Majibu ya JK yamekwepa hoja!

yaani mwenzetu unaota mchana
eti historia na huyo obama anaejibu front ana kwa ana itaitwaje hiyo yake, huyu jamaa anajitayarisha siku saa na majibu, wa nini huyu sie jamani,

matatizo ya nchi yako wazi yanajulikana sasa hakemei wala hazuii badala yake anajibu maswali hiyo ndio nini
 
kweli kabisa mi mwenyew sikuzima simu tangu mwanzo mbona sikupokelewa, nae huyu asijibu maswali afanye vitendo bwana
 
hakuna cha record hapa,nilichogundua wana CCM wanataka kumuongezea umaarufu mwenyekiti wao kupitia mrango wa nyuma,majibu yake sijui ni nani aliyelizika nayo? yote ni kutafuta umaarufu tu, ina maana hiyo mbinu ameigundua leo? hatudanganyiki tena, Puttin wa russia ndo aliyeweza mchezo huo kwa kikwete bado sijaona.
 
Hivi Nyerere alipokuwa akienda vijijini na mijini na kufanya gumzo hilo halikuwa sawa na hili la Kikwete kwenye Redio? Je alipokuwa akienda Nkrumah Hall na kuwekana mieleka na Wasomi na ujibu maswali, hiyo haitambuliki?

Je Mzee Mwinyi na vikao vyake vya wananchi Ikulu, Lumumba na mabaraza ya Wazee kuongea na wananchi ana kwa ana nalo halijulikani?

Kama mtasema ni wa kwanza kutumia teknolojia, nitawaelewa, lakini kuonngea na kujibu hoja za Wananchi eti yeye ni wa Kwanza, huo ni uongo na UNAFIKI na zaidi ni kujikombakomba na kujipendekeza!
Kuna Kila Dalili yale mambo ya Mwaka 2005 kujirudia maana kuna baadhi ya vyombo vya habari Tanzania viliwahadaa Watanzania kwa kusema na kuchochea mambo ya Jk kama vile ni Chaguo la Mungu
 
tunavyofuata mambo bila ya kuangalia undani wake ndio maana tunashindwa hata kuwa na uwezo wa kimawazo,leo hii kikwete kujibu maswali mawili matatu kwenye tv,watu wasema ni historia,
kwanza jiulize,je kuongea kwenye tv na wannchi wawili watatu ndio njia bora ya kujua matatizo,kero,machungu,mapendekezo,au dukuduku za watu(fikiri hili huku ukilinganisha na njia za kawaida kama,mikutano ya uso kwa uso na wananchi, au wawakilishi watendaji wa rai, sio wazee walio jaa elimu huria)
pili,miaka minne imepita toka awe madarakani na hajawahi kufanya mambo haya sasa umebaki mwaka mmja kabla ya uchaguzi ndio tanamwona anataka kuongea moja kwa moja na wananchi,je hii sio kampeni ya uchaguzi?
tatu ,hakuna uchambuzi wa kiasi gani amefanikiwa kupata undani wa matatizo ya wananchi na njia gani bora /mbovu za kuwasiliana zaidi na wananchi zilizojitokeza ktk huu muundo?
mwisho je swala la utatuzi wa hayo matatizo liko wapi?hii ndio lengo kubwa la hayo mawasiliano,au nakosea?
 
Jamani hii kweli ni historia kwa kipindi hiki ambacho taifa linakumbwa na misukosuko mikubwa.
Taifa lipo pabaya linakumbwa na hali kubwa ya umasikini na ufisadi. mzee kashindwa kabisa kujibu maswali ya watanzania walio wengi, ambao wanahoji juu ya hali yao ya umaskini itaisha lini, hali inayokithiri ya ufisadi itatokomezwa lini?
Maana mtu anaulizwa juu ya ufisadi tena sio dagaa ni ule ufisadi papa, yeye anajibu generaly eti kesi za rushwa zimeongezeka mahakamani. kwa nini asituambie lowasa, chenge, rostam na wengine watapelekwa lini mahakamani? ili warudishe fedha zetu. Kwa nini asituambie wale wababaishaji bandarini aliojigamba anawafahamu kwa majina watafukuzwa lini na hatimaye washitakiwe? na wale pia wauza madawa ya kulevya ambao alipelekewa majina yao ni wakina nani? watakamatwa lini?
Anaulizwa hali ya chama anasema mambo ni shwali wakati ukweli kila mwenye macho haambiwi tazama, anaona tu kuwa hali ya chama ni taaabani. chama kinaposhikwa na kuendeshwa na wenye pesa anasema ni shwari? chama kinakuwa si mali ya wanachama watu wachache wanataka kumnyanganya kadi mwanachama mwenzao hali ni shwari? jamani tuache ya historia tuangalie taifa letu linaelekea wapi? kuweka historia hakuna maana kama hali ya wanjonge itaendelea kuwa duni.
Mimi nafikiri mzee kaona hali ngumu na hii ni mikakati ya kushafisha njia 2010. Maana hata namna ambavyo simu zilikuwa zinapokelewa inaleta mashaka kwani simu zilikuwa haziingiliani na mazungumzo. halafu hivi huyu jamaa siku hizi tuseme amekuwa jiniasi sana kukariri data kiasi kile. au maswali haya yaliandaliwa majibu hivyo alikuwa na maswali kabla. ( wajinga ndio waliwao)
Halafu swali ambalo ni specific kwa mfano swali la kigoma kuna haja gani kujibu mpaka asikoulizwa ruvuma nk. au ni jinsi ya kupoteza muda na kufanya aonekane anajibu vizuri sana. hapana kama mimi ningelikuwa msahihishaji basi nafikiri unajua angepata ngapi ya mia. ( swali na maksi mbili unajibu kurasa nane unafikiri maksi zitaongezeka). Hapa ni kwa kiswahili tuachane na vituko vya siku ile anahojiwa na kabinti ka CNN.
Jamani tanzania hii umaskini umezidi kuna maswali ya wakina mama ambao wako kijijini hospitali ni umbali wa km 30, hawana redio wala umeme video wanaangalia kwa walanguzi wanaowatembelea kipindi cha mavuno tu. tena wanaangalia kwa malipo ya mazao( namaanisha kisado cha mahindi au mpunga). Hawa ni watanzania wenzetu ambao rais wao amewatenga. Anasema anaongea na watanzania watu hawa hawajui hata kama kuna raisi anaongea maskini. Leo nimesikitika kwani nimepokea barua kwa posta eti wananiuliza hivi kikwete amesema ataleta lini hospitali? Wanamaswali mengi mno. je watayafikishaje?
Mafanikio ya ziara moja wapo ni ya kuongea na tajiri eti alete chandarua kila kaya tanzania? Jamani hivi ninyi mnakubaliana na jibu simple kama hili? chandarua? Aibu!!! hivi tujiulize kuna haja ya kuwa ombaomba kiasi hichi. hii ni laana au ni kukosa ......, hivi tuchukue pesa inayotumika kwenye uchaguzi tu ya kununulia kanga zenye picha na maandishi ambayo nadhani kwa makusudi yanatengenezwa ili zikivaliwa picha na maandishi chagua sisi yanakuwa kwenye makalio. haziwezi kutupatia chandarua kwa kila mtanzania. sio katika kaya tu bali ni kwa kila mtz. Tuachane na hizo je mabilioni yanayoibiwa benki kuu je? Rada? Ndege ya rais? Madini? Yanayowatesa watanzania wenzetu mpaka wanapoteza maisha. Yote haya ni mabilioni ya fedha sasa kuomba chandarua! Tumefika sehemu mbaya. Watu wanaiba pesa zaidi ya ambazo tunaenda kuomba kwa kununulia chandarua tunasema tunawajua kwa majina. Halafu tunatabasamu sana tu. Tunaenda kuomba chandarua?
Tunasahahu wakina mama wanaokosa vitanda kwa ajili ya kujifungua mpaka walala chini, Hawa ni watanzania jamani kwa nini tusikirie matatizo haya jinsi ya kutatua. Tunakimbilia kuomba misaada ya kutudhalilisha.
Jamani tutaomba mpaka lini wakati Mungu ametupa kila kitu madini, maziwa, bahari, wanyama, mapango, misitu na watu wa kutosha milioni kama 40 hivi. hivi hatujiulizi watu kama uingereza ambao waliendelea na kufikia kuitawala dunia kwa kutumia time management tu. tusome maendeleo ya nchi kama singapore, china, japani nk.
Kuna nchi zimefanikiwa kwa kuwa na rasmali watu tu. je hizi nchi zingefikiria kuomba hata chandarua zingefika zilipo?
next time tumuulize hivi alipojibu swali huko majuu kuwa hajui kwa nini tz ni maskini? alitaka msaada wa nini? maana kahaidi maisha bora. sasa tena hajui chanzo cha umaskini atunongoneze hatutamuuliza hewani ilikua gia ya kuomba nini?
 
Nilifikiri ni peke yangu aliyelistukia ishu hilo!
Tido Mhando alikuwa keshakula dili pale. Matangazo kibao na kupiga wimbo wa Tanzania bila sababu za msingi, ili tu muda uishe bila kuaibika. Wanaomsifu sielewi wana vigezo gani vya upekee wa hotuba yake!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom