliyokuwa maalumu kwaajili ya kuwaandaa vijana wa kiafrika kukabidhiwa nchi zao.
Barani Afrika Jesuiti ilibadili mbinu kwakuwa dola la Kiingereza lilikuwa kikwazo kwa sehemu fulani, haikujikita kwenye dola isipokuwa ilisimama katika muundo wa shirika likifanya shughuli zake ndani ya Kanisa. Dhamiri ilikuwa lazima itimie, kama ilivyosemwna huko mwanzo kuwa hawa ndio wabobevu wa elimu ya juu kwa kila nyanja na ndio wanaotawala ulimwengu, hivyo vikwazo havikukwamisha wao kufikia malengo. Mwisho Malkia wa Uingereza aliamua kuungana tu na Jesuiti ili Julius Nyerere apewe nchi.
Katika Tanganyika chini ya Udhamini wa Jumuiko la Kimataifa, kulikuwa na harakati za hapa na pale za kudai haki za kiraia kwa wenyeji. Ifahamike kuwa vyama vya harakati hizo Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe.
Mwaka 1927 hadi 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12 februari 1929 Zelger alistaafu wadhifawake kwa lazima. Ni mwaka huohuo wa 1927 ndio Chama cha African Assosiotion (AA) kilianzishwa na Gavana Sir David Cameron maaluma kwaajili ya kuratibu sherehe za watu weusi huko pembeni ya mji huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na kuwapa ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa.
Lakini historia ya Tanganyika haiwataji waasisi wa AA, Rais wa kwanza Mwalimu Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za mjerumani kutoka kabila la Wayao), katibu mkuu wa kwanza Klest Sykes (Mzulu Baba yake alikuwa mateka wa kikoloni toka Afrika Kusini), Mwekahazina Ali Ramadhan (mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania).
Hao ndio mwaka 1927 waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933 Mwalimu Cesil Matola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho bwana Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948 yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest aliyeitwa Abdulwahid Sykes huyu alikuwa ametoka kupigana vita vya pili vya dunia huko Burma, na aliporudi alikuwa na mawazo ya ujana toka vitani, akampindua baba yake kwa kumpiga ngumi puani, mapinduzi yaliyoitwa “ondoa wazee”.
Kisha AA ikabadilishwa jina na kuitwa TAA, Rais wake wa Kwanza akawa Dr Vedasto Kyaruzi (Mhaya), huyu ndie dakitari wa binadamu wa kwanza kabisa wa kiafrika Tanganyika, Katibu mkuu akawa Abdulwahid Sykes na Mweka hazina akawa Dosa Azizi, utawala huo ulienda mpaka mwaka 1953 uchaguzi ulipofanyika na Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo Mnazimoja leo, mwaka 1954 Nyerere akabadili jina la chama na kuwa TANU jina ambalo lilibuniwa na Abdulwahid Sykes, TANU ilikwenda mpaka mwaka 1977 na kisha kikazaliwa chama kiitwacho CCM baada ya Muungano wa ASP na TANU".
Dowload hapa chini sasa..
Amazon.com: Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi (Afrikaans Edition) eBook: YERICKO NYERERE: Kindle Store