Majibu ya mgombea ubunge chalinze kwa cuf kuwa sio raia

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
kwanza labda niweke sawa zile fomu hakuna sehemu ambayo inasema uambatanishe na vielelezo vya shughuli unayofanya kama yeye alivyosema’
‘Kiuhalisia mimi ni mfanyabiashara wa siku nyingi nafanya biashara na maduka ya nyama, kuhusu kughushi sahihi ya wadhamini hili ni suala ambalo sio la ukweli kwa sababu wakati tunarudisha fomu ilihakikiwa na mkurugenzi ambae ndiye msimamizi wa uchaguzi, sio saini za mkono peke yake zipo za dole gumba na zipo mchanganyiko na tunazo pia zile shahada za wapiga kura, tulifanya uhakiki na shahada zenyewe hivyo mkurugenzi alihakiki na kusema zipo sawa sawa’
‘Kuhusu kusema kuwa mimi sio Mtanzania hilo suala sio la kwangu, nafikiri wanalo uhamiaji au wanalo wenyewe C.U.F mimi ni Mtanzania halali na ninacho kitambulisho cha kupigia kura ambacho nafikiri watanzania wengi ndio wanakitumia’
Kuhusu kusoma na kuandika mgombea huyu amesema ‘fomu nilizijaza mbele ya Mkurugenzi na yeye mwenyewe aliona nafanya kazi hiyo hata katiba yetu inasema kwamba ni kujua kusoma na kuandika, swala la Kiingereza na Kiswahili ni swala la kuchagua lugha unayoiweza na mimi nikachagua Kiswahili kwa sababu ndio lugha ninayoiweza’
 
Huyu mbunge anazidi kunipa wasiwasi na uraia wake pamoja na uwezo wake inaonekana nimdogo sana, lakini siwezisahangaa sana sababu wengi wa chama hicho wanafanana!!
 
Back
Top Bottom