Kuna watu wana "powers" kama ma Sharifu!. ukimtibua akakasirika, yatakukuta ya kukuta!.
1. Alipoanzisha ITV akatishiwa na DTV. Mmiliki wa DTV Shabir Dewji aliswekwa 'ndani!'. Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani wakati huo, Silvanus Adel alipoingilia tuu, 'alimwaga unga!'.
2. Kwenye ule 'mchezo mchafu' wa Kilimanjaro hotel, Masilingi alipayuka sana!. Kapoteza ubunge na kapoteza uwaziri he is nobody now!.
3. Alipogombana na Masha, Masha kapoteza ubunge, kapoteza uwaziri, he is nobody now!.
4. Alipogombana na Rostam Aziz kwa kumuita 'Fisadi Papa!' na alipomjibu yeye ni 'fisadi nyangumi!', Rostam kapoteza ubunge, kapoteza biashara zote, kaikimbia nchi!. Kampuni zake zote zinapumulia mashine!.
5. Alipozozana na Yusuph Manji, Hivi sasa Manji anaelekea kufilusika!. Ameuza kila jengo limebaki jina tuu!.
6. Kile kipibdi cha 'Kiti Moto' kilikuwa OK kilipokuwa Channel Ten, Mzee akakinunua kwa dau kubwa na kukihamishia ITV . Alipotaka kuingilia 'contents', alitofautiana na mwendeshaji kipindi kilikufa mpaka leo mwendeshaji yuko juu ya mawe!.
7. Alipotofautiana na Tido kuhusu Kombe la Dunia na UK premier league!. Tido alipoteza kazi!.
8. Alipotofautiana na Mhariri Mkuu wa Guardian, Vumi Urasa, he lost his job and lost his life!.
9. Alipotofautiana na Mhariri Sunday Citizen, Sakina Datoo, Sakina lost her job and she is nobody now!.
10.Yule Mzungu Sarah Harmitage alimsema vibaya kumuunganisha katika sakata la 'Silvadale Farm', she has lost everthing and lost all the cases!.
Kuna watu ukiwatibua, utaishia ku loose!.
Mifano hai ipo!. Sasa ni zamu ya Prof. Muhongo!. Msubirieni tuu, siku zake zinahesabika!.
Pasco.