Majibu ya Kigwangalla: Utatuzi wa Ajira kwa Vijana wa Tanzania?


Ops,...nilitaka kutoa maoni yangu lakini kumbe una conclusion tayari?
Sasa unataka maoni ya nini kama unajua watanganyika hawataki mawazo mapya?
Well,...
Iambie serikali iongeze shule za kata ili kuwe na walimu wengi.
Iongeze magari ya UDA ili makonda waongezeke,...
etc,etc maana hayo ndo mawazo ya "zamani" na wanayo penda watanganyika.
 

Pamoja na kwamba wewe si msemaji wa serikali lakini chama chako ndo kinaserikali na kwa kauli zenu chama kinaweza kuiamru serikali. Unahitaji mjadala wa kitaifa. Ila ni vema tukiangalia historia maana ndo inaweza kutudirect wapi twende. viwanda vyote alivyoacha Nyerere ccm imeua, aliacha shirika la ndege na ndege 11 leo hakuna hata moja, reli is no longer productive, unadhani kama vyote vingefanya kazi leo hii watanzania wangapi wangepewa ajira? Umeme hakuna, ni watu wangapi wanakosa ajira hapo? Nafikiri history inatuhukumu. Sera mbovu za ajira, angalia wageni wangapi wanafanya kazi nchini na wanasifa sawa na za watanzania?

 

msemaji ndan ya bunge na mwaharakati,sijawahi hata siku moja kukusikia bungeni ukiwasilisha hoja imara kama hii pamoja na kua ulikua na mawazo kwa miaka minne iliyopita..
DR unajua lowassa ndo muuaji wa viwanda tanzania?
Alitengeneza bomu je ninyi hamkuona?
Acheni siasa ktk mambo ya msingi..tena waambie ccm wenzio kifo ndo dawa yenu
 
Kwenye upande wa uzalishaji na viwanda bila umeme ni sawa na kujaribu kupaka upepo rangi.

Tutainvest vipi kwenye biashara ya viwanda kwenye mazingira haya ya umeme?

Ghorofa haijengwi bila msingi.
 
Mh.hk nakupongeza kwa mawazo mazuri na kama changamoto kwa serikali,chama chako na wananchi,napenda nikukumbushe kuwa jambo lolote zuri lilianza ktk kufikiri yaani wazo,na baadae aidha mtu mmoja akaweka ktk utendaji na wengne wataendeleza,binafsi nathamini mawazo yako na nashawishika kusema ni mbunge mwenye muono wa mbali,unaonaje kama utatumia mawazo hayo mazuri kuanzisha mchakato kama huo ktk eneo lako kwakuwa ardhi ipo ya kutosha,vijana wapo wenye taaluma mbalimbali,tengeneza mazingira ili sote tujadili kilichowezekana kupitia wewe mwenzetu,tusizungumze kwny jukwaa ulichoona india,bangladesh n.k maana ili wazo lipate mashiko liwe na mfano wa mazingira yetu na si china maana si kila mtu anakufaham china.onesha njia kwa wazo hili zuri tuondoke kuwa wazungumza kuliko utendaji.
 
Wote vijana, na wote mnavaa kijani.
Ila mkuu wewe ni mheshimiwa mbunge na mwenzako wala si diwani.
Unavyochambua hoja zako... dah!! yaani very shallow.
Mwangalie au msaome Mchambuzi humu jamvini, halafu jifasnanishe na ukarudie kuandika upya!

Mfuko huo ningeomba uchanganue source ya fedha, aina za kaZI ZITAKZOPEWA KIPAUMBELE, preferential group ya vijana, eg. wanawake, cooperatives za vijana, vijana wasio na ardhi, hands on au vocational training, huo mfuko utakuwa chini ya nani? etc...

Kama upo serious chambua zaidi, otherwise inaonyesha kama unatuhadithia ndoto uliyoota jana .
 
Reactions: Nzi
Kingwala naomba Nikuulize swali dogo tu ?

  • Samani yaani furniture za Ofisi yako ya jimbo zimetoka wapi zimetengenezwa nchi gani na nani
  • Katika pair zako za viatu ni ngapi umechongessha mechongwa na fundi gani wa tanzania au Dizaina gani wa Italy
  • Katika suti zako za Suti unazovaa mjengoni umeshoneshwa kwa nani au umenunua duka gani la Tanzania au tabora...?
Mimi nitapenda kusikia Suti za Mheshimwa "XYZ" zinatenegnezw na K mwanamboka au fundi fulani wa tabora. Nimetaja ni vitu vidogo vidgo sana lakini kwa kuwa nyie ni vingozi onyesheni mfano kupenda bidhaa za Nyumbani msisingizie Quality. With market availabilty quality itaogezeka.

Wekeni sera ya Upendeeao kiasi fulani. Kiti cha CEO ofisini kiwe cha china o tukubali lakini hata viti vywa wageni na meza tena kwenye halmashauri.......
 
Mawazo mazuri mh mbunge.
Ugumu unakuja kuwaunganisha watu waweke kando mahaba yao ya kisiasa na kutafakari nje ya boksi.
Naamini Tanzania yenye neema kwa kila mtu inawezekana kama kila mmoja wetu akitambua wajibu wake.
OTIS
 
Usilete siasa za itikadi tofauti tunapoongelea mambo serious ya kitaifa, hautakula siasa za chama chako bali mikakati inayotekelezeka italeta mabadiliko kwenye maisha yako na wajukuu zako!


call a spade spade

usipotaka kukubali ukweli wazo lako litabakia kuwahadaa wananchi kisiasa kwa kutumia nadharia shawishi

je wewe binafsi umeshatoa ajira ngapi kwa vijana wa kitanzani (direct employment)?
 

Mkuu, kumlinganisha Mchambuzi na HK (katika uchambuzi wa siasa za TZ na CCM) ni sawa na kumlinganisha Cristiano Ronaldo na Mrisho Ngasa.
 
Wazo zuri Mh. Ila naona kwa hali ilivyo sasa jinsi serikali ilivyoacha soko la ndani la Tanzania kumilikiwa na bidhaa za nje, kwa mfano, Viwanda vya mafuta ya kula vinatoa mafuta ghafi Malasia n.k huku, kilimo cha michikichi kwa mikoa kama Kigoma kimekufa, Viwanda vya bia, asilimia kubwa ya ngano yao wanatoa Afrika Kusini na Canada, Juice tunakunywa toka urabuni na Kenya. Kasoro viwanda kiwanda cha Sigara na sukari tu, ndivyo vinatoa material yao hapa nchini. Kwa hali iliyopo sasa hata ukiwa na proposal nzuri kama yako inakuwa ni utopian tu. Kafanyeni mabadiliko bungeni ili kumuokoa mzalishaji hasa mkulima wa Tanzania hata muweke quarter basi sio watu wanaingiza holela mafuta ghafi namna hiyo tena wengine wenye viwanda ni wabunge wenzako. Tena na huko EAC mnakotupeleka ndio tunaenda kucomit suicide kabisaa.
 


Swala la ajira kwa vijana ni time-bomb kwa Tanzania; ni muhimu sana kulipatia majibu sahihi mapema kabla haijawa too late.

(1) Sera za kiholea za uwekezaji zilizoletwa na serikali ya CCM zirekebishwe ili kuwa na kipengele kinachouzia mwekezaji kuleta wafanyakazi kutoka nje kufanya kazi ambazo kuna watanzania wanaoweza kuzifanya. Haina mantiki kwa mwekezaji kujenga hoteli Tanzania, halafu watumishi wote hata wafua mashuka watoke nchi za nje, halafu eti serikali yetu bado inawapa vibali vya kazi.

(2) Tenda za ujenzi wa miradi mbali mbali ya serikali ya CCM ziweke wazi kuwa mshindi atatakiwa kuajiri vijana wa kitanzania kwa kazi zote wanazoweza; mkandarasi awe analeta wataalamu tu. Zamani sana wakati viwanda mbalimbali vinajengwa chini ya utawala wa Nyerere, wakandarasi walikuwa wanakuja na wataalamu na wasimamizi tu, huku wafanyakazi zote wakiwa ni watanzania. leo hii eti wachina wanaleta wabeba kokoto kutoka kwao na serikali hii inawapa vibali vya kazi.

(3) Sera ya serikali ya CCM kuhusu elimu kwa watoto wetu ifutwe na kurudisha elimu ya Kujitegemea iliyoasisiwa na Nyerere ikiwatayarisha vijana kufanya kazi. Kwa kufanya hivyo, shule zote za Kata ziangaliwe upya na zile ambazo hazitoshelezi kutoa elimu ya sekondari zifungwe. Elimu yetu itoe mkazo mkubwa wa kufundisha vijana stadi mbalimbali zinazowawezesha kujiajiri pamoja na kuwaandaa kujiendeleza kwa elimu ya juu zaidi. Kile kitu kilichokuwa kinaitwa mchepuo kirudi tena. Chni ya elimu ya kujitegemea, michepua mbalimbali ilikuwa inawapa vijana stadi ambazo ziliweza kuwafanya baadhi wajiajiri.

(4) Serikali yetu ya CCM ipange vipaumbele vya nchi kwa makini sana kwa kuondoa matumizi yasiyokuwa na tija kwa taifa kama vile posho kubwa kwa wabunge, marupurupu makubwa kwa viongozi wa serikali, matumizi ya magari ya bei kubwa, na kutumia pesa hizo katika miradi ya maendeleo ambayo itatoa elimu nzuri na ajira kwa vijana wetu.
 
Mh. Kigwangalla,
Wazo lako ni zuri sana lakini hayo ni maneno na sio vitendo, kama ulivyodai mwanzo wa maelezo yako, "Vijana wa zama hizi hawataki maneno, wanataka vitendo. Maneno na mipango mizuri iliyoandikwa haitowasaidia sana, wanahitaji fursa za ajira, za kujiajiri, za kuendesha maisha yao. Tena vijana wa siku hizi hawako tayari kutumiwa na wanasiasa kwa faida za kisiasa", mwisho wa kukunukuu.

Tatizo jengine ni kuwa wazo lako ni zuri na umelielekeza kitaifa wakati taifa hili ni kama ulivyosema wewe mwenyewe kuwa "TZ ni tabu kuja na wazo jipya likakubalika".

Bahati mbaya TZ imekuwa nchi ya wanasiasa kusema na wananchi kulalamika na kama wanavyosema Waswahili, Mkono mtupu haulambwi, mimi nabadilisha kidogo huo msemo kwa kusema "maneno matupu haya hayaleti tija." Kiini cha tatizo la kuangukia katika maneno mengi ni kuwa Watanzania kila mtu ni mwanasiasa, siasa imekuwa dini, siasa imekuwa mtaji, siasa imekuwa ngao ya kujikinga na kushambulia...SIASA KWANZA NCHI BAADAYE. Angalia mfano mdogo tu, wasomi wengi walivyojikita kwenye siasa, kuna Ph.Ds zaidi ndani ya siasa kuliko katika jamii (ninaweza kuwa nime "exaggerate" kidogo kuhusu hili lakini ukweli ni kuwa wataalamu ama wanakimbilia siasa au wanakimbia nchi kwa sababu kwengineko elimu yao hailipi).

Ushauri wangu kwako kama mleta mada na mwengine aliye na mawazo na uwezo kama wako, ni kuwa safari ndefu huanza hatua ya moja ya mwanzo. Wewe kama mmoja wa viongozi wakuu wa jimbo lako, fanya yafuatayo:
- Andaa mradi, kama huna utaalmu tafuta wataalamu wakuandalie.
- Mradi wenyewe uwe mdogo tu kama wa majaribio, ambao utawashirikisha vijana 10, unaweza hata kuanza na hao vijana 6 waliokuja kukumba kazi. Usiwape samaki, wape mshipi. Watu husema "hata chembe ya mchanga kwa muhitaji ni sawa na mlima"Ukifanikiwa wengi watataka kujiunga. Hapa jiepushe kutumia siasa na chama. Utafanya kosa kusema ni mradi wa wanachama gani, wa maskani gani, kijiwe gani n.k., uwe ni mradi wa vijana. Ukiwafanya waamini kuwa ni wao wataulinda, ukifanya kwa lengo la kisiasa, utahujumiwa.
- Mradi wenyewe uwe wa kutumia "assets" zilizopo katika jimbo lako - ardhi, misitu (bila ya kupelekea uharibifu wa mazingira).
- Wananchi wakielekezwa wanakuwa rahisi kutoa ushirikiano, washirikishe wanananchi, pale wanapoweza kutumia nguvu zao wazitumie, wasisubiri serikali ije kuwafanyia kila kitu.
- Bila ya shaka utahitaji fedha, andaa shughuli za kukusanya fedha kwa njia za harambee, matamasha ya mziki/sanaa, kuwaomba wafanyabiashara, makampuni ya ndani na ya kigeni, wafadhili wa ndani na wa nje, mashirika ya maendeleo ya ndani na ya nje ya nchi. Zungumza na Mama Ananilea Nkya wa TAMWA, uzoefu wake utakusaidia sana. Kama itabidi, omba mkopo benki wewe mwenyewe binafsi.
- Anzisha mradi na uusimamie mwenyewe binafsi na kama unamwamini mtu,mkabidhi.
- Ukifanikiwa mradi huo na kuleta tija, unaweza kuusogeza katika vijiji na sehemu nyengine. Bila ya shaka kwa kutumia mafanikio yako, wa mikoa jirani watafuata nyayo.

Kila la heri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…