Azim Sokoine
JF-Expert Member
- Aug 20, 2014
- 1,379
- 2,533
alifukuzwa au aliahirisha mwaka?Samahani wapendwa, naona kama kuna harufu ya vita binafsi kwa hawa ndugu wanaozungumzia jambo hili. Sipendi kwenda huko lakini kwa maneno machache tuu nijaribu kuangalia kati ya wasomi wenye shahada nyingi na wasio nazo waliowahi kuongoza vizuri nchi.
Namkumbuka Lyatonga Mrema sijui kama alikuwa na shahada alipoongoza wizara fulani na nikimlinganisha na aliepo leo kwenye wizara husika sijui mnapembuaje mnapozungumzia shahada zenu! Nadhani labda niite tuu karatasi mnazopewa mkikaa pale mlimani kwa muda fulani.
Sitaki kuamini kwamba kila aliyepita pale kawekeza kichwani !! Kuna wengine aibu hata kuwatambulisha kitaaluma " kuna mkuu wa wilaya fulani huko tanga aliziita degree za ch...". Hii ni kutofautisha nini kinakutambulisha kama umekaa pale ukatoka na nini kichwani.
Kuna wengine wanaitwa madoctor huku lakini kiwango chao cha maamuzi na upembuzi wa mambo bora wangeishia form two. Mifano mnayo ya kutosha. Kila anayesoma hapa anamjua mmoja au wawili ama kadhaa katika hili.
Hebu tuangalie hoja ya maji ubungo,Mnyika ni mbunge wa ngapi tangu uhuru?
Wakati mnaomba kura za uraisi mlisemaje? Ile meli kule mwanza imeshalowekwa ziwani?
Kigoma imeshakuwa dubai?
Hivi hichokitu walichoshindwa kukifanya sisiem kwa miaka 52 huyu Mwampamba na Juliana ndiyo wataweza?
Hata kama watanzania ni wajinga sana lakini tunaangalia kabla ya mkutano nilikuja na nini kichwani na baada ya mkutano naondoka na nini?
Itafika mahali hamtapewa nafasi kuzungumza matusi, mwulizeni nchemba kule igunga watu waliondoka. Hamzungumzi hoja mnaongea mambo ya chupini. Hayabadilishi maisha ya kesho.
Kina Nape walizunguka nchi nzima wakiimba ufisadi hebu leteni mrejesho! Wapo wapi. Nyie mtazunguka mkiimba nini habari itakuwa kiporo hiyo.