Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 267
- 583
Ndugu Watanzania!
Serikali ya Tanzania, kupitia Supplement Na. 30 imetoa Tangazo la Serikali Na. 673 la 2/9/2024 la kufuta Kata 11, Vijiji 25 na Vitongoji 96 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro katika Mkoa wa Arusha. Kuna taarifa kuwa nyaraka hii inayosambaa mitandaoni kuanzia leo asubuhi imetoka katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kama ni hivyo, basi inahitajika hekima kubwa ili kutatua Mgogoro wa Ngorongoro kwa sababu Wamaasai wanaoandamana kule Ngorongoro wanajiona kuwa wao ni wananchi na wakazi wa Ngorongoro wakati Serikali kupitia Tangazo la Serikali, inaona Ngorongoro hakuna wananchi, hakuna makazi; hakuna Kata, Vijiji na Vitongoji.
Tafsiri ya Tangazo hilo ni pana kwani kuanzia tarehe ya Tangazo hilo watu wote waishio kule Ngorongoro wako kinyume cha Sheria na hivyo hakuna huduma ye yote watu wa Ngorongoro wanaweza kupata kutoka Serikali - maji, shule, hospitali, mahakama, polisi, barabara, umeme, nk. Ina maana kuwa huduma zote zinatakiwa ziondolewe kuanzia tarehe ya Tangazo hilo.
Ni jambo la kushangaza kuwa Serikali iliamua kutoa Tangazo hilo wakati muafaka haujafikiwa kati ya Serikali na wananchi wa Ngorongoro. Lakini je, Serikali ina mamlaka gani kisheria na kikatiba kukuwaondoa wakazi wa Ngorongoro?
Soma Pia: Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673
Kabla ya Ukoloni, nchi yote hii ambayo baadaye ilikuwa sehemu ya Tanganyika ilikuwa katika mkusanyiko wa nchi mbalimbali. Wakoloni wa Kijerumani na baadaye wa Kiingereza walijua ukweli huu na walitawala shirikisho la nchi hizo na waliendelea kuitambua mipaka ya nchi hizo.
Kwa hiyo kulikuwa na Nchi ya Wachaga, Nchi ya Wahehe, Nchi ya Wanyakyusa, Nchi ya Wasambara, Nchi ya Wamaasai, Nchi ya Wasukuma, Nchi ya Wazaramo, nk.
Wakati wa kudai Uhuru wa Tanganyika, Rais wa TANU ambaye alikuwa Julius Nyerere alifanya ziara katika nchi nzima akikutana na watawala wa nchi hizo kuwashawishi waungane kumtoa mkoloni ambaye alikuwa ni Mwingireza. Moja ya makubaliano ambayo Nyerere aliyafanya na watawala wa nchi hizo ni kuomba baadhi ya mamlaka ya watawala wa nchi hizo kuachiwa TANU na Serikali yake.
Alipofika Kyela na sisi Wanyakyusa tulitoa au tuliachia baadhi ya mamlaka hayo kwa TANU na Serikali yake. Ndio maana watoto wengi wa machifu miaka ya mwanzo walipewa madaraka serikalini kwani hiyo ilikuwa pia ni sehemu ya baadhi ya makubaliano baada ya kuchukuliwa nafasi zao za kutawala. Kumbukumbu zetu pia zipo Julius Nyerere alipofika Kyela na kuonana na Chifu Korosso Mwamakula wa nNkilwa kule Kajunjumele kabla ya Uhuru.
Moja wa mambo ambayo Askofu Mwamakula alielezwa wakati anakuwa ni juu ya mkataba au makubaliano ya kukabidhi mamlaka ya Himaya au Milki ya Mwamakula kwa TANU chini ya JK Nyerere. Kuwa Mbunge wa kwanza wa Kyela kuwa ni Mchungaji Chifu Makilini Mwakalukwa Mwamakula haikuwa ni jambo la bahati mbaya. Pia, Mzee Mrisho Kikwete (Baba yake Jakaya), Chifu Adam Sapi Mkwawa, Chifu Abdalah Said Fundikira, Chifu Anderson Mwakalinga na watu wengine kupewa madaraka wakati wa utawala wa Nyerere haikuwa ni bahati mbaya. Ilikuwa ni namna ya Nyerere kuwaweka karibu watoto wa watawala wa nchi zilizounda Tanganyika ili nao wasije wakaasi na kudai nchi zao zijitoe katika Serikali ya TANU.
Lakini baadaye, kwa njia ya ujanja ujanja, bila ya kuwashirikisha kikamilifu watawala wa nchi husika, ilifuta mamlaka ya uchifu. Watawala wa nchi hizo hawakuwa wameafiki wote lakini kwa kuwa TANU ilikuwa na Jeshi na kwa kuwa pia walimheshimu na kumuamini Julius Nyerere na TANU; hawakuweza kuanzisha migogoro na Serikali ya TANU. Hata hivyo, lile vuguvuvugu la kutaka mamlaka za tawala za jadi zirejee kama bado halijawahi kukatika. Uganda ilisharejesha mifumo hiyo kisheria ingawa sio kwa kiwango kikubwa.
Baada ya kueleza historia hiyo, ni wasilisho letu kuwa Serikali ya CCM ni mtoto wa Serikali ya TANU. Serikali ya CCM inapaswa ikumbuke ya kuwa TANU ilikuwa na makubaliano na jamii au mamlaka za nchi zilizokuwa Tanganyika wakati ule. Kuondoa kwa lazima watu katika makazi yao ya asili haikuwemo katika makubaliano yetu (mamlaka za jadi na TANU).
Ndio sababu Operesheni ya Vijiji vya Ujamaa ilishindwa na kufeli kwa kuwa Serikali ya TANU iliyakiuka pia makubaliano (rejea kusoma kitabu 'Ujamaa Utafaulu'?). Kitabu hicho kinaeleza sababu za kufeli kwa vijiji vya Ujamaa ni kwa sababu watu hawakutaka pia kuhama katika maeneo na nchi zao. Ramani na mipaka ya Vijiji vya Ujamaa havikuzingatia mipaka na tamaduni za watu katika nchi zao.
Kama yalivyo makubaliano yote duniani kuna wakati mashirikisho, makubaliano, muungano na falme huanguka na nchi zilizounda hayo pia hurudia mipaka yake ya asili. Rejea shirikisho la Yugoslavia, Urusi, Chekislovaki, Uingereza, nk ambako mashirikisho yalivunjika na mipaka ya zamani ikarejea zikatokea nchi za Ukraine, Czech, Macedonia, Ireland, Serbia, nk. Mfano mzuri Afrika ni iliyokuwa Sudan, ikagawika na kuzaliwa Sudan na Sudan Kusini; Ethiopia pia ikagawika na kuzaliwa Elitrea na Ethiopia.
Ni kwa mantiki hiyo, kihistoria na kimkataba, Serikali yeyote inayotawala nchini Tanzania haina mamlaka ya kuhamisha watu waliokuwa ni sehemu ya nchi zilizounda shirikisho la nchi za Tanganyika kwa makubaliano maalum na TANU. Serikali inahitaji kufanya makubaliano na jamii husika ndio iwahamishe watu hao.
Sisi Askofu Mwamakula tumeona tuandike hili ili tuingie katika kumbukumbu kuwa tulishauri, tulionya na tulitahadharisha. Tuko tayari kwa yo yote yatakayotupata kwa kusema ukweli wetu katika nchi ambayo watu wanaogopa kuusema ukweli wanaoujua kwa sababu ya kuogoa sana kutekwa na kupotezwa!
Je, kama ikitokea Muungano wa Tanzania nao ukaja kubadili muundo, hiyo nchi ya Wamaasai itakuwa na mipaka gani? Ni kwa nini tusizame katika kujifunza historia ya dunia na ya kwetu ili kuimarisha Muungano wetu? Kama katiba yetu inamtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ashauriane na Rais wa Zanzibar pale anapotaka kugawa mipaka ya Zanzibar, ni kwa nini tusianze kufikiri kufanya hivyo kwa taifa la Wamaasai pia ambao sote tunakubaliana kuwa wana utamaduni na historia ya kipekee kama ilivyo kwa Zanzibar? Je, Australia haijatunga Sheria maalum ya kulinda mipaka ya watu wale walio wa asili kabisa walio na tamaduni pekee?
Sheria haiwezi kuwa juu ya katiba na pia katiba haiwezi kuwa juu ya makubaliano. Kama katika yale tuliyokubaliana na TANU hayakuingizwa katika katiba yetu basi ni lazima yaingizwe ili kuepuka kuwa na katiba iliyopora haki za watu. Katiba ikipora haki za baadhi ya makundi basi ni dhahiri kuwa katiba hiyo haitaheshimiwa na watu hao na isipoheshimiwa nao kutakuwa na migogoro. Tunataka tuwe na katiba ambayo pia sote tutaiheshimu na ambayo itazihifadhi na kuzilinda haki zetu sote.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 20 Agosti 2024; saa 3:24 asubuhi