Majibu ya IKULU dhidi ya Tanzania Daima kuhusu ndege ya Rais na safari ya Davos

"Tatu, nivigumu kujua Gazeti la Tanzania Daima limepata wapi habari kuwa safari hiyo yasiku nne inagharimu kiasi cha sh. milioni 300. Ukweli ni safari ya MheshimiwaRais Kikwete na ujumbe wake ni ya siku nane, kama tulivyoeleza jana, ambakoatahudhuria mikutano ya WEF na ule wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Afrika (AU)mjini Addis Ababa, Ethiopia atakapowasili Jumamosi, Januari 28, 2021".

Hapo kwenye Red kumbe tatizo ya typo erro hata Kurugenzi ya mawasilano ikulu mnachapia?hii ni aibu iliyoje hakuna proof reading?Mnasaisha makosa na nyinyie mnarudia makosa hayo hayo.
"Daima Uongo hata ukiupaka mafuta utabaki kuwa ungo tu"

 
Du! jamaa anaponda mali ya nchi kweli kweli! milioni 300 zote hizo? si angetuma tu wawakilishi watatu tu ili fedha nyingine anunue vitanada na mashuka hospitalini.
 
me nlishangaa kuona imeandikwakwenye TOP PAGE eti Davos iko sweden wakati iko switzerland=uswis.pia eti shirika la Qatal badala ya Qatar,waziri NDUNDU badala ya Nundu,huu ni ubabaishaji,inabidi jamaa waombe radhi

waandishi wa habari sio miungu, smtms wanakosea....unapofanya interpretation of words, hata km maneno yamekosewa au umefanya wrong citation kitu cha msingi tunachoangalia je mwandishi alikua anakusudia nini? Ujumbe nimeupata haijalishi makosa hayo!
 
Wadau. Nadhani ni 80 percent ya wana jf waliobahatika kusoma majibu ya ikulu kuhusu yaliochapishwa na tanzania daima. Kiukweli ni kwa ikulu haikujibu kitu zaidi ilijiabisha tu kwa kutoa majibu mepesi na yasiyo na tija....kwa kifupi majibu ya ikulu ni mepesi mno ukilinganisha na umuhi wa stor yenyewe. Haya ni maoni yangu tuu. Nawasilisha.
 
leo ni zamu ya FF kutetea ubabaishaji wa ikulu hajibu hoja na kazana nonsense matter haya binti tutafika hata kama tutakuwa tumechoka ila tutafika tu
Mkuu usiumize kichwa kujibishana na watu kama hao,kwani hawawezi kuzuia upepo wa mabadiliko unaokuja kwa kasi ya ajabu.
Soma sainecha yangu hapa chini.
 
Pamoja na makosa ya kiuandishi....lakini ahsante Tanzania Daima kwa kumtoa nyoka pangoni! tena nyoka mwenyewe ni kibogoyo tu
hana meno wala sumu
 
Yap! Nilisoma. Walijikita zaidi kukosoa spelling errors kuliko kujibu hoja.
 
Wala haishangazi gazeti la Tanzania daima ni la chadema na hapa Jf wanachadema unategemea majibu ya Ikulu yatapongezwa?
 
Ok, 1: kama hatatumia milioni 300 atatumia milioni mia ngapi?
2: kwa kuwa unarekebisha sentensi i.e QATAL kuwa Qatar, je nini maana ya kuonana na WAKUBWA ?
3: huoni kwamba miradi ya wafadhali haileti maendeleo ya kweli ? Mradi wa Mbarali uliendeshwa kwa tija sana na JICA , ukafa
baada ya wao kuondoka, sasa mnaleta SAGGOT, matokeo si yatakua yaleyale?
4: Safari ya JK haitakua ya siku nne Uswisi. itakua ya siku ngapi Uswisi?
5: Kwa nini ameondoka ameacha hali ya mgomo wa waganga ikiwa tete?

Swali la nyongeza: CT Scan Muhimbili inatengenezwa lini?

naumia kuendelea kujihakikishia kuwa nchi yetu hatuna viongozi wanaoihurumia nchi, kwani jamaa angeahirisha safari na hiyo hela wakalipwa madactari si mgomoungeisha? au na wao wamekuwa wanafunzi wa UD?
Nakumbuka JK alikuwa waziri wa mambo ya nje before being Presdaaa, so nahisi now amepata cheo na kuwa raisi wa mambo ya nje!
 
mtoa hoja kakimbia hoja yake alikuwa anapima upepo au alikuwa anajaribu kushindanisha Tanzania Daima na Ikulu
 
Siwezi kimbia, na nitatetea hoja ya ngu kwa nguvu zote bila kufungamana na chama chochote, siku zote serikali inatakiwa kuwa deep zaidi inapoutaarifu umma na si kutoa majibu mepesi mepesi pasi na sababu za msing.
mtoa hoja kakimbia hoja yake alikuwa anapima upepo au alikuwa anajaribu kushindanisha Tanzania Daima na Ikulu
 
Hivi kwa nini watanzania Hatuna umoja wa kutuwezesha kukataa huu ujinga?

Wenzetu wa ngapi wanaotegemea Hospitali za serikali wanakufa coz madaktari hawapewi haki zao na sisi tunawaaangalia tu kama si wenzetu vile?

walimu wakitaka kugoma tunawwwcha wenyewe kama hatuathiriki na madai yao na wakati almost kila mtu anandugu mwalimu, na waTZ wote tunaathirika na hali za walimu coz ndo wanawalea watoto wetu na kushinda nao muda mrefu kuliko wazaziwenyewe?

Wanafunzi wakigoma ndo kabisa utasikia wamezidi hawa nao, na wakati ukweli ni kuwa hao watoto waliopo vyuoni ndo wanatuhusu waTZ wote hata kama ni undugu wa kunusa, na hali ya maisha tunaijua ni ngumu hata kuwasomesha, na zaidi ndo wataalam wanaotegemewa katika secta mbalimbali.

Je watanzania Tumelogwa jamani? hivi inaingia kweli kichwani majibu ya kijinga kama haya kwa watanzania kuhusu ufujaji wa fedha unaofanywa na Raisi?

Kwanini tusiandamane kwa amani nchi nzima kukataa haya yote? au tumesahau kuwa mafisadi hawajashughulikiwa na bado wanaendelea kuiba na kuishi kwa anasa?

kwa nini tusiandamane au hamjaona Tanesco wakipandisha bei bila sababu ya msingi sana (my take "kulipa deni la Dowans kinyemela") na hali ya maisha ya mtanzania yakizidi kuwa mabaya?

kwanini Tusiandamane kama gharama za vyakula zimepanda maradufu na kufikia hatua Watanzania wenzetu wengi wanakula mlo mmoja kwa siku? na JK anakula KUKU uswis?
 
Back
Top Bottom