Majibu kwa Mtatiro juu ya hoja yake kuwa ACT ndio kikwazo cha ushindi wa UKAWA

Hansen Nasli

JF-Expert Member
Mar 18, 2012
886
225
MAJIBU KWA MTATIRO MCHAMBUZI ALIYEJAA MAHABA HADI ANASHINDWA KUTOA FACT NA KUTUTOLEA VITUKO HADI WATOTO WANAULIZA YUPO DARASA LA NGAPI?

Hoja hii hapa ya Kaka yangu Mtatiro ndio inayojibiwa, nimechukua kipande kidogo tu alichoishambulia ACT kuwa imekuwa kikwazo kwa ushindi wa UKAWA na kushindwa kutuwekea tafiti anayosema CUF ilibebwa na CHADEMA katika uchaguzi Mkuu wa 2015.

Aise my braza Mtatiro yaani sijaona analysis uliyofanya zaidi ya kuonesha vituko hebu niambie ACT unasema iliharibu Mpango wa UKAWA kwani ACT ilikuwa kwenye mpango wenu? Badala useme CHADEMA iliharibu ushindi wa UKawa segerea unalia na ACT Ambayo haikuwa kwenye mpango wenu.

Tuzungumzie JIMBO la Kasulu Mjini ulilolitolea matokeo kama mfano CCM kumshinda mgombea wa ACT kwa kura 3000 na kura hizo 3000 na kitu kuchukuliwa na UKawa, kama dhamira ni kuitoa CCM Huoni huyo mgombea wa UKAWA ndio aliharibu ushindi wa ACT kwa kuzipokonya kura 3000 za ACT ambazo zingeishinda CCM?

UKAWA Mngekuwa na dhamira ya kweli ya kuitoa CCM mngeijibu barua ya ACTwazalendo ya maombi yao ya kujiunga UKawa. Shida nyie mnaojiita upinzani mnaongozwa na chuki na ubinafsi mkiendelea hivi tusitegemee mabadiliko yeyote zaidi ya kuzidi kuua upinzani kwa kuchochoea migogoro. Tujifunze kwa wenzetu Afrika na Dunia wanaungana kuunganisha nguvu kukitoa Chama tawala nyie mnafikiria wengine wawaunge nyie tu hata kama hawafaidiki na muunganiko huo na wala hamuwahitaji mnataka wawafuate tu bila kujua hata malengo yenu ni yapi, na wanaowafuata kesho mnawasimanga mmewabeba.

My braza Julius S. Mtatiro tulipata uhuru ili kuuondoa utumwa Ila kijana kama wewe uliyeenda shule bado unawaza kitumwa kweli? kuwa eti ushindi wa CUF ni nguvu ya CHADEMA na sio nguvu ya ushirikiano UKAWA halafu cha kuchekesha unajichanganya tena kuwa NCCR NA NLD hawakuwa na ujenzi mzuri wa kujenga base za Chama chao na wagombea wao ndio maana CHADEMA ilishindwa kuwabeba.

Naomba nikuachie homework hizo base zilizojengeka za hivyo vyama viwili ndani ya UKAWA (CUF na CHADEMA) Vilijengwa wakati gani na Chini ya viongozi gani??

Jenga hoja kikubwa kamwe huwa halaumiwi mtu au taasisi ambayo haipo kwenye mpango wako au wenu wala hamna makubaliano yeyote, ACT haikuwa na makubaliano yeyote na UKAWA mlaumiane UKAWA wenyewe na sio ACTWAZALENDO.

Mwisho nakubaliana na hoja inayosema 'Tanzania kusoma ni kupata Sifa tu na sio kuelemika'
 
Mgango

JF-Expert Member
Oct 27, 2016
2,344
2,000
Mimi ninadhani mtatiro yuko sahihi ila wewe hauifahamu vizuri act na huyo anayejiita kiongozi mkuu wake. Ni vyema u waulize wanaomtazama vizuri kijana huyo watakueleza vizuri sana juu ya u ndani wa usaliti wake kama alivyofuta Yuda kwa Bwana Yesu
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,965
2,000
Mtoa mada hajui malengo ya ACT yalikuwa nini na Zitto ni mtu wa aina gani.
Zitto hata wenzake alio anzisha nao ACT wamesha mjua na wanajitenga naye
 
idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
23,912
2,000
Tunajua lengo la Chadema ni kuuwa upinzani na kuwa chama pekee cha upinzani Tanzania.

Tunajua Mtatiro pamoja na umahiri wake wa uchambuzi wa siasa za Tanzania lakini linapokuja swala la Chadema hana tofauti na vijana waliopiga deki barabara Lowasa ili apite.

Hatimaye naona siasa za mikakati miovu ndani ya Chadema, kupitia mtalaamu wa siasa za mikakati Lowasa.!
 
Nov 29, 2016
96
125
Mtatiro yupo sahihi,,,,wew ndiyo unamtindio wa ubongoo,,,maadui wa tatu wa mabadiliko ni act na zito wake,Dr slaa na Prof mapumbaaa nawachukia sana
 
Yohana Kilimba

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
8,116
2,000
Tunajua lengo la Chadema ni kuuwa upinzani na kuwa chama pekee cha upinzani Tanzania.

Tunajua Mtatiro pamoja na umahiri wake wa uchambuzi wa siasa za Tanzania lakini linapokuja swala la Chadema hana tofauti na vijana waliopiga deki barabara Lowasa ili apite.

Hatimaye naona siasa za mikakati miovu ndani ya Chadema, kupitia mtalaamu wa siasa za mikakati Lowasa.!
Naona hii propaganda ya CHADEMA Kuhusishwa na eti kutaka kiviua Vyama Vingine vya Inazidi Kushika Kasi...Ajabu Wanaoieneza Wanasahau Kuuliza ni Nani Anayempa Ulinzi Limpumba na Kumuunga Mkono Anapoendelea Kukipasua Chama Cha CUF Katikati!
 
chabusalu

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
7,564
2,000
MAJIBU KWA MTATIRO MCHAMBUZI ALIYEJAA MAHABA HADI ANASHINDWA KUTOA FACT NA KUTUTOLEA VITUKO HADI WATOTO WANAULIZA YUPO DARASA LA NGAPI?

Hoja hii hapa ya Kaka yangu Mtatiro ndio inayojibiwa, nimechukua kipande kidogo tu alichoishambulia ACT kuwa imekuwa kikwazo kwa ushindi wa UKAWA na kushindwa kutuwekea tafiti anayosema CUF ilibebwa na CHADEMA katika uchaguzi Mkuu wa 2015.

Aise my braza Mtatiro yaani sijaona analysis uliyofanya zaidi ya kuonesha vituko hebu niambie ACT unasema iliharibu Mpango wa UKAWA kwani ACT ilikuwa kwenye mpango wenu? Badala useme CHADEMA iliharibu ushindi wa UKawa segerea unalia na ACT Ambayo haikuwa kwenye mpango wenu.

Tuzungumzie JIMBO la Kasulu Mjini ulilolitolea matokeo kama mfano CCM kumshinda mgombea wa ACT kwa kura 3000 na kura hizo 3000 na kitu kuchukuliwa na UKawa, kama dhamira ni kuitoa CCM Huoni huyo mgombea wa UKAWA ndio aliharibu ushindi wa ACT kwa kuzipokonya kura 3000 za ACT ambazo zingeishinda CCM?

UKAWA Mngekuwa na dhamira ya kweli ya kuitoa CCM mngeijibu barua ya ACTwazalendo ya maombi yao ya kujiunga UKawa. Shida nyie mnaojiita upinzani mnaongozwa na chuki na ubinafsi mkiendelea hivi tusitegemee mabadiliko yeyote zaidi ya kuzidi kuua upinzani kwa kuchochoea migogoro. Tujifunze kwa wenzetu Afrika na Dunia wanaungana kuunganisha nguvu kukitoa Chama tawala nyie mnafikiria wengine wawaunge nyie tu hata kama hawafaidiki na muunganiko huo na wala hamuwahitaji mnataka wawafuate tu bila kujua hata malengo yenu ni yapi, na wanaowafuata kesho mnawasimanga mmewabeba.

My braza Julius S. Mtatiro tulipata uhuru ili kuuondoa utumwa Ila kijana kama wewe uliyeenda shule bado unawaza kitumwa kweli? kuwa eti ushindi wa CUF ni nguvu ya CHADEMA na sio nguvu ya ushirikiano UKAWA halafu cha kuchekesha unajichanganya tena kuwa NCCR NA NLD hawakuwa na ujenzi mzuri wa kujenga base za Chama chao na wagombea wao ndio maana CHADEMA ilishindwa kuwabeba.

Naomba nikuachie homework hizo base zilizojengeka za hivyo vyama viwili ndani ya UKAWA (CUF na CHADEMA) Vilijengwa wakati gani na Chini ya viongozi gani??

Jenga hoja kikubwa kamwe huwa halaumiwi mtu au taasisi ambayo haipo kwenye mpango wako au wenu wala hamna makubaliano yeyote, ACT haikuwa na makubaliano yeyote na UKAWA mlaumiane UKAWA wenyewe na sio ACTWAZALENDO.

Mwisho nakubaliana na hoja inayosema 'Tanzania kusoma ni kupata Sifa tu na sio kuelemika'
Binafsi sijaelewa povu lote hilo ni kwa ajili ya nini! Ni rahisi tu kuona uchambuzi unaoushambulia unaonyesha vikwazo vilivyojitokeza na kusababisha UKAWA kushindwa katika majimbo yaliyotajwa, ambapo hakuna ubaya kwa mchambuzi kukitaja ACT kuwa miongoni mwa vikwazo. Ni uchambuzi wa kawaida kabisa, kama ambavyo ACT nao wanaweza kuonyesha katika uchambuzi wao kuwa UKAWA ilikuwa kikwazo kwao!
 
GODLOVEME

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,629
1,500
Tunajua lengo la Chadema ni kuuwa upinzani na kuwa chama pekee cha upinzani Tanzania.

Tunajua Mtatiro pamoja na umahiri wake wa uchambuzi wa siasa za Tanzania lakini linapokuja swala la Chadema hana tofauti na vijana waliopiga deki barabara Lowasa ili apite.

Hatimaye naona siasa za mikakati miovu ndani ya Chadema, kupitia mtalaamu wa siasa za mikakati Lowasa.!
NI MIMI SIJAELEWA AU
 
zithromax

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
1,636
2,000
Mimi ninadhani mtatiro yuko sahihi ila wewe hauifahamu vizuri act na huyo anayejiita kiongozi mkuu wake. Ni vyema u waulize wanaomtazama vizuri kijana huyo watakueleza vizuri sana juu ya u ndani wa usaliti wake kama alivyofuta Yuda kwa Bwana Yesu
mtatiro ni zoba flani hivi , badala ya kusema ukweli cuf ilihujumiwa huko segera na aliyehujumu yeye kazawadiwa , ubunge wa maalum yeye anaangaika na ACT ambayo haikuwa na hata impact si ujuha huo
 
zithromax

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
1,636
2,000
Binafsi sijaelewa povu lote hilo ni kwa ajili ya nini! Ni rahisi tu kuona uchambuzi unaoushambulia unaonyesha vikwazo vilivyojitokeza na kusababisha UKAWA kushindwa katika majimbo yaliyotajwa, ambapo hakuna ubaya kwa mchambuzi kukitaja ACT kuwa miongoni mwa vikwazo. Ni uchambuzi wa kawaida kabisa, kama ambavyo ACT nao wanaweza kuonyesha katika uchambuzi wao kuwa UKAWA ilikuwa kikwazo kwao!
mkuu act ambayo haikuwa na hata 2% ya kura inakuwaje kikwazo kwa magiant kama ukAwa ni sawa na kusema sisimizi amenizibia njia nisiweze kuvuka barabara upande wa pili huo si uendawaZimu huo
 
chabusalu

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
7,564
2,000
mkuu act ambayo haikuwa na hata 2% ya kura inakuwaje kikwazo kwa magiant kama ukAwa ni sawa na kusema sisimizi amenizibia njia nisiweze kuvuka barabara upande wa pili huo si uendawaZimu huo
Mkuu utakuwa ama hujausoma huo uchambuzi, au hujaelewa tafsiri yake!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom