Maji ya AC yanafaa kuoshea vyombo na kufulia?

Nimewahi kunywa maji ya AC ni balaah!! niliwashwa sana kooni na nilipata kikohozi na mafua makali sana na kichwa kuuma.Haya maji yatakua hayafai kunywa kabisa cjajua khs kufulia nguo na kuoshea vyombo!!!ngoja waje wataalam wengine kwa majibu zaidi.

Ac ina vyuma vyenye madini hatari,vumbi,virainisho vya mota na feni,gundi kwa ajiri ya nyaya za mota ni hatari sana. Ulikuwa kilaza sana kaka,ungepata madhara makubwa ndio zingekusogea.
 
Maji hayafai mkuu utapata matatizo na familia yako, maji yanapita kwenye mazingira machafu sana. Vumbi, wadudu, moshi kilakitu kinachovutwa huko ndani kinarudinkwa huko kwenye condenser na maji yanapita hapo pia. Nakushauri utumie kwa mambo mengine sio kunywa na kupikia.

Atumie kwa mambo mengine yapi? Atawazie? Unawezaje mshauri mwenzio atumie maji yanayotoka kwenye AC! Yale ni maji taka,hayana tofauti na maji kutoka migodini na viwandani. Yana kila aina ya uchafu wa mitambo.
 
Najua pressure kubwa na masikio ya wengi yapo Dodoma.. ila naomba msaada kwa wanajua hili..
Nilipo kunatatizo kubwa la maji ya bomba.. sasa nimefunga AC na tumejikuta tukivuna maji mengi sana kwa siku inafikia ndioo 5 za lita 20.. kwa kutumia maji yanayotiririka kutoka kwenye AC-

Swali ni je? Maji haya yanaweza kufaa kwa matumizi ya kuoshea vyombo au kufulia nguo.. nikimaanisha maji haya ya AC hayana madhara yoyote? ..

Nawatakia subira njema toka chama tawala

Umewahi tembelea kiwanda au mgodi? Basi huko kuna maji yanayotumika kupozea mitambo,kusafishia bidhaa n.k. Hayo maji hayana tofauti na maji kutoka kwenye AC. Nikiwa shule ya msingi mzee amewahi leta AC mbovu (SANYO) toka Ofisini kwake kwa utundu wangu nilifungua ili niibe mota. Ukifungua AC kasha lake lile kwenye yale matundu ya wavu utaona kila aina ya uchafu,nzi,vipepeo,memde,vumbi,utando wa buibui n.k. Hiyo feni inayopiga hewa,hewa hiyo hukusanywa,hupulizwa na kisha hugandamizwa ndani ya kasha hilo ndipo hutengeneza hydrogen mbili H2 na Oxygen moja 0 na ndipo tunapata maji (H20). Maji hayo hukutana na vitu hivyo,kutu,vumbi,utando,mende,buibui,vipepeo,virainisho vya mota,mabaki ya msunguano wa vyuma vya mota,grisi,kutu n.k. Hivyo maji hayo ni maji machafu sawa na yale ya mgodi wa dhahabu yenye mecury. Hapa ndipo tofauti yetu sisi na wazungu kufikiri inapokuja kwa muungwana kutumia maji haya.

Jaribio: Kagua pale ambapo maji hayo yameamwagikia kwenye sakafu au marumaru,yaache yakaukie hapo usiyafute,utakacho kibaini njoo ushee hapa na sisi watu wa bara la giza.
 
Hiyo nyumba ni jokofu la kutunzia samaki? utakuwa uliuziwa nyumba ya tafiri, nawaza hiyo ac ya kutoa ndoo tano za maji itakuwa imetengenezwa bulgaria.
 
Wakuuu Mimi naongea nikimaanisha wengime wanafanya utani humu. Mm nimeomba ushauri
 
Umewahi tembelea kiwanda au mgodi? Basi huko kuna maji yanayotumika kupozea mitambo,kusafishia bidhaa n.k. Hayo maji hayana tofauti na maji kutoka kwenye AC. Nikiwa shule ya msingi mzee amewahi leta AC mbovu (SANYO) toka Ofisini kwake kwa utundu wangu nilifungua ili niibe mota. Ukifungua AC kasha lake lile kwenye yale matundu ya wavu utaona kila aina ya uchafu,nzi,vipepeo,memde,vumbi,utando wa buibui n.k. Hiyo feni inayopiga hewa,hewa hiyo hukusanywa,hupulizwa na kisha hugandamizwa ndani ya kasha hilo ndipo hutengeneza hydrogen mbili H2 na Oxygen moja 0 na ndipo tunapata maji (H20). Maji hayo hukutana na vitu hivyo,kutu,vumbi,utando,mende,buibui,vipepeo,virainisho vya mota,mabaki ya msunguano wa vyuma vya mota,grisi,kutu n.k. Hivyo maji hayo ni maji machafu sawa na yale ya mgodi wa dhahabu yenye mecury. Hapa ndipo tofauti yetu sisi na wazungu kufikiri inapokuja kwa muungwana kutumia maji haya.

Jaribio: Kagua pale ambapo maji hayo yameamwagikia kwenye sakafu au marumaru,yaache yakaukie hapo usiyafute,utakacho kibaini njoo ushee hapa na sisi watu wa bara la giza.
umetoa maelezo yanayojitoshereza na yamejaa ukweli ndani yake naamini mleta hoja amepata kile alichokuwa anakiitaji.
 
Ngoja nitoe over view kidogo maana chili in dual a LA utaalam na so siasa unaongea tuu bila kua name fact

Mie ni engineer coet-udsm moja ya course ilikua refrigeration and air conditioning kwa hiyo nazungumza kama mtaalam na so maamuma

air ni mchanganyiko wa gase nyingi nyingi na maji.in simple language una weza uka ikamua hewa ikakupa maji.

naeleza function mbili za ac kutokana na mazingira yetu.kwa dar utahitaji cooling and dehumidification, yaani dar kuna joto na moisture content kwenye hewa in nyingi

(up to 75% ya hewa no maji kwa dar) kwa hiyo tuna hitaji kuipooza hewa up to 22 deg cnt grade pia kuyapunguza maji yaliyo kwenye hewa kwa 50%) kwa hiyo maji yanayotoka kwenye ac yamekamuliwa kutoka kwenye hewa kwa hiyo ni maji safi kabisa.

pia ukiwa mbeya utahitaji ac tofauti na ya dar kwa sbb moisture content in ndogo.kama utahitaji kupoza hewa basi uongeze moisture,yaani cooling and humidification

ntarudi kueleza jinsi maji yanavyotokea.kwa kifupi O'Shea vyombo yapo safi kabisa
 
Bado nahis siyo salama sababu gass zinazotumika R22 na r407 zina amonia ndani yake ambayo kiafya si rafiki
 
Kwani yale maji si nimatokeo ya baridi tu inayofuliwa.. inauhusiano gani na mchanganyiko wa hizo geses
 
Bado nahis siyo salama sababu gass zinazotumika R22 na r407 zina amonia ndani yake ambayo kiafya si rafiki

yale maji hayatoki kwenye hizo gesi, mfano rahisi chukua glasi weka maji ya baridi then iache, baada ya muda utaona ile glass ina tengeneza condensation, hilo kila mtu ana fahamu,exactly kina chotokea kwenye ac

kuna kitu kinaitwa dew point temperature, hii ni temperature ya air ambayo ndio sbb ya condensation,

tukizingumzia kwa mfano wa glass yenye maji ya baridi, ili uyaone yale maji yanayotokea pembeni ya glass ni lazima hii dewpoint temp ya air iwe kubwa kuliko ile temperature ya glass yenye maji ya baridi.

kuna water dispense ambazo hazitumii maji, una weka tu ndani ukitaka maji ya kunywa una kinga tuu, huweki kabisa maji, ila hii itafanya kazi dar es salaam, lindi, tanga, yaani ile mikoa yenye bahari. water dispense ya aina hiyo haiwezi kufanya mikoa kama arusha, mbeya, iringa.kinachofanyika hapo ni kama hayo maji una yoyaona yanayo dondoka kwa ac, yana hifadhiwa then poa kwa matumizi
 
vipi kuhusu ventilation zilizoko kwenye evaporator za material ya aluminium anyway sina utaalamu ila siwezi simama 100% kumshauri mtu kuwa ni safe
 
Kuna ofisi moja nilikuta mlinzi anapiga story na mwenzie kuwa hayo maji yanafaa kunywa kwani yamechujwa kama gongo
 
swahiba hiyo sio AC ni mtambo wa kutengeneza maji hehehe....lita 100 kwa siku.
 
Mkuu hayo maji ni sawa na distilled water so tafuta mashule ya sekondari uwe unawauzia waalimu kwa ajiri ya wanafunzi kufanyia practicals mimi nakumbuka wakati nkiwa chuo technician alikuwa anayatumia hayo maji,so hiyo ni dili asee
 
Kuna mtu hapa kaongea kitaalam sana landa inaweza kuwa na ukweli ndani yake kuwa hayafai kabisa.. ndio maan tunasema jf ni kila kitu
 
Nimewahi kunywa maji ya AC ni balaah!! niliwashwa sana kooni na nilipata kikohozi na mafua makali sana na kichwa kuuma.Haya maji yatakua hayafai kunywa kabisa cjajua khs kufulia nguo na kuoshea vyombo!!!ngoja waje wataalam wengine kwa majibu zaidi.
Khaa!! Ajabu sana. Siku hizi kuna vifaa vinatengeneza maji (water dispenser) kwa mfumo huohuo kama AC inavyofanya kazi. Yaani kukusanya unyevunyevu uliopo hewani na kugeuza kuwa maji. Labda haya maji ni halisi sana (pure water) kwa sababu hayana madini muhimu kwa mwanadamu. Btw labda kama ulikuywa ukiwa umelewa lakini haya maji ni salama sana kuliko hata cool blue. Ila kwa lita 100 kwa siku sijui labda uwe na AC ya BTU 12000 kwenye darasa la shule ya kata iliyopo Dar
 
Umewahi tembelea kiwanda au mgodi? Basi huko kuna maji yanayotumika kupozea mitambo,kusafishia bidhaa n.k. Hayo maji hayana tofauti na maji kutoka kwenye AC. Nikiwa shule ya msingi mzee amewahi leta AC mbovu (SANYO) toka Ofisini kwake kwa utundu wangu nilifungua ili niibe mota. Ukifungua AC kasha lake lile kwenye yale matundu ya wavu utaona kila aina ya uchafu,nzi,vipepeo,memde,vumbi,utando wa buibui n.k. Hiyo feni inayopiga hewa,hewa hiyo hukusanywa,hupulizwa na kisha hugandamizwa ndani ya kasha hilo ndipo hutengeneza hydrogen mbili H2 na Oxygen moja 0 na ndipo tunapata maji (H20). Maji hayo hukutana na vitu hivyo,kutu,vumbi,utando,mende,buibui,vipepeo,virainisho vya mota,mabaki ya msunguano wa vyuma vya mota,grisi,kutu n.k. Hivyo maji hayo ni maji machafu sawa na yale ya mgodi wa dhahabu yenye mecury. Hapa ndipo tofauti yetu sisi na wazungu kufikiri inapokuja kwa muungwana kutumia maji haya.

Jaribio: Kagua pale ambapo maji hayo yameamwagikia kwenye sakafu au marumaru,yaache yakaukie hapo usiyafute,utakacho kibaini njoo ushee hapa na sisi watu wa bara la giza.
mkuu umeacha wizi????
 
Back
Top Bottom