Majibu ya Kigwangalla: Utatuzi wa Ajira kwa Vijana wa Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majibu ya Kigwangalla: Utatuzi wa Ajira kwa Vijana wa Tanzania?

Discussion in 'Great Thinkers' started by HKigwangalla, Feb 19, 2012.

 1. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #1
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Leo nimeamka nikimfikiria kijana wa kitanzania. Haswa baada ya kupokea maombi ya vijana 6 kwa sms wakitaka niwasaidie kupata mahala pa kujishikiza, kwa 'marafiki zangu'. Mtihani huu mgumu sana. Nitautatuaje? Marafiki zangu kila siku wanatoa nafasi za ajira kwenye mashirika yao? Nikasema, labda tuanzishe mjadala mahsusi wa kitaifa, utakaolitazama suala la ajira kwa vijana wa kitanzania kwa mapana na marefu, na kulifanyia utekelezaji. Vijana wa zama hizi hawataki maneno, wanataka vitendo. Maneno na mipango mizuri iliyoandikwa haitowasaidia sana, wanahitaji fursa za ajira, za kujiajiri, za kuendesha maisha yao. Tena vijana wa siku hizi hawako tayari kutumiwa na wanasiasa kwa faida za kisiasa.

  Hii ni Tafakuri Tunduizi yangu juu ya ufumbuzi wa tatizo la ajira kwa vijana na pia kukuza uchumi wa nchi yetu. haimaanishi hii ndiyo kila kitu na kwamba lazima vijana wote watataka kuwekeza kwenye industry nilizozitaja hapa, hii ni dira tu;

  Tuanzishe mfuko maalum wa kutoa mikopo ya uwekezaji kwa vijana wa kitanzania. Mfuko huu utawalenga vijana watakaowekeza kwenye sekta ambazo tutazichagua, sana sana tutoe kipaumbele kwenye sekta za kilimo na viwanda vyenye backward au forward linkage na kilimo, moja kwa moja. Vijana hawa waingizwe kwenye challenge ya kupata mikopo, ambayo itatakiwa iwe na masharti nafuu, iwe na riba ndogo (asimilia 8 kushuka chini), iwe na payback period ndefu, ya miaka 15-20, isiwe na masharti ya dhamana/security za mali (maana vijana hawana assets zozote!) bali iwe na dhamana nafuu kama cheti cha elimu ama ardhi (shamba lililorasimishwa). Mpango huu uendane na kutengeneza utaratibu mzuri na rahisi wa kusajili mashamba. Yatengwe maeneo maalum ya kuwekeza. Vijana wawe guided kuwekeza kwenye sekta zilizochaguliwa na wawezeshwe kupata mitaji hiyo. Kama tutakuwa na vijana wataowezeshwa kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda kama vya kuchambua pamba, kukoboa na kusaga unga/chakula cha mifugo, kukamua na kusafisha mafuta ya kula, pia kutengeneza sabuni, kusindika juice, viwanda vya nyuzi (spinning mills), tutaweza kuwataka wawekezaji hawa vijana kuhamasisha kilimo cha kisasa na kusupport wakulima kwenye maeneo yao (linaweza kuwa sharti mojawapo la kupata mikopo hii maalum kwa ajili ya vijana) kwa kuwa-supply farm inputs, farm machinery, improved seed varieties etc - hii itasaidia kuongeza tija na ufanisi kwa wakulima.

  Pamoja na kuongeza tija na ufanisi (productivity and efficiency), tutakuwa tumeongeza volume of farm and industrial produces (uzalishaji), uhakika wa soko utakuwepo (market stability and sustainability) na hatutouza mazao fresh kutoka shambani bali tutauza finished goods au semi-processed goods ambazo zimefanyiwa value addition kwenye viwanda vyetu; finally tutakuwa tumetatua tatizo si tu la ajira bali hata la kiuchumi kwa kuongeza uzalishaji, kuongeza thamani ya mazao yetu, kuhakikisha masoko ya uhakika kwa wakulima wetu na mwishowe kupunguza inflation ya vitu na zaidi zaidi kuongeza exports na kupunguza imports kitu ambacho kitasaidia ku-stabilise our BOP (balance of payments) account. Hapa pia tutakuwa tumetatua tatizo la kuanguka thamani kwa shilingi yetu. Ukiongelea kuimarisha uchumi wa nchi basi ni lazima uongelee kuongeza tija na ufanisi ambao utaongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa zenu, na wala siyo austerity measures za muda mfupi zinazopelekea kuimarisha fedha na viwango vyetu vya exchange rate against other foreign currencies. Ukiuangalia mpango huu utagundua kwamba kutakuwa na vijana wasomi (watakaoandaliwa kuwekeza kwenye viwanda) na wale ambao hawajasoma (watakaowekeza kwenye kilimo), haya makundi yatabebana - kwenye model hii, na hivyo kila kundi litatoa ajira kwa watu wengi zaidi.

  Kwa nini basi mimi hapa napendekeza mikakati hii iwalenge vijana? Vijana, tukiondoa factors nyingine, kibaiolojia tunawategemea bado watakuwepo kuwepo hapa duniani kwa muda mrefu kidogo kuliko makundi mengine, na hivyo kama tutaendelea kuwa na uchumi unaokuwa kwa kasi hii ndogo na usiwaowashirikisha vijana kwa maksudi, maana yake wataishi maisha yao yote ya ujana, ujuzi, nguvu na ndoto kwa shida sana bila kutumika ipasavyo. Pia, ili kuwa na uchumi imara, ni lazima tujipange kwa kuangalia mbali kidogo, siyo kwamba tunafanya nini leo ili tufanikiwe leo! Tukiwatumia vijana kwa kuona mbele, wakiwekeza leo na wafanikiwa kuendesha biashara zao kwa faida maana yake ni kwamba baada ya miaka 20, Tanzania itakuwa na matajiri wengi zaidi, na itatoka kwenye kundi la nchi za daraja la tatu! Pia, ni rahisi sana kwa kijana kuchukua risk na kufanya kazi kwa bidii kufikia ndoto zake bila wasiwasi, na zaidi kundi hili likopewa kipaumbele linaweza kuibadili kabisa culture ya watanzania kutoka kwenye 'business as usual' na 'laissez-faire' na kuwa nchi ya watu wenye kufanya kazi kwa ubunifu wa hali ya juu na passion ya ukweli. Mimi naliona hili ndiyo kundi pekee litakaloweza kuijenga Tanzania mpya, Tanzania ya miaka 20 ijayo... haimaanishi wazee 'wa busara' wasiwepo kabisa, hapana lakini kwenye mpango huu wa kujenga upya viwanda vyetu na kutoa ajira kwa vijana, wasihusike.

  Ni lazima tuwe na ndoto. Ni pia ni lazima tujipange kuzifikia ndoto zetu. Hakuna ujanja mwingine. Hatuwezi kufanikiwa kwa kutumia mikakati ile ile iliyotufikisha hapa. Huwezi kupanda mchicha ukajiandaa kuvuna bangi! Tunahitaji kubadilika, tunahitaji new approaches, new ideas... tukiwa na new approaches sasa hapo tunaweza kuona new results!

  Wakatabahu,
  HK.
   
 2. m

  mchambakwao Member

  #2
  Feb 19, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh. kwa mtazamo wangu bado naona umejikita kwenye maandishi kama ulivyoanza kusema awali.

  Nchi yetu ilikuwa na viwanda lukuki mfano General Tyre-Arusha,ni kutokana na sera zenu (CCm) mmekibinafsisha kiwanda na hadi wataalamu wote wamekimbilia kiwanda cha matairi cha kenya ingawa bado pale General Tyre mitambo yake bado ni mipya asikwambie mtu,vijana wameachishwa kazi,hali kadhalika UFI-Ubungo,ZZK-Mbeya.nakadhalika,nakadhalika.

  Mh.nadhani ni bora mngeweka au kutenga fedha kwa ajili ya kufufua viwanda kwanza kuliko kupiga bla bla!

  Watu wameua viwanda ili kukumbatia wafanyabiashara wa nje waingize bidhaa ndani, ni uamuzi ambao inabidi uangaliwe upya.
   
 3. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,636
  Likes Received: 906
  Trophy Points: 280
  Ndio Mh Kigwangala, Hongera sana kwa constructive ideas. Nimekusoma mara nyingi, una mawazo mazuri, creative. tatizo ni nyumba uliyopo, nyumba uliyopanga. Wenye nyumba hawasikiii, hawataki changes.

  Hapa ninakupongeza na kukupa maoni.

  Kwanza Taifa linapata hasara sana kwa kuachia nguvu kazi ya nchi (vijana) kukaa bila kazi.

  taifa linatakiwa kuzalisha na kuuza nje.

  Kuzalisha na kuuza nje kunainua uchumi wa mtu mmoja mmoja, pia serikali itapata kodi na forex.

  Sekta ambayo imedorora ni pamoja na kilimo, pamoja na kauli za kisiasa bila mikakati vitendo za kilimo kwanza.

  kilimo kwanza ni wawekezaji kwanza.....

  Kwani hiyo ardhi nzuri wanayopewa wawekezaji kwa ahadi ya 10%, wangepewa watanzania ingekuwaje????

  Unakuta viongozi wanahodhi ardhi kubwa halafu vijana wanazurura.

  unakuta manispaa wanapima ardhi halafu wanauza ki ujanja ujanja (million 5 hadi 50). Ardhi ya manispaa walinunua au ardhi ipo tu bure kwa ajili ya wananchi? Gharama ya kupima ni laki au million 5?

  Je kwa nini mwekezaji aje mikono mitupu halafu aondoke akiwa tajiri?? Mfano mwekezaji anakuja, anapewa ardhi pamoja na deed ya 99 years, anapata mikopo benki. Halafu wazawa ndo wanakuwa watumwa wa kulima kwa ujira mdogo na unyanyasaji.

  Mheshimiwa Mbunge, unasoma hizo point? ishauri serikali ya chama chako tawala mzee.

  Je Kilimo kwanza ni kwa ajili ya wawekezaji wa nje?

  je kilimo kwanza ni kwa ajili ya wafanyabiashara wakubwa??

  Kugawa mbolea ya ruzuku ndo kilimo kwanza??

  Serikali yetu ina bureau crazy sana kwa watanzania wanaotaka ardhi walime.... Hakuna channel moja ya kueleweka ya kufuata ili kupata ardhi. Sijui TIC, sijui CHC, sijui wizara ya ardhi, sijui wapi.

  What is the clear channel for tanzanians to apply for agricultural land??

  Je wafanyakazi serikalini wataacha longo longo au wanataka 10% - waongezewe mshahara ili wasiombe rushwa.

  Sina la zaidi, may be wengine watachangia. Asante.

  Natumaini utafuatilia ujibu hoja hapa. Pambana Mheshimiwa, aluta continue
   
 4. TASLIMU

  TASLIMU Senior Member

  #4
  Feb 19, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hamisi vp ile AHADI yako katika ukurasa wa Facebook,kipindi kile cha mgomo,ulisema kuna maamuzi utafanya mbona kimya,au Hoja ile umeshaitoa mezan,tuambie basi,uliniambia niendelee kusubili,au nieendelee kusubili
  Iwa mwema
  Wakatabahu
  TASLIMU
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Sekta nyingi nchini hazina tija, zinafanyika kwa mazoea! we need to change everything!! Miradi ( mega-millions projects haifanyiki inavyotakiwa) ikianzishwa inaishia kuwanufaisha walio tayari kupaa badala ya kuwainua walio chini kabisa. Wenye nazo wanashindwa kuizungusha fedha yao hadi kwa mlala hoi kutokana na sera mbovu! kwa hiyo sera zetu bado nii zile za kulindana siyo za kunufaishana wananchi wote, ndiyo maana unaona bado kuna kundi moja linaloamini lenyewe ndo linamiliki nchi, na lina haki ya kufanya hivyo.
  Sekta ya viwanda inahitaji mapinduzi ya hali ya juu, kuanzia kwenye processing raw materials hadi kwenye parkadging tayari kwa kuuza ndani na nje. watu wa uchumi watusaidie namna ya kukuza soko la ndani ili watu waache kukimbilia bidhaa za nje badala yake wapende za ndani, siyo kama ilivyo sasa utakuta viongozi wanapiga kelele tu "tupende kununua bidhaa za ndani, huku wanasahau kutengeneza mazingira ya kufanya hivyo".
   
 6. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #6
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  nakushukuru mkuu kwa mawazo yako, japokuwa umenipiga maswali, mimi nadhani sistahili maswali kwa kuwa si msemaji wa serikali na wala mimi siko huko. Mimi ni msemaji wako ndani ya Bunge na mwanaharakati wa kutaka kuleta ustawi wa kiuchumi na kijamii katika nchi yetu, sipendi utoa majibu.

  Kama utakuwa umeona vizuri utagundua kuwa mimi nayajua mengi ya matatizo uliyoyaweka na majibu ya maswali uliyoyaweka, na ndiyo maana nikaja moja kwa moja nikipendekeza 'Majawabu ya Kigwangalla'. Hii inatakiwa ikuoneshe tu kwamba ninajua tuna tatizo wapi na wapi na ndiyo maana sasa mimi napendekeza solutions.
   
 7. m

  mubi JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Ni vizuri , natoa ushauri wa bure kabisa, nenda ubalozi wa Marekani uulize ni vitu gani ambavyo viko kwenye AGOA, ufuatilie kisha uwatengenezee Ajira vijana hao kwa kupata market ya vitu vinavyopatikana Tanzania na kuuzwa USA duty free. Kwa njia hiyo utaweza kutengeneza hata viwanda vidogo vidogo kadhaa. sasa ngoma kwenye umeme hasa huko kwako Nzega. Lakini unaweza ukatengeneza viwanda vinavyotumia Handloom kwa upande wa texttlie, hivyo havihitaji umeme na pamba iko hapo Nzega, Shimyanga na Mwanza. Jaribu hiyo utakuwa na viwaanda vya kutengeneza sox, gause za mahospitalini, sweater, towel , jaribu hiyo ni nzuri na kama ukitaka standard wanayotaka wamarekani watakupa vifaa vyao utalipa baada ya mauzo yako, au mikopo hiyo ya benki zetu.
  Best of luck your excellence.
   
 8. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #8
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa nyumba uliyopo ndio chanzo cha yote hayo na sijui kama ukianzisha hili watakuelewa kama lile la Madr nasikia ulibanwa Dom,
  Sasa tuunganishe vijana tufikishe swala hili serikalini kwani umesema wewe si serikali na serikali yenyewe ni nyang'au unaweza usieleweke andaa vijana tupe njia kupeleka swala hili mbele ajira ni ngumu sana hapa natamani hata mimi nikupm unisaidie kupata kazi nipo na kadegree kangu nasota tu mtaani
   
 9. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #9
  Feb 19, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Si rahisi kutekeleza hayo unayosema chini ya serikali dhaifu ya ccm. Kwa miaka 50 walichofanikiwa ni kuigeuza nchi yetu dampo la bidhaa za nje na kuua kabisa viwanda vichache vilivyokuwepo. Kibaya zaidi mmeendelea kuuza rasilimali za nchi kwa manufaa yenu 'vigogo' na familia zenu na kuendelea kuwalinda waporaji wa rasilimali zetu kwa mgongo wa 'uwekezaji'. Suala la ajira kwa vijana, kana kwamba wasio vijana wana ajira, mnalitumia kwa malengo ya kifisadi. JK na maharamia wenzake (wanamtandao) walikuja na mbwembwe nyingi zenye ahadi lukuki, tena wakatenga mabilioni ya walipa kodi yakaliwa na matajiri kwa jina la 'mabilioni ya JK' kana kwamba JK anakiwanda cha kuzalisha fedha kule bagamoyo. Nchi inaliwa, ccm wanachekelea.

  Tunachopaswa kufanya sasa ni kuiondoa serikali hii dhaifu madarakani hapo 2015, japo inaniuma kuona tunaongozwa kwa namna hii mbovu hadi wakati huo lakini tuheshimu demokrasia. Serikali ijayo ishirikiane na wananchi kutekeleza sera mpya za kuwakwamua kiuchumi. Haiwezekani mkulima alime kwa taabu halafu azuiwe kuuza bidhaa zake kwa soko linalompa faida.

  Suluhu ya kwanza ni kuiondoa ccm madarakani. HK huko uliko hakuna jipya litakalopatikana katika kutatua matatizo yetu. Uko kwenye genge la wanyang'anyi na majambazi wa rasilimali za nchi.
   
 10. m

  mubi JF-Expert Member

  #10
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  tatizo kubwa watanzania hawataki kufanya kazi. Na hatuna techniciens wa kutosha....tunahitaji kutoa elimu kwa wananchi wetu
   
 11. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #11
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mhe. Kingwangala
  Mawazo yako ni mazuri hasa kwenye suala la kuwekeza kwenye Kilimo, Mimi Naamini Vijana wengi wasomi na wasiowasomi wako tayari kuwekeza kwenye kilimo, lakini wanawekeza vipi ilihali resources zote za uwekezaji wanapewa wageni?

  Tatizo kubwa la nchi yetu ni kufanya mipango ya zima moto, hatuna mipango ya muda mrefu. tunataka kupanda mpera ili tule sisi na si watoto au wajukuu zetu. Mwl. alipofungua viwanda vingi ilikuwa ni kwa ajili ya kizazi hiki, lakini walewale wa kizazi chake waliviua na vingine wameviuza kwa bei poa kwa kisingizio cha uwekezaji.

  Juzi hapa Zitto kapeleka muswada Bungeni kuhusu Mkonge, wewe ni shahidi wa kilichotokea, kizazi kile kile kimepinga kwa sababu wao wanataka mipango ya kula leo, siyo kesho. Nani asiyejua Mkonge ni zao linaloweza kupunguza tatizo la ajira kwa kiwango kikubwa?

  Viongozi wetu kama kweli wanasutwa na tatizo la ajira hawana budi kuandaa mpango wa muda mrefu kwa vitendo. tumechoshwa na misamiati ya mchakato, sijui yakinifu to hell with that. hata hizo pesa za EPA na Rada zingefaa sana kuelekezwa kuwakopesha vijana kwa ajili ya kuwekeza kwenye kilimo.
  Ardhi tunayo, Lakini uongozi....................!!!!!!!!
   
 12. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #12
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mheshimiwa Hamis (Andrea) Kigwangwala watu waliosababisha vijana wetu wakose ajira ni wakubwa zako makada wakuu wa chama walipokuja na sera za kubinafisha viwanda bila kuweka sheria na kanuni makini!!! Walitakiwa waweke sheria kwa yeyote anayenunua kiwanda ahakikishe kinaendelea kufanya kazi tena kwa ufanisi ili Watanzania wapate ajira, kama mtu hawezi basi atuachie kiwanda chetu!!! Sasa ndugu kwa tamaa za wakubwa wakauza kwa mgao viwanda vyetu mradi wanapewa mshiko!!! Kwa vile hawa watu bado wapo kwenye mamlaka basi waambie kuwa tunahitaji viwanda vyetu vifanye kazi vijana wapate ajira!

  Kama hawawezi basi wakimbie mapema maana tutawaambia vijana adui wao mkuu ni aliyeuza viwanda, mashamba, mighodi na rasilimali zetu ili tuwatimue turudishe mali zetu tuweze kuleta ajira kwa vijana wetu!
   
 13. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #13
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mubi, ahsante kwa ushauri wako. Hili wazo ninalo kwa miaka karibu minne sasaa, baada ya kutembelea textile/garment manufacturing industries kule India, Bangladesh na Thailand, lakini hapa Tanzania ni kazi sana kuja na wazo jipya na likakubalika kirahisi kwa kuwa watu wengi, kuanzia wale walioko serikalini na hata wale wa mtaani, wana mawazo hasi sana na hawako ayari kupokea mawazo mapya kirahisi
   
 14. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #14
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  I couldn't agree more
   
 15. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #15
  Feb 19, 2012
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mh Kigwangala,
  Hongera kwa kufikiria nje ya box. Tanzania ya leo tunahitaji growth ya maana kwenye uchumi wetu ili vijana wetu wengi wapate kazi za kuajiriwa pamoja na zile za kujiajiri. Growth ya sasa ya around 7% ni ndogo sana ukilinganisha na ongezeko la watu lakini pia na opportunities mbalimbali zilizopo.

  Kwa uzoefu wangu kule wilayani kwetu, naona mikopo pekee sio solution. Level ya ujinga na kukosa creativity ni kubwa mno kiasi kwamba kwa walio wengi hata wakipewa pesa bure bado wanaweza wasifanikiwe kwenye biashara au kilimo. Vijana wengi hawazioni hata opportunities ambazo zimewazunguka. Aliyesema opportunities follow prepared minds hakukosea. Ni muhimu minds zibadilishwe kwanza kabla ya vijana kuwa na uwezo wa kweli wa kufaidika na opportunities zilizopo.

  Mimi nafikiri hatua ya kwanza lazima iwe kurudi kwenye VETA za maana kwenye kila wilaya. Badala ya kujenga shule nyingi za sekondari, halmashauri wajenge pia shule za VETA chache ambazo zitakuwa na vifaa pamoja na walimu na hizo shule ndio ziwe chanzo cha ujasiliamali na ubunifu mwingine mbalimbali. Baadhi ya wanafunzi katika hizo shule ambao wanaonyesha uwezo wa kuweza kujisaidia basi wasaidiwe kwa mikopo mbalimbali ambayo inaweza kuanzishwa kwenye level ya halmashauri pamoja na ile ya kitaifa.

  Wilaya inaweza kuwatumia vijana katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa miradi ya maendeleo, kilimo, ufugaji na biashara nyingine kama sehemu ya apprenticeship na kisha kuwaachia wakiwa wamepikwa tayari kwa kujiajiri au kuajiriwa sehemu zingine.

  Hizi programs zinaweza kufanywa kwenye level ya jimbo na bila hata kuhusisha pesa za ziada kutoka ngazi ya taifa. Resources za kutosha tayari zipo, kinachokosekana labda na will ya wahusika katika ngazi ya wilaya.

  Nakubaliana na wewe, we need to think big, be creative and face the reality that status quo is no longer sustainable and not working too. Inabidi kujaribu njia zingine kuanzia level ya familia, wilaya mpaka taifa.

  Hili si suala tu la serikali iliyoko madarakani tu, ni suala ambalo sisi kama wananchi pia tunaweza kuamua na kuchukua maamuzi. Serikali kuu ikiunga mkono itakuwa nzuri sana, lakini itakuwa makosa makubwa kukaa kimya tukisubiri mpaka serikali kuu iamke.

  Mkuu Mh Kigwangala kama mbunge, haya mengine yako chini ya uwezo wako kabisa na halmashauri yako. Tuonyeshe mfano kwa matendo na wananchi wengi au wilaya zingine zitaiga na kufuata.
   
 16. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #16
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Usilete siasa za itikadi tofauti tunapoongelea mambo serious ya kitaifa, hautakula siasa za chama chako bali mikakati inayotekelezeka italeta mabadiliko kwenye maisha yako na wajukuu zako!
   
 17. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #17
  Feb 19, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Umesahau Mara hii? Si wewe uliyesema kuwa serikalini watu hawataki mawazo mbadala? Serikali hii ya ccm ndo tatizo la kwanza. Kama kweli una dhamira ya dhati ya kufikia malengo ya kumsaidia mtanzania lazima uondoke katika kundi la watu wanaokwamisha mawazo mbadala. Nchi hii ni tajiri lakini ina kundi la wezi na majangili wa rasilimali. Kwa bahati mbaya sana, wamejificha kwenye kichaka cha serikali ya ccm na ndani ya ccm. Hatuwezi kuendelea bila kuvunja 'circle of poverty' iliyosababishwa na majambazi wa ccm.

  Hata kama hutaki kukubali, lakini unajua kuwa huu ndio ukweli. Nchi yetu chini ya serikali ya ccm haiheshimu taaluma za watu. Siasa zimeshika hatamu, matokeo yake wataalamu wako frustrated na hawana motisha wa kufanya maendeleo. Vipaumbele vya serikali ni wizi, rushwa, ufisadi na kumilikisha rasilimali za nchi kwa wageni. Bila kuondoa hawa wezi (ccm) hatutaweza kuanza upya kuijenga nchi yetu.

  Endelea kuchumia tumbo lako ndani ya ccm, utadumaa kwa kukosa fikra mbadala.
   
 18. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #18
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 4,544
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona na wewe unakua na mawazo hasi tu?! Umekuja na wazo zuri, halafu wakati huo huo unasema wazo kama lako ni vigumu sana kukubalika serikalini na mtaani!!
  Sasa dhumuni la wewe kuandika humu ni nini kama huamini katika utekelezaji wa kile ulichokiandika?!?!
   
 19. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #19
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Nimesema 'ni kazi sana kuja na wazo jipya na likakubalika kirahisi' ...underline the word 'kirahisi' utaona namaanisha kwamba ni kazi ngumu lakini ni lazima ifanyike. Ni hatua muhimu kutambua kuwa kuna watu wenye mawazo hasi kwenye jamii na hata kwenye serikali na hivyo unahitaji kujipanga kuzishinda hizo changamoto zote...
   
 20. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #20
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 4,544
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo juu ni maneno yako mwenyewe. Kwa namna ulivyoyaandika unakua huna tofauti na hao watu walioko serikali na mtaani. Hayajaonyesha ni kwa kiasi gani utaweza kuikabili hiyo hali katika kufanikisha wazo lako!!

  Ebu tuache maneno mengi kama ulivyosema katika post yako ya kwanza.
  Nieleze umejipanga vipi katika kuzishinda hizo changamoto unazozisema kuwa zipo serikalini na mtaani??
   
Loading...