Kuchasoni Kuchawangu
JF-Expert Member
- Aug 21, 2012
- 623
- 378
Najua mnaumia sana jinsi tunavyofanikisha kuleta maendeleo kwa wat wa Nzega.Halmashauri zote nchini huwa zina bajeti ya'capacity building' sema huwa hazipati pesa kwa ajili hiyo. Capacity building inasaidia kukuza weledi na uelewa wa watu na nishughuli nyeti sana katika kuleta maendeleo:in fact kwenye mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano, human capacity development (kuendeleza rasliman watu) ni kipaumbele, na mpango huu unatokana nailani ya uchaguzi ya CCM. Sisi katika halmashauri tulipopata pesa kutokana naushuru wa huduma kutoka mgodini tulitumia akili sana kusema tuziweke katika akaunti maalum ya fixed deposit ili izae na itupatie pesa kwa ajili ya semina na ziara kwa waheshimiwa madiwani (ambazo kila mwakahuwa haziji kwenye bajeti). Pesa ya mwanzo iko pale pale. Kuna watu walinipinga sana wakati nikianza harakati za kudai pesa hizi wakiwemo viongozi wa chama na watu wanaotamani nafasi niliyonayo kwa sasa,walisema wanasubiri wajifunze kutoka kwangu aina mpya ya siasa na uongozi, sasa wameona naamini wamejifunza. Nashangaa leo wamekuwa mstari wa mbele kudai wanajua tena kuzipangia matumizi pesa hizi.Kuna watu walipinga ziara ya madiwani na wabunge kwenda Dodoma kufuatilia maswala mbalimbali yanayohusiana na ufuatiliaji wa hizi pesa,leo wanaibuka na kujidai wanajua zaidi matumizi yake.Kuna watu wanaomba hizi pesa wajenge mradi wa CCM (w) hata utaratibu hawaelewi kuwa hilo haliwezekani,hii ni mali ya umma siyo ya CCM. Yote haya yanaibuka leo kwa sababu watu hawaelewi utaratibu na wanaongozwa zaidi na chuki dhidi ya Kigwangalla na mafanikio anayoyapata katika utekelezaji wa majukumu yake.Wana Nzega na watanzania muwakatae hawa na msikubali wawavuruge.