Majibu ya IKULU dhidi ya Tanzania Daima kuhusu ndege ya Rais na safari ya Davos | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majibu ya IKULU dhidi ya Tanzania Daima kuhusu ndege ya Rais na safari ya Davos

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bibikuku, Jan 25, 2012.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Yafuatayo ni majibu ambayo IKULU imeyatoa dhidi ya gazeti la Tanzania Daima kuhusu utata wa ndege ya Rais 5H-One ambayo iko katika matengenezo nchini Marekani. Nimeona niwaletee habari hii kwa urefu wake ili msoma na kutafakari.

  TAARIFAKWA VYOMBO VYA HABARI
  Gazeti laTanzania Daima la leo, Jumatano, Januari 25, 2012, kwenye ukurasa wake wakwanza limechapisha habari yenye kichwa cha habari, "Ndege ya JK utata:Iko nje kwa miezi miwili. Serikali yakwama kuilipia."

  Miongoni mwayaliyoandikwa kwenye habari hiyo ni pamoja na "Ukataunaiokabili Serikali umesababisha kukwama kuilipia ndege hiyo maalum yaRais…Ndege ya Rais mahususi kwa ajili ya safari za namna hiyo imezuiliwa njebaada ya Serikali kukwama kulipia gharama za matengenezo yake…Kutokuwepo kwandege hiyo, kumesababisha Rais Kikwete na ujumbe wake wa watu 14, ulioondokanchini jana kwenda Davous, nchini Sweden kuhudhuriamkutano wa dunia wa uchumi, kuondoka na ndege ya Shirika la Ndege la Qatal".

  LimeendeleaGazeti hili la Tanzania Daima kudai kuwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa ndegehiyo ya Rais gharama za safari hiyo ya Rais zimeongezeka na ziara hiyo ya Raisya siku nne kuhudhuria mkutano huo itagharimu kiasi cha shilingi milioni 300.Aidha,Gazeti hili linadai kuwa mkutano huo hauna tija kwa taifa, kwamba Rais Kikweteamehudhuria mikutano hiyo mara nyingi lakini hakuna faida iliyopatikana kwataifa.

  Kwa hakika,maandishi na kauli hizi za ovyo na zisizokuwa za kweli za Gazeti la TanzaniaDaima zinalenga kuupotosha umma wa Tanzania bila sababu za msingi na hivyokuusababishia umma chuki isiyokuwa na msingi kwa Rais. Katika kuuelezea ummaukweli wa safari hiyo ya Mheshimiwa Rais Kikwete tunapenda kutoka ufafanuziufuatao:

  Kwanza, kama tulivyoeleza, kwa usahihi, katika taarifa yetu kwa vyombo vya habari janajioni, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekwenda katika mji/kijiji chaDavos, nchini Uswisi kuhudhuria Mkutano wa World Economic Forum (WEF) unaoanzaleo. Rais Kikwete hakuwenda katika mji wa
  Davous, nchini Sweden kamalinavyosema Gazeti hili. Aidha, Rais Kikwete na ujumbe wake umesafiri kwa ndegeya Shirika la Ndege la Qatar na siyo Qatal kama linavyoripoti Tanzania Daima.

  Pili,Serikali haijakwama, kwa sababu zozote zile, kulipia matengenezo ya kawaida (routinemaintenance) ya Ndege ya Rais. Hili limefafanuliwa vizuri na ipasavyo naMtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali, Rubani Kennan Paul Mhaiki jana.Isipokuwa nivyema kuongeza kuwa matengenezo ya ndege hiyo yalimalizika juzi tu, Jumatatu,Januari 23, mwaka huu, wakati ndege hiyo ilipofanyiwa safari ya majaribio (testflight) kule Savannah, Georgia, Marekani na wala siyo miezi miwili iliyopitakama linavyodai Tanzania Daima. Hivyo, madai kuwa ndege hiyo imezuiliwa nje kwamiezi miwili sasa kwa sababu ya Serikali kushindwa kulipia gharama zamatengenezo ni porojo tu zisizokuwa na msingi.

  Tatu, nivigumu kujua Gazeti la Tanzania Daima limepata wapi habari kuwa safari hiyo yasiku nne inagharimu kiasi cha sh. milioni 300. Ukweli ni safari ya MheshimiwaRais Kikwete na ujumbe wake ni ya siku nane, kama tulivyoeleza jana, ambakoatahudhuria mikutano ya WEF na ule wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Afrika (AU)mjini Addis Ababa, Ethiopia atakapowasili Jumamosi, Januari 28, 2021.

  Hivyo, sikweli kwa Gazeti hili kudai kuwa nauli tu na matumizi ya safari ya MheshimiwaRais ni shilingi milioni 300 kwa siku nne tu.
  Nne, TanzaniaDaima linadai kuwa safari za Mheshimiwa Rais mjini Davos hazina tija na walafaida yoyote. Huu pia ni uongo mwingine wa dhahiri wa Gazeti hili.

  Tunapendakukumbusha faida chache tu zilizotokana moja kwa moja na Mheshimiwa RaisKikwete kushiriki mikutano ya WEF kama ifuatavyo:
  (a)Moja, ni kubuniwa na kupitishwa kwa Mpango Kabambe wa Uendelezaji Kilimokatika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania wa Southern Agricultural Growth Corridorof Tanzania (SAGCOT) uliozinduliwa wakati wa WEF mwaka jana.

  Mpango huuutakaotekelezwa kwa pamoja na sekta binafsi na sekta za umma kwa kushirikishaSerikali ya Tanzania, Mashirika ya Kimataifa, Makampuni ya Kimataifa unalengakuleta faida zifuatazo:
  (i) Uwekezaji wa kiasi cha dola za Marekanibilioni 3.4 katika kilimo cha Tanzania na kuongeza uzalishaji wa kilimo hichomara tatu katika miaka 20 ijayo.
  (ii)Kuchochea uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara kwenye eneoya hekta 350,000.
  (iii)Kutengeneza kiasi cha ajira 420,000 za kudumu.
  (iv)Kuwatoa kwa namna ya kudumu kiasi cha watu milioni mbili katikaumasikini.
  (v)Kuleta usalama wa kudumu wa chakula kwa kuhakikisha kinapatikana chakulacha kutosha kwa Tanzania na nchi za jirani.
  (vi)Kuboresha miundombinu ya umwagiliaji, barabara, reli, nishati na bandarikatika eneo lote la Mradi wa SAGCOT.(vii) Kuwahakikishia wakulima masoko ya mazao yao,kuwawezesha kupata dhana za kisasa, na kuwaanzishia mifumo ya kisasa yaumwagiliaji.
  (viii)Kuingizia wakulima mapato ya kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.2 kilamwaka. (Kiasi cha dola za Marekani milioni 50 zinaendeleakuingizwa katika mfuko wa uanzishwaji wa Mpango wa SAGCOT utakaotelekezwa kwakuanzia katika maeneo ya Sumbawanga (Rukwa), Ihemi na Ludewa (Iringa),Kilombero (Morogoro), Mbarali (Mbeya), na Rufiji (Pwani)(b)

  Pili, ni uwekezaji kabambe wa kiasi cha dolaza Marekani milioni 20 katika mfumo wa upakuaji wa mbolea kwenye Bandari ya Dares Salaam unaofanywa na Kampuni ya Yara International, moja ya makampunimakubwa zaida ya uzalishaji wa Kampuni ya Yara International, moja yamakampuni makubwa zaida ya uzalishaji wa mbolea duniani.
  Yara International ni mmoja wa washirika wakubwakatika SAGCOT na uwekezaji wake unalenga kuhakikisha kuwa Tanzania na hatamajirani wanapata mbolea ya kutosha kwa ajili ya kuimarisha kilimo.

  (c)Tatu, mikutano ya WEF ni shughuli moja inayomwezesha Kiongozi wa Nchikukutana na kufanya mazungumzo na wakubwa wote duniani – wawe wa siasa, wabiashara, wa uchumi, wa uwekezaji, wa kijamii – katika jitihada zake zakuitangaza Tanzania kama kituo muhimu cha uwekezaji.

  Katika sikutatu zijazo, kwa mfano, Mheshimiwa Kikwete miongoni mwa watu wengine atakutanana Bwana Bill Gates wa Bill&Bellinda Foundation, Naibu Waziri wa Uchumi,Nishati na Kilimo wa Marekani Bwana Robert Hormats, Rais wa Benki ya DuniaBwana Bob Zoellick, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Australia Bwana Kevin Ruud, Mkuuwa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani Bwana Raj Shah, MtendajiMkuu wa Benki ya ABSA Bi. Maria Ramos, na Waziri Mkuu wa Thailand Bi. YingluckShinawatra.

  Tunapendakumalizia kwa kusisitiza, kwa mara nyingine tena, kuwa ni vyema Gazeti laTanzania Daima lijiridhishe na usahihi na habari zake kabla ya kuzichapishakama inavyoelekeza misingi mikuu ya uandishi wa habari na weledi wa kazi hiyo.Uandishi wa habari za uongo unaleta hofu na kuanzisha uzushi usiokuwa na sababuzozote miongoni mwa wananchi na hiyo siyo kazi ya uandishi wa habari.

  Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasilianoya Rais,
  Ikulu, DAR ES SALAAM.
  25 Januari, 2012
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sasa gazeti litafungiwa au ndio mshasema na ndio basi.?
   
 3. D

  Deo JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,190
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  SAGCOT itakuwaje ikiwa mjukuu wa Richmondi? Ni ile kampuni ya mpanda?
   
 4. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo huko pia JK kaenda kupitisha libakuli alilomnyang'anya matonya?
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Na kwa nini Ikulu isiweke utaratibu huu wa kujibu kwa kirefu na kwa ufasaha tuhuma mbali mbali zitokazo vyombo vya habari dhidi ya utendaji wa JK na utawala wake -- kama vile EPA, Radar, hiyo hiyo ndege ya rais ilivyonunuliwa, sakata la Jairo na mengineyo mengi?

  Au Ikulu hujibu tu yale yanayoigusa kasri hilo pabaya?
   
 6. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ukiangalia sana IKulu haijakanusha kitu, bali imetoa clarification kwa mambo kadhaa. Mfano haijakanusha kuwa JK na msafara wa watu 14 wanatumia sh milioni 300 kwa safari yao, bali imesema wanatumia siku nane na sio siku nne kama Tanzania daima lilivyoandika
   
 7. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Mtajijua wenyewe
   
 8. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kuna kila dalili kuwa hilo ni kubwa linalompeleka huko
   
 9. W

  We know next JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sasa huko ni kukanusha au ni habari nyingine iliyo hovyo hovyo kabisa!!
   
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  1. Mbona hamjataja gharama halisi rais atakazotumia ? 2) kwanini aende rais wakati waziri husika yuko?
   
 11. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  1. Mbona hamjataja gharama halisi rais atakazotumia ? 2) kwanini aende rais wakati waziri husika yuko? 3). J.k ni rais wa Tanzania ju raisi wa mambo ya nje?
   
 12. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sasa huyu Salva Rweyemamu anakataa kwamba gharama ya hiyo ziara siyo Shilingi 300 Millioni mbona hataji sasa kiasi halisi kwa kutoa mchanganuo?
   
 13. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nadhani anakubaliana na ukweli kuwa gharama ni sh milioni 300, lakini ni kwa siku nane sio siku nne
   
 14. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  sidhani kama amekanusha gharama, bali amekanusha kuwa sio siku nne ni siku nane
   
 15. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Masalia ya masurufu ya Safari hii matokeo yake ni kuongezeka kwa Semi trailer za LAKE OIL na DALBIT
   
 16. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,601
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Mmesubiri mpaka mchokonolowe ndo mje na mitakwimu yenu feki!, mara saggot mara mradi utagalimu shs........?.. Hovyo.
   
 17. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Na kama kukanusha kwa siku kumesababisha siku zilizotajwa na Tanzania daima kupungua mara mbili maana yake ni kwamba gharama halisi za safari zinaweza fika Milioni 600.

   
 18. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Ok, 1: kama hatatumia milioni 300 atatumia milioni mia ngapi?
  2: kwa kuwa unarekebisha sentensi i.e QATAL kuwa Qatar, je nini maana ya kuonana na WAKUBWA ?
  3: huoni kwamba miradi ya wafadhali haileti maendeleo ya kweli ? Mradi wa Mbarali uliendeshwa kwa tija sana na JICA , ukafa
  baada ya wao kuondoka, sasa mnaleta SAGGOT, matokeo si yatakua yaleyale?
  4: Safari ya JK haitakua ya siku nne Uswisi. itakua ya siku ngapi Uswisi?
  5: Kwa nini ameondoka ameacha hali ya mgomo wa waganga ikiwa tete?

  Swali la nyongeza: CT Scan Muhimbili inatengenezwa lini?
   
 19. K

  Kanyigo JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 959
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  uhuni tu si ajabu ni m.700 badala ya 300 iliyotajwa na TanzaniaDaima.
   
 20. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  naona nao hawa wanatapa tapa tu
   
Loading...