Majibu ya kisayansi: Lowassa na Sumaye!

TeamLowassa

JF-Expert Member
Nov 30, 2013
1,495
936
Hawa jamaa wana majibu ya kisayansi sana!

Lowassa:


Eti nilikuwa mojawapo ya list of shame! Hata kama ingekuwa kweli, hiyo list ilikuwa na watu wangapi, mimi ndio niko upinzani nashambuliwa hao wengine wako wapi? Tusonge mbele, mabadiliko ni lazima
Edward Lowasa.

Sumaye:

Amesema ni kweli nina shamba ambalo nimelinunua kwa kiinua mgongo changu baada ya kustaafu
Mm sina ela ya kujenga maghorofa nankuwekeza kwenye miradi mikubwa

Nimeamua kuwa mkulima sasa wanasema mwingine anafuga ng'ombe eti ni ufisadi

Je walitaka tufanye kama kinana kuua tembo au familia ya Jk waliokwapua ela za escrow.hili tuonekane waadilifu

Nimeipenda
 
Hawa wazee watawauwa Ccm,Naona mpaka Makamba mzee wamemtoa pangoni lakini kaishia kupata aibu
Mpango wa mungu hauziiliki kwa vihoja vepesi,El ni chaguo la mungu na ikulu anaingia.
 
Walutheri hao katika ubora wao dhidi ya waislam! Haya yetu macho


hii ni hatari sana,.....na haya ndiyo mawazo ya kukurupuka kwa wanaukawa (chadema) wengi...sasa sijui hawa waumini wa dini hii wametajiwa nini hapa....na wenyewe sijui watakuwa na tafsiri gani? na mwisho hiyo tafsiri sijui itamnufaisha nani kt ya pande hizi mbili?...kinachonishangaza zaidi, chama chenye mlengo fulani wa waumini tajwa kipo kwenye umoja huo unaoitwa ukawa. na vitendo kama hv visivyo na hata chembe ya matumizi ya akili, utashangaa baadaye mijitu inalalamika....oh, tumeibiwa kula! imani yangu ni kuwa, watu tunaowaona kwenye mikutano ya kampeni hii, ni wachache sana ukilinganisha na ambao hawafuatilii viwanjani na badala yake wanafuatilia wakiwa majumbani na mitaani. na wengi wa watu hawa ndiyo wale ambao zaidi huzama kwenye hoja, na siyo ushabiki au mkumbo km hawa wa viwanjani. sasa maneno yasiyo na maana km haya....shauri yenu. oktoba siyo mbali....
 
Walutheri hao katika ubora wao dhidi ya waislam! Haya yetu macho


Hata wawe dini gani, MABADILIKO NI LAZIMA. Dawa imeshaanza kukolea, ndio maana mmemfumua mzee makamba kutoka pangoni aje kujaribu kuokoa jahazi. Na ndio maana mnaanza kutumia kete/karata ya udini sasa. Mtashika kila tawi, hamtafanikiwa - kwani siku ya kuanguka nyani matawi yooote huteleza.
 
Mzee Makamba katoka pangoni kuja kummaliza Sumaye kumbe kampalia mkaa Kinana, huyu Mzee akikumbushiwa issue zake enzi za Ualimu si atachanganyikiwa?
 
Back
Top Bottom