Majibu ya JK yamekwepa hoja! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majibu ya JK yamekwepa hoja!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Sep 12, 2009.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Sep 12, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Majibu ya JK yamekwepa hoja! Thursday, 10 September 2009 17:14 *Beregu: Yalikuwa mepesi hayakukidhi haja za wananchi
  *Aonesha wasiwasi baadhi ya maswali kuandaliwa
  *Shekhe Issa: Napongeza Rais kukemea tishio la udini
  *Hamad Rashid apongeza utaratibu wa papo kwa papo lakini...
  *Slaa atetea waraka, Lipumba alia muafaka, Mrema apongeza

  Na Waandishi wetu

  BAADHI ya maswali aliyoulizwa Rais Jakaya Kikwete jana kwenye utaratibu mpya wa'Muulize Rais'kwa kupiga simu, kutuma barua pepe na kujibiwa moja kwa moja kupitia redio na televisheni hayakupata ufafanuzi wa kina kulingana na uzito wa masuala husika, kama ilivyotarajiwa na wengi, imedaiwa.

  Masuala yanayodaiwa Rais hakuyatoa majibu fasaha ni pamoja na vita dhidi ya ufisadi, safari zake za nje na nyaraka zinazotolewa taasisi za dini, ambapo imedaiwa majibu yake yalikuwa mepesi na hayakukidhi haja ya wananchi.

  Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CKD), Profesa Mwesiga Baregu aliliambia gazeti hili jana kuwa wananchi wengi waliondoka na kiu kubwa ya majibu kutokana na maswali mengi aliyoulizwa Rais Kikwete kutofafanuliwa kwa kina.


  Prof. Baregu ambaye ni mtaaluma wa masuala ya Sayansi ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, alisema majibu aliyotoa Rais Kikwete juu ya vita dhidi ya ufisadi hayalingani na uzito wa jambo hilo ambalo limechukua sehemu kubwa ya mijadala nchini takribani kipindi chote cha utawala wake.

  "Suala la ufisadi hakulitolea majibu ya kuridhisha kulingana na uzito wake unavyostahili, mpaka sasa ni moja ya mambo ambayo yametuchukulia muda mrefu katika kuyajadili bila kupata majibu sahihi.

  "Alizungumzia TAKUKURU tu kwa muda mrefu lakini ninavyojua mimi chombo hicho pia kiliwahi kutuhumiwa katika vita dhidi ya rushwa kuwa kinasafisha watu na hakifanyi kazi yake sawasawa, sidhani kama kuongelea chombo hicho pekee ilikuwa ndio jibu sahihi la swali lile juu ya vita vya ufisadi," alisema Prof. Baregu.

  Akizungumzia safari za mara kwa mara ambazo Rais Kikwete amekuwa akizifanya nje ya nchi, Prof. Baregu, alisema huenda Rais hakuelewa mantiki ya muuliza swali hivyo kujikuta akijibu tofauti.

  Alisema mantiki ya swali lile lilikuwa ni kutaka kujua umuhimu wa safari hizo ambapo muda mwingi Rais Kikwete amekuwa akitumia kuzunguka kuomba misaada kwa nchi tajiri kuisaidia Tanzania, badala ya 'kuiuza' nchi kwa kutumia maliasili zilizopo na kutafuta wawekezaji makini wanaoweza kusaidiana na serikali kuziendeleza.

  "Swali lile nahisi lilimpiga chenga, safari zake hizo za nje badala ya kutuingizia nafikiri zimekuwa zikitu-cost (kutugharimu) zaidi, badala ya kutumia fursa hiyo kutambulisha rasilimali zetu ziendelezwe ili zitusaidie wananchi wote, amekuwa akienda kuomba misaada.

  "Mbali ya kuwa unapoomba unajinyima uwezo wa kujitegemea, lakini pia hakuna nchi itakupatia kitu bure, hivyo swali halikueleweka, tutaendelea kuomba omba mpaka lini?" alihoji Prof. Baregu.

  Huku akionekana kuwa na wasiwasi na utaratibu uliotumika kuwasiliana na Rais, akisema kuwa inawezekana baadhi ya maswali yalikuwa yameandaliwa mapema, Prof. Baregu alisema suala la nyaraka za taasisi za dini nalo pia halikupata majibu muafaka.

  Alisema haoni mantiki ya majibu ya Rais Kikwete kuwa nyaraka hizo (waraka na Ilani ya Wakatoliki na Mwongozo wa Waislamu) zitaleta mgawanyo miongoni mwa wanajamii.

  "Nafikiri nyaraka hizo kwa jinsi nilivyozisoma na kuzielewa zililenga kupata viongozi waadilifu, na kwa hakika viongozi wa dini wana wajibu wao katika jamii kuhakikisha kuwa maadili yanakuwepo, sasa vipi zilete matatizo.

  "Ingawa pia viongozi wa dini walitakiwa kuunganisha nguvu zao za madai pamoja lakini kama taifa linalotaka kuwa na viongozi waadilifu basi Rais hakuwa na haja ya kuziogopa," alisema Prof. Baregu.

  Kwa upande wake, Shekhe Mohamed Issa ambaye ni mwanazuoni na mchambuzi mahiri wa masuala ya dini, alisema wanashukuru kuwa hatimaye Rais Kikwete amezungumzia masuala hayo baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

  Shekhe Issa, alisema Rais anastahili kupongezwa kwa hatua hiyo ya kuzungumzia hatari ambayo taifa linanyemelewa kwa kusukwasukwa na mambo ya kidini, lakini akahoji kwa nini hatua hiyo imekuja baada ya Waislam kutoa mwongozo wao?

  "Waraka wa Wakatoliki umetolewa karibu miezi tisa nyuma, tunaamini kabisa Rais Kikwete alijua kwa kutumia njia zake za kupata habari, anajua mambo ya waraka toka Januari, lakini alikaa kimya.

  "Lakini mara zote katika nchi hii hatari imekuwa inaonekana pale waislam wanapoamua ku-react (kujibu) katika msuala yao, hapo ndipo watu huanza kusema kuna hatari na hali hii imekuwepo toka awamu ya kwanza ya utawala wa nchi hii," alidai mwanazuoni huyo.

  Akizungumzia kuhusu Waraka na Mwongozo, alisema kuwa kimsingi demokrasia inahusisha mambo mengi ikiwemo kusikiliza na kusimamia maoni yanayotolewa na makundi ya kijamii.

  Alisema hakuna tatizo kwa makundi mbalimbali ya kijamii kama yale ya kidini, walemavu, wawindaji na mengine kutoa maoni na malalamiko yao kupigania haki au stahili yao, lakini itakuwa vibaya tu endapo kundi moja litatoa maelekezo ya kukandamiza maslahi ya makundi mengine.

  "Mfano watu wenye ulemavu wa ngozi, wenye virusi vya UKIMWI, Wahadzabe wote wanahaki ya kutoa maoni yao jinsi wanavyohitaji kutimiziwa stahili zao ilmradi tu, wasikandamize maslahi ya makundi mengine.

  "Hivyo hakukuwa na makosa kwa watu wa dini kutoa utashi wao kwa serikali au vyama vya siasa kuvionesha namna gani wanapaswa watendewe, ikiwa ni mojawapo ya michakato ya demokrasia.

  "Ilani ya Wakatoliki na Mwongozo wetu haina shida, labda tatizo liko kwa ule Waraka wa Kichungaji ambao umeweka mambo ya kidini zaidi, hivyo sisi tunasisitiza tutamchagua yeyote yule bila kujali dini ilimradi atimize haki zetu za msingi," alisema.

  Naye Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Bw. Hamad Rashid Mohamed amesema mbali na kuridhishwa na utaratibu mpya wa Rais Jakaya Kikwete kujibu maswali ya wananchi papo kwa papo kupitia vyombo vya habari amesikitishwa na kiongozi huyo kuwa kigeugeu katika suala la muafaka wa kisiasa visiwani Zanzibar.

  Bw. Hamad alidai Rais Kikwete ndiye kikwazo kikubwa cha kupatikana muafaka visiwani Zanzibar kwani wakati akilihutubia Bunge alisema kuwa ajenda zote tano zilizokuwa zinazungumziwa baina ya CCM na CUF zimemalizika lakini baadaye alikuja na ajenda ya sita ya kupigakura ya maoni kwa wananchi.

  "Rais Kikwete ni mwepesi wa kujua matatizo yanayojitokeza katika jamii lakini ni mzito wa kutoa majibu jambo ambalo ni hatari sana hasa kwa suala kama la muafaka visiwani zanzibar," alisema Bw. Rashid.

  Alidai kuwa vyama vyote katika vikao vyake vilikubaliana kwa pamoja mambo yote yaliyokuwamo kwenye ajenda tano ambazo walijiwekea lakini cha kushangaza wakati wakielekea mwisho, Rais akaja na ajenda ya sita ya kupigakura za maoni kitendo ambacho hakiwezi kuleta suluhu kutokana na udhaifu uliopo kwenye chaguzi zote.

  "Huwezi kuwa na 'double conflict' kwamba mazungumzo yamemalizika lakini unakuja na ajenda nyingine ya kura za maoni kwa madai kuwa kuna mabadiliko makubwa ya Katiba na utendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar," alisema na kuongeza kuwa shughuli ya uchaguzi Zanzibar haiaminiki kwa nini ulete kura ya maoni?

  Alisema dosari hiyo inaweza kuigharimu Zanzibar kwani wakatijitihada za muafaka zinaanza, aliahidi kufanyika kwa wiki tatu lakini cha kushangaza imechukua zaidi ya wiki 18 bila ufumbuzi.

  Naye Mbunge wa Karatu, Dkt. Wilbroad Slaa (CHADEMA) alisema Rais Kikwete amepotosha kuhusu waraka uliotolewa na Kanisa Katoliki kuelimisha wanaumini wao namna ya kuchagua viongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao mwakani kwa kueleza kuwa una hatari kwa mustakabali wa Taifa.

  Dkt. Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, alidai Rais Kikwete alipaswa kusoma vizuri waraka huo na kuuelewa.

  "Rais alitakiwa kuusoma vizuri waraka huo kabla hajalizungumzia suala hilo mbele ya wananchi ambao wengi wa waliousoma, wameonesha kuukubali,"alisema.

  Alisema Rais Kikwete alipaswa kuwapongeza wanataaluma Wakatoliki kwa kundaa waraka huo kwani unalenga kutoa elimu kwa watanzania hususan katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu.

  "Nitamshangaa mtu yeyote anayepinga waraka huu kwani haufundishi kuchagua kiongozi kutokana na dhehebu au dini anayotoka bali unafundisha jinsi ya kumpata kiongozi asiyejihusisha na rushwa na ubinafsi," alisema Dkt Slaa.


  Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema chama chake hakikuridhishwa na majibu ya Rais Kikwete kwani alipaswa kuelezea undani wa suala la muafaka wa CCM na CUF lakini hakufanya hivyo.

  "Kwa kweli majibu aliyotoa hayajatufurahisha ... tumemwandikia barua zaidi ya nne kuhusu jambo hilo lakini hadi sasa hakuna hata moja iliyojibiwa," alisema Prof. Lipumba.

  Kuhusu waraka wa Kanisa Katoliki, Prof. Lipumba, alisema wameshangazwa majibu ya Rais Kikwete kwani pamoja na malalamiko yote vipo vipengele umuhimu vyenye manufaa makubwa.


  Akizungumzia ahadi ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania kama Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inavyoeleza, Prof. Lipumba alisema hali ya maisha inazidi kuwa ngumu siku hadi siku.

  Alisema, Rais Kikwete anakosea kutumia kigezo cha huduma za jamii kama afya na elimu kwani idadi ya vifo vya kina mama wajawazito na watoto inaongezeka siku hadi siku.

  Mwenyekiti wa Tanzania Labour (TLP) Bw. Augustino Mrema alisema kuwa, ufisadi uliokithiri nchini ndicho chanzo cha nyaraka zinazotolewa na madhehebu kwani watu wamechoshwa na hali hiyo.

  Alisema wananchi wamechoshwa kuona watu wachache wanafaidi rasilimali za umma na wengine wakiumia kwa umasikini wa kutisha.

  Hata hivyo, Bw. Mrema alimpongeza Rais Kikwete kwa jitihada zake za kupambana na mafisadi kwa kuwa ndiye rais wa kwanza kushughulikia kero hiyo na kumshauri kuongeza nguvu zaidi.Source: http://www.majira.co.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=1399:majibu-ya-jk-yamekwepa-hoja-&catid=34:kitaifa-tanzania&Itemid=57
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Sep 12, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  JK a-improve namna ya kujibu maswali. Naona hata mimi sikuridhishwa sana na jinsi anavyojibu maswali. Anatoa majibu shallow sana. Anajaribu kuiga style ya Nyerere ya utani bila mafanikio. Kwa upande wa Nyerere alikuwa na utani lakini alikuwa anatoa majibu ya uhakika!
   
 3. B

  Bull JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2009
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Nyerere aliwahi kujibu swali Gani??? Nadhani kweli wewe bado mtoto.
  Kwataarifa yako; Nyerere alikua aambiliki, na-haulizwi, always zidumu fikira zake, maswali hayana majibu ni msemo wake wa kawaida anapoulizwa maswali anakunyang'any'ganya kadi ya CCM
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Sep 12, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wewe ndio katoto sio ka jana ila ka leo! Pole sana! Huyu rais ambaye hajui kwa nini Tanzania ni maskini tutegemee nini toka kwake? Kazi tu kuendeleza umatonya huko nje na hajui kwamba hakuna msaada usiokuwa na gharama, whether ni za kiuchumi au kisiasa! Awamu ya nne tumeshaliwa, tusubiri awamu nyingine!
   
  Last edited: Sep 12, 2009
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono, Nyerere alikuwa haambiliki! Dikteta wa hali ya juu, na ndio maana akaifanya hii nchi kuwa ya mwisho (au sijui ya kwanza) kwa umasikini duniani!
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mtabwabwajaaaaaa.... lakini kwa EAC hakuna kama J.K.Nyerere. Nyote mnaweza kubwabwaja hayo kwa sababu tu mlisoma bure kwa juhudi za nyerere
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Katika southern sahara, ukiondoa Namibia, Botswana na SA, ni nchi gani mnayoiona iko juu kimaendeleo kuliko TZ?? au hamjatembelea hizi nchi na kujionea??

  Wakati mwingine msiongee tu kwa kuangalia data za WB na IMF, ukienda kwenye field mambo ni tofauti.
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hii nchi sasa inatakiwa ikamatwe na dikteta kidogo ili mambo yaende. Kikwete angeomba asigombee na ampendekeze Mzee John Pombe Magufuli.
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nani aliesoma wakati wa Nyerere? Ngumbaro nayo unaiita ni kusoma?
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Sep 12, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sure, ila udikteta huo usije ukawa kama wa His Excellent, Al-Haji, Field Marshall Dr Idi Amin Dada, V.C., D.S.O., M.C., Life President of Uganda!
   
 11. Sungi

  Sungi Senior Member

  #11
  Sep 12, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi ndiyo ilivyokuwa wakati Rais Jakaya alipoongea na watanzania (Live) moja kwa moja kupitia Redio na Televisheni na kuulizwa maswali mbalimabli na wananchi ili kupata ufafanuzi wa mambo kadhaa yahusuyo utendaji wa serikali na matarajio ya watanzania.
  Utaratibu huu umebuniwa kwa mara ya kwanza na Rais Jakaya na ni kwa mara ya kwanza toka tujipatie uhuru kutoka kwa wakoloni, Mh Rais alizungumzia mengi na kujibu maswali mengi kutoka kwa wananchi

  Lakini moja ya mambo aliyozungumzia ni uhuru wa wananchi kuzungumzia na kukosoa utendaji wa serikali na akazungumzia pia uhuru wa vyombo vya habari na kusisitiza vyombo hivyo kufuata maadili ya kazi zao bila kuandika habari za uongo na uchochezi, hili ni jambo jema sana kwani tunahitaji habari nyingi zaidi lakini pia tunahitaji habari za kweli na zenye upembuzi yakinifu ili jamii iweze kupata habari zilizo sahihi

  Tunakupongeza sana Mh Rais kwa uamuzi wako wa kuongea na wananchi huku ukiulizwa maswali mabalimbali na kuyajibu, kwa kutendo hiki umeandika historia mpya ya uhuru wa umma kupata habari na kutoa maoni yao juu ya uendeshaji na uboreshaji wa maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla tunakupa Heko kwa uamuzi wako huu na tunadhani utazaa matunda, tunakutakia mafanikio mema katika kazi zako za kila siku katika kujenga Taifa letu Tanzania.

  Source: CHAMA CHA MAPINDUZI - MAREKANI
   
 12. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Hivi Nyerere alipokuwa akienda vijijini na mijini na kufanya gumzo hilo halikuwa sawa na hili la Kikwete kwenye Redio? Je alipokuwa akienda Nkrumah Hall na kuwekana mieleka na Wasomi na ujibu maswali, hiyo haitambuliki?

  Je Mzee Mwinyi na vikao vyake vya wananchi Ikulu, Lumumba na mabaraza ya Wazee kuongea na wananchi ana kwa ana nalo halijulikani?

  Kama mtasema ni wa kwanza kutumia teknolojia, nitawaelewa, lakini kuonngea na kujibu hoja za Wananchi eti yeye ni wa Kwanza, huo ni uongo na UNAFIKI na zaidi ni kujikombakomba na kujipendekeza!
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Kwa maneno ya juzi ni kweli kabisa Muungwana ameweka record mpya ya kuwa muwazi, Mapungufu ya matendo ya Muungwana kiuongozi yanajadilika, lakini sio siri kwamba kwa aliyoyafanya juzi ameweka record, mnyonge mnyongeni,

  - Mwalimu alijaribu sana siku ile alipozungumzia mikingamo, pale Diamond Jubilee na kubabaishwa sana na Eda Sanga, lakini not even close na hii ya juzi. The only time Mwalimu alijaribu sana ni siku ile pale Kilimanjaro Hotel alipokuwa retired, aliposema kwamba aliwahi kumtoa uwaziri Chief Fundikira kwa sababu ya rushwa na alipoongelea wake wawili wa Sir George.

  Kukubali ukweli wa siasa sio dalili za unyonge, ila ni political maturity.

  Respect.

  FMEs!
   
 14. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Heshima mbele, Hoja yetu hapa ni Je ni kweli Mh. Kikwete ni Rais wa Kwanza kujibu maswali ya wananchi Live? Jibu sio kweli. Kwa hiyo haiwezi kuwa record. Kwasababu watangulizi wake, Mwalimu na Mzee Mwinyi tayari walishafanya hivyo. Nakumbuka Mwalimu alikuwa na utaratibu wa kujibu Maswali Kumi ya papo kwa papo kila alipoenda mikoani, haikuziita KERO yeye alisema anataka maswali na alitoa ufafanuzi. Nilimwona mafinga 1984 kwenye mkutano wa hadhara akijibu maswali ya wananchi.

  Suala la kuwa muwazi hilo ni comperative na subjective issue, naweza kusema inatagemeana na mtazamo wa msikilizaji kwa hiyo ni opinion za msikilizaji, Wakati wengine wanamuona JK ni muwazi wengine watampa Jibu la US Congressman Joe Wilson kwa Obama Juzi. Kwa hiyo JK kujibu maswali ya wananchi haiwezi kuitwa record labada teknolojia aliyotumia
   
 15. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145


  Mtaniwia radhi nikiwauliza tena . Hivi kweli JK alijibu maswali kwa jinsi mnavyo elewa maana ya swali na majibu yake ? Hakika kama ni mtihani naamini JK asingefaulu . Siamini kama alikuwa anajibu maswali pale .
   
 16. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
   
 17. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2009
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Nina mashaka na jinsi simu zilivyokuwa zinapokelewa.. naona mkuu alikuwa anapewa vi - note kuul;izwa km simu inayouliza swali fulani ataipokea ama la. Maswali aliyojibu siyo hasa wananchi tulitaka kujua, binafsi nilishindwa hata kupata njia kwani line muda wote ilikuwa engaged.
   
 18. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kama kweli hiyo tunaweza kuiita historia that will be very interesting. Naona hata Ben Mkapa aliweka historia kwa kuita watu makini wamuulize maswali na kuyajibu, na yeye mwenyewe kuwauliza maswali nakumbuka niliwahi kuona ITV. So anyone can make history, not that hard, as long as it is close to the election date. I wonder how that benefits a Tanzanian, and how does that improve peoples lives.
   
 19. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Maneno hayo ndiyo sasa ya kuuliza wanazi wa siasa za ajabu ajabu na maji taka . Nakaa ningoje majibu .Thanks mkuu
   
 20. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Inawezekana pia waulizaji walikuwa wameandaliwa, tutajuaje!? Serikali yaweza kuandaa watu kuuliza kutoka mikoa mbalimbali wakiwa tayari na maswali yaliyoandaliwa na hivyo yanajulikana. Huu ni wasiwasi wangu tu. Laweza kuwa changa la macho.
   
Loading...