Majibu yanatokaje?!

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,328
23,879
Habari zenu wakubwa,
Naomba kuuliza..hivi kama ume-apply kazi mahali, unapataje habari kama umechaguliwa?
Mfano; kama tangazo lilitolewa gazetini..je ni kwamba watapost kwenye gazeti majina ya watu walioitwa kwenye interview? au watakupigia simu? au barua pepe?
Au kwa kuwa barua yangu niliituma posta, je na majibu yatatumwa posta vilevile?
na ni baada ya muda gani nisubiri? maana mengine hayakuwa yamesema labda, "usiposikia kutoka kwetu in two months ujue haujachaguliwa!"
Vitu kama hivyo..natanguliza shukrani!
 
wanaweza kufanya vyovyote wapendavyo...ajira za serikali na mashirika ya umma mara nyingi wanapenda kutuma barua na kutangaza magazetini. Mashirika binafsi mara nyingi wanapendelea simu na email.... Pia ni wajibu wako mwenyewe kufuatilia ikiwezekana ukapiga simu kuuliza kama waliotuma maombi wameishakuwa shortlisted.... Kila la heri
 
Duh..sasa mbona nyingine sikukopi hata namba za simu aisee..anyway, shukrani for the info! will look into dat...:decision:
 
duh..sasa mbona nyingine sikukopi hata namba za simu aisee..anyway, shukrani for the info! Will look into dat...:decision:

we mento kumbe una utani hata kwenye mambo muhimu?
Utaandikaje barua ya kuomba kazi usiweke contact zote?
Hapo ndipo unaponiacha hoi haswa nikikumbuka matani yako.
 
Kwa kifupi usipopata habari yoyote ujue haujapata kazi.
 
Back
Top Bottom