Majibu ya Kigwangalla: Kwa Nini Sikusaini Hoja ya Mhe. Zitto Zuberi Kabwe (MB)!

....Kawadanganye wasiokujua! tunaokufahamu tunajua wewe ni njaa kali!! huwezi kusimama na "wanaume" kutetea hoja bila kufikiria tumbo lako.
 
Huyu Kigwangwallah ni mpumbavu kama walivyo Wapumbavu wengine, huyo anajuwa kwamba ni mbunge wa kamati kuu ya CCM, mwenye jimbo lake mwenyewe ni Hussein Bashe, kwahiyo sishangai kuja hapa na thread za kichangudoa.

Na nina hakika thread amemtag Nape Nnauye, Wilson Mkama pamoja na Mkwerre. kwa msiyomjuwa huyu Fisadi wa elimu, ni kwamba huyu alikuwa kwenye ile taasisi ya kitapeli WAMA.
Hakuna alichonishangaza mimi huyu Kilaza kwa hii thread yake ya kipuuzi.
 
muheshimiwa kigwangala utetezi wako ni sawa na majibu ya wazir wa afya na katibu mkuu wake mama nyoni wakati mko kwenye mgomo wa madactari, majibu yako ni mepec sana na hayana nguvu kabsa,
Najua moyono kiukweli upo ma1 na zito, lakini kwa kuwa unataka kulinda ki2mbua chako kicingie mchanga ndo mana unafanya hivo, nikutoe 2 wacwac kwamba ucogope . kwenye kura za maoni utapita tu km kweli utakuwa una uchungu na rasilimali za taifa hili na nina uhakika kuwa kwa sasa hawatapindua matokeo km mlivyompindua L.Serelii
 
Mtu mzima hovyo!!? kwa hiyo hata kama nchi inatafunwa kiasi hiki, wewe kazi yako ni kuilinda ccm yako?. hufai hata kuwa kiongozi wa familia!
 
Uchangiaji huu "vernomous" hata kama tumechoshwa, hauleti tija kwenye mijadala. Nasikitika na ninachokisoma kwenye hii thread, kinawanyima watu haki ya kutoa hoja ambazo zinaweza kumrekebisha mtu. Matusi, kejeli, n.k. havitamfanya mtu yeyote achukue misimamo tunayotaka aichukue. We must argue and not shout, insult, degrade, look down, etc.

Jamani tujifunze uungwana!
 
Hivi jamaa dokta alishinda au alishindishwa?? Angeandika kwa Kiingereza ngesema msomi lugha inamburuta!

Nataka tu kukukumbusha hata Nyerere (RIP), aliye-engineer hicho chama chako aliishakusaidia kufikiri- kwamba CCM c mama yako. Sasa we unajifanya kuwa na machungu zaidi ya uyu mzee aliyeishi kiitikadi, mkosa unafiki wa kweli, moyoni na kivitendo? Who do u think u r than him? Usijifanye unajua zaidi nin kilianza kati ya yai na kuku daktari (MD, MPH, MBA)! N try to get educated n not education!
 
are you a fool? Hivi kila ambaye kaenda kinyume na huyu bwana ni mwanachadema? Mbona umefilisika? Kwa taarifa yako hata baadhi ya wana ccm hawakubaliani na mawazo kiduchu ya huyu bwana sasa hayo n matusi?.
Unategemea wote watamchekea kama wewe? Wacha wampe za uso bana. Heshima? Heshima gani? Kajivua heshima yeye mwenyewe kwa mchango wake mfu.

Nilivyomuelewa majebere baadhi yetu hatujibu hoja au kuuliza swali kwenye hii thread ya jamaa ila tunaishia kumkashifu..
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu wanabodi,

Nimeamua kuja kujibu kama ambavyo mngependa nifanye. Siyo kwamba nimekimbia JF, la hasha. Siwezi kukimbia na wala sina sababu ya kufanya hivyo. Ni kwamba gadget yangu ninayotumia kwa mawasiliano ilipata mushkeri na nikawa nalazimika kutumia kompyuta na bahati mbaya sana kwa jinsi nilivyokuwa bize na ujenzi wa Taifa nilijikuta nakosa muda wa kukaa kuanza ku-surf. Nisamehewe kwa hilo.

Mimi sijawahi kuwa mnafiki, at least kwa alama tatu za mnafiki kama tunavyofundishwa sisi waislamu. Kwa faida ya mjadala huu, niseme alama zenyewe. Moja ni kuwa akitoa ahadi hatekelezi. Mbili, ni akiaminiwa anahalifu na tatu, akizungumza husema uongo. Namshukuru Mungu sina hata moja ya alama hizi na hivyo kushindwa mtihani wa kuwa 'mnafiki'. Ungeniita mnafiki kama nisingekuwa tayari kutoa maelezo ya maamuzi yangu, ama kama ningewasaliti CCM na kupeleka siri za huku kule, ama kama ningeahidi kuunga mkono hoja hiyo kisha nikakimbia. Leo hii mimi niko chama kimoja tu, CCM, na nitafanya mambo yanayokubalika ndani ya CCM. Siku nikihamia CHADEMA/CUF/NCCR basi nitafanya ya huko bila kusaliti kule na kurudisha CCM ama kupeleka kokote kule kinyume na utaratibu. Huo ndiyo msimamo wa ukweli na siyo unafiki.

Kuna uwezekano wa kuwa na tafsiri tofauti kutokana na pre-conceptions zetu vichwani, siwezi kulizuia hilo hata kidogo. Kwa kuwa ninakalia kiti cha uwakilishi, nina-feel ninawajibika kwenu kutoa maelezo ya msimamo wangu kwenye hili, na wala sintomumunya maneno.

Kwanza, hoja yenyewe siikubali. Kwa sababu ninaamini serikali ya Chama Changu (CCM) haijashindwa kufanya kazi ya watanzania kiasi cha kung'olewa madarakani kwa namna hiyo. Pili, naamini na ninakubali, na kwa hakika ninakerwa na baadhi ya watu waliopewa dhamana za kuongoza baadhi ya ofisi nyeti za umma wametuangusha watanzania, na hivyo naunga mkono hoja ya kutaka kuwatoa hawa. Mhe. Zitto Kabwe (MB) alipokuwa akijumuisha hoja yake, alitaka serikali iwawajibishe baadhi ya mawaziri na watendaji wakuu wa Wizara na Mashirika ya umma, na akasema kama serikali haikufanya hivyo kufikia J3 iliyofuata basi sisi (Bunge) tuna uwezo na WM na kwamba atapitisha karatasi ya kukusanyia saini 70 ili kukidhi matakwa ya kikanuni ya kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na WM; kwa tafsiri yangu ni kwamba Mhe. Mbunge alilenga kuweka presha kwa serikali, kuitaka iwajibike kwa kuwawajibisha mawaziri hao (watano) kama alivyowataja yeye. Kwanza mwanzoni nilielewa hivyo. Baadaye jinsi ilivyopokelewa na wadau mbalimbali nikaona kama hoja inahama sasa na kwamba si mawaziri hao watano wenye tuhuma mbalimbali, ni PM na kwa maana hiyo ni serikali yote Bungeni! Hili mimi siliungi mkono na silikubali. Nasema wazi hivyo kwa sababu, mimi nina imani na WM, nina imani na Rais - aliyemchagua WM, na nina imani na Mawaziri wengine wengi wazuri tu kwenye serikali hii, na msimamo wangu huu uko wazi sana tu.

Mbili, sioni sababu ya kuiingiza nchi kwenye wasiwasi wa kiutawala kiasi hiki. Na kwa kuwa wabunge wa CCM kwenye party caucus tulikuwa tayari tumeishaambiwa kwamba kuna mawaziri wameamua kujiuzulu wenyewe (tena siyo wale watano, ni wanane kabisa) kutokana na tuhuma hizo na presha kutoka kwa wabunge wa CCM na wengine, sikuona sababu ya mimi kusaini hoja ya Zitto (ambayo kikanuni ilikuwa imekosewa - kitendo kilichonidhihirishia wazi kwamba hakuwa na u-seriousness wa kutaka kweli kumuondoa WM bali ni baadhi ya mawaziri, sema alichomeka tu hiyo kauli ili kutia presha zaidi!). Zaidi ya hapo, ninaamini hoja hiyo ni nzito na kimsingi, kwa sasa, imegeuka kuwa ni mchezo wa kisiasa na media na haitofika popote! Kama Mhe. Mbunge Zitto alikuwa na nia ya dhati ya kumuondoa WM asingekurupuka kiasi kile, angewashirikisha watu wengi zaidi, hususani wabunge wa CCM, na kimkakati zaidi angewapa wabunge wa CCM walioibua hoja hizo za kuwataka mawaziri wang'olewe na hapo angefanikisha malengo ya kumuondoa WM na serikali yake Bungeni. Kwa namna ilivyo hawezi kupata support ya wabunge wa CCM na kwa kuwa sisi ndiyo majority, hoja hiyo haitopita - na hii itaturudisha kule kule kwenye nilichokisema kule twitter kwamba hoja hii ni ......politically right but technically flawed!

Jamani, hoja ya kumuondoa WM madarakani siyo kitu kidogo, siyo kitu cha mchezo, ni lazima ujipange. Ukweli ni kwamba rafiki yangu Mhe. Zitto hakujipanga kuifanikisha (bila shaka yeye mwenyewe analielewa hili vizuri - he is smarter than this, I know him!)

Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic! Mfumo wa Bunge letu ni wa Westminster, na hivyo kuna kambi ya Upinzani (yenye interest ya kutaka kuiangusha serikali inayotawala) na Kambi ya Serikali (ambayo ina interest ya kutaka kuilinda serikali yake). Kwa maana hiyo sisi wabunge wa CCM tuna jukumu la kuilinda Serikali inayopatikana kutokana na sisi kuwa majority. Serikali ni lazima i-enjoy majority status ndani ya Bunge ili nchi itawalike kwa amani na utulivu, japokuwa haimaanishi kuruhusu ubadhirifu na ndiyo maana kwenye Party Caucus wabunge wana nguvu na fursa ya kusema chochote dhidi ya serikali ya Chama Chao. Kuna wengine wanataka Bunge liwe Bunge huru (ama 'An Indipendent Power House') disregarding political opinions/inclinations/affiliations na serikali iwe serikali, hii haiwezekani kwa katiba tuliyonayo leo. Tubadilishieni kwanza katiba na mfumo wa kufanya kazi ndipo mtutake tufanye hayo mnayoyatamani.

Nadhani nimejiweka wazi bila unafiki, sasa tujadili kwa hoja siyo kwa hisia na matusi kama hatukwenda shule vile.

Wakatabahu,
HK.

HK nasikitika sana kwa uliyoyasema chini ya kivuli cha dini yangu tukufu, pia nakujibu kwa uthabiti kwa kuwa mimi ni mzalendo, siasa nimesoma darasani na wala si kwa kuambukizwa, nafahamu sana siasa ya chama chako kwani imenilea mimi na wazazi wangu, nafahamu upendeleo ulopata kuingia bungeni, lkn naomba nikujibu kwa kifupi sana na tena kwa uchungu wa rasilimali za nchi hii na hatma ya Tanzania ijayo,


Zitto hakuipinga CCM na ndiyo maana alikataa lawama asipewe Raisi kwani yeye akishateua majukumu yanahamia ktk usimamizi wa majukumu na kubebebwa na Waziri mkuu na waziri husika, kama angeipinga CCM basi angemghalifu rais, alichokisema ni mawaziri husika kuwajibika/shwa au plan B waziri mkuu kuachia ngazi, hili ni wazo la kizalendo na si kichama, sasa wewe unajibu kichama na si kizalendo, wewe unaonesha una miungu wawili CCM na Allah, na wewe ni mnafiki kwa kuwa upo tayari kuita nyeusi ranga nyeupe ili usimuudhi bwana mkubwa, ni mnafiki kwa kuwa CAG ameonesha kinadharia na kivitendo kuwa fedha zimeliwa lkn wewe unakata tena hadharani, lkn sikuhukumu kwa kuwa unaabudu siasa, unamakosa mengi siwezi kumaliza kusema, tunaelewa cc c watoto samahani
 
Need i say more... kaka umemaliza yote. so sad hao wasomi wetu wanapokuja na hoja zaifu zilizokosa mashiko. sitaki kuamini kama ndio aina ya viongozi wetu hao. na hapo utashangaa anajiita yeye PATRIOT.

regards

NB: jamani vilaza wote wa aina hii mkiwa mnakuja na hoja zenu dhaifu. muwe naandika kwa lugha za kwenu ili watu wa mataifa mengine wasielewe walau tufiche aibu hii.

fredwash
 
Nilivyomuelewa majebere baadhi yetu hatujibu hoja au kuuliza swali kwenye hii thread ya jamaa ila tunaishia kumkashifu..
Unajua kuna watu humu sijui ndio wanaona ni sifa kutukana wabunge? Mtu kajitokeza badala ya kutumia nafasi yao ya kumkaanga kwa maswali wao wanarukia kutoa matusi, ndio maana viongozi wetu wanatuona kama makondoo wa kupewa majibu mepesi mepesi.
 
hongera kwa kua msomi MD, MPH MBA duh si mchezo...ila ulivyoandika hapo nilidhani hujaenda shule mpaka nilivyoona hapo chini qualifications zako...haya mzee kaa mkao wa kula utapewa uwaziri na wewe very soon sa sijui utaanza kujenga/kununua nyumba kwanza au utaanzisha kampuni hewa kila la kheri...
 
Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini safi mkuu, bila shaka unakusudia kutuambia CCM IS A BIG PROBLEM mh mkuu wa chama nae aliwahi kuhofia wabunge wa ccm kwenye issue muhim ya muswada wa katiba. sasa tukisema 2015 tuiondoe ili nchi yetu iwe sawa, utaacha unafiki na kuungana na wengi?
 
Mkuu kila nikisoma hii comment yako nacheka sina mbavu!
Uyu kijana kweli ana masihara!hahahaahah

Mkuu LR
Huyu mtu anatuchezea kabisa na tusipo kuwa wakali kwa uzembe kama huu nchi yetu itaangamia..

He's not serious at all..

Maisha ya watanzania yeye anafanya 'Political goose chase' na anakiri kabisa kwa arrogance ya madaraka na immunity which is actually absolute impunity aliyopewa na wananchi!! Leo sijui ni wananchi wangapi ambao wanaishi below poverty line tokana either na uzembe au ufisadi unaofanyika Serilkalini, halafu analeta maskhara hapa!!

Huyu hafai kabisa kuwa kiongozi!!
 
Uchangiaji huu "vernomous" hata kama tumechoshwa, hauleti tija kwenye mijadala. Nasikitika na ninachokisoma kwenye hii thread, kinawanyima watu haki ya kutoa hoja ambazo zinaweza kumrekebisha mtu. Matusi, kejeli, n.k. havitamfanya mtu yeyote achukue misimamo tunayotaka aichukue. We must argue and not shout, insult, degrade, look down, etc.

KipimaPembe, mi sioni tatizo la style watu wanayotumia kuwasilisha hoja... Infact kaianzisha lugha mbaya mwenyewe kwa kudharau shule zetu...hisia na matusi hazina uhusiano na shule-hata viongozi wa ukweli e.g. Nyerere msomi (PhD) wa kweli alitumia hisia sana kumkabili Mwinyi (CCM), Kenyatta etc.

Na TUSI KUBWA zaidi kwetu ni kutukana INTERLIGENCE zetu kwa utetezi tasa km huu, hasa kudharau maslahi ya wananchi in the interest of the status quo
 
Uchangiaji huu "vernomous" hata kama tumechoshwa, hauleti tija kwenye mijadala. Nasikitika na ninachokisoma kwenye hii thread, kinawanyima watu haki ya kutoa hoja ambazo zinaweza kumrekebisha mtu. Matusi, kejeli, n.k. havitamfanya mtu yeyote achukue misimamo tunayotaka aichukue. We must argue and not shout, insult, degrade, look down, etc.

Jamani tujifunze uungwana!
Na wewe ni wale wale tu akili ziko likizo au either umezifungia kabatini, sasa hapa ndio umechangia nini katika topic husika?

Ndio nakusikia wewe leo eti kwamba keyboard nayo inashout!!:nono:
 
Mhe. sana Kigwangallah,

Baada ya Rais na Mwenyekiti wako Kiwete kwenda mbele ya CC na kuomba baraka za kuvunja Baraza la Mawaziri kwa HOJA YA CHADEMA kupitia Zitto Kabwe una hoja gani kutetea upu.pu wako???

Hii imedhihirisha UNAFIKI MKUBWA wa Wabunge wa CCM wewe ukiwa ni mmoja wao. Shame on you!!!
Napenda kukufahamisha tu kuwa pamoja na Udaktari wako IQ yako haifikii hata 0.25 ya Mhe. Zitto Kabwe. Wewe ni sawa na kihiyo yeyote ambaye hajaenda shule. Peace!
 
kigwangalla kati ya watu wanafki wewe ni no one.. yani unavyokana sio mnafki kama unasema sijaiba mbuzi nimeiba mtoto wa mbuzi. shame on you wewe ndio mp mwenye ndoto za kuigeuza nzega kama ulaya duuh..
 
kama mti ungekatwa, ungeanguka, ungetukuta chini ... ndio wasiwasi wa wabunge wa CCM. Tumeamua kukwea juu sijui mtapaa hewani!!
 
Kama Kumuangusha Waziri Mkuu na serikali yote Bungeni na kukimaliza kisiasa CCM si kuyapokea mabadiliko, basi nimeshindwa. wamekosea mawaziri watano (or rather wanane) wewe utake kuiangusha serikali yote, lini tutafanya mambo ya maendeleo? Mimi sikubaliani na huo mtazamo, na kwa kuwa nimeuweka wazi sina unafiki ndani yake, so just take it or leave it!

Haya sasa angalia,serikali usiotaka kuangushwa sasa hivii imeshaangushwa, sasa utaipeleka wapi sura yako. Bora usingeleta mada hii hapa. Ungepeleka tu Hulu Facebook
 
Back
Top Bottom