Maji ya AC yanafaa kuoshea vyombo na kufulia?

Maji ya AC yanafaa kuoshea vyombo na kufulia?

NI MTAZAMO TU

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
1,203
Reaction score
1,001
Najua pressure kubwa na masikio ya wengi yapo Dodoma ila naomba msaada kwa wanaojua hili..
Nilipo kuna tatizo kubwa la maji ya bomba.. sasa nimefunga AC na tumejikuta tukivuna maji mengi sana kwa siku inafikia ndoo 5 za lita 20.. kwa kutumia maji yanayotiririka kutoka kwenye AC-

Swali ni je? Maji haya yanaweza kufaa kwa matumizi ya kuoshea vyombo au kufulia nguo nikimaanisha maji haya ya AC hayana madhara yoyote?

Nawatakia subira njema toka chama tawala
 
Nimewahi kunywa maji ya AC ni balaah!! niliwashwa sana koo, nilipata kikohozi na mafua makali sana plus kichwa kuuma.Haya maji yatakua hayafai kunywa kabisa sijajua khs kufulia nguo na kuoshea vyombo!!!ngoja waje wataalam kwa majibu zaidi.
 
Hata kunywa yanafaa kabisa,ila hakikisha kuwa yanadondokea sehemu salama yanapokuwa yanatoka ktk AC,na pia hiyo AC isiwe na kutu kabisa,hayo maji ni soft water kwa maana ya kuwa hayana chumvi chumvi,maji yenye chumvi huitwa hard water,ukiona yanadondokea ktk mazingira ambayo ni unsafe basi yachemshe kwa FH Degree 100,yaani yachemke hadi kutokota ndo yatakuwa salama kwa kunywa.
 
Niliwahi kunywa kuna hali fulani niliisikia mdomoni na kooni sio ya kawaida, kifupi yaliniopesha.
 
Yanafaa,hasa kwenye rejeta za magari yanafaa zaidi,sababu hayana mchanganyiko wowote wa madawa,kwa kunywa hayafai kabisa.
 
Upo mahali penye shida ya maji ila umekuwa na uwezo wa kufunga AC yenye uwezo wa kutoa ndoo 5 za maji za lita 20 kwa siku ambazo kam ni kweli kwa haraka haraka umesave sh.200 X 5 kwa kupata 100! Mkuu kuna chunguza vizuri huenda umefungiwa bomba la maji na si AC maana kuna maswali yasiyo na majibu hapa!
 
hizo ac ziko ngapi ? Kama ni moja hadi kumi bado uwezi pata maji kiasi hicho umetudanganya mkuu. Hayo maji ni machafu huo ni weupe tu wa maji. labda kamwagie chooni
 
Kufulia yanafaa. Kupikia sijui japo nimewahi kupikia chai na ilikua poa tuu
 
Maji hayafai mkuu utapata matatizo na familia yako, maji yanapita kwenye mazingira machafu sana. Vumbi, wadudu, moshi kilakitu kinachovutwa huko ndani kinarudinkwa huko kwenye condenser na maji yanapita hapo pia. Nakushauri utumie kwa mambo mengine sio kunywa na kupikia.
 
hizo ac ziko ngapi ? Kama ni moja hadi kumi bado uwezi pata maji kiasi hicho umetudanganya mkuu. Hayo maji ni machafu huo ni weupe tu wa maji. labda kamwagie chooni

Atakuwa na central cooling huyo,ndio system yenye uwezo wa kuzalisha maji mengi, nje outdoor moja na indoor unit kama nane. Na indoor moja kwa saa1 inatoa maji 20ltrs.
 
Upo mahali penye shida ya maji ila umekuwa na uwezo wa kufunga AC yenye uwezo wa kutoa ndoo 5 za maji za lita 20 kwa siku ambazo kam ni kweli kwa haraka haraka umesave sh.200 X 5 kwa kupata 100! Mkuu kuna chunguza vizuri huenda umefungiwa bomba la maji na si AC maana kuna maswali yasiyo na majibu hapa!

hahahahaha! JF , unarudishwa kama ulivokuja ... hehehe!

huyu jamaa muongo
 
hahahahaha! JF , unarudishwa kama ulivokuja ... hehehe!

huyu jamaa muongo

Mara zote arts ya ku propose swali ama arguments inatakiwa iwe kubwa na isiyoacha shaka kuliko arts ya kujibu swali husika ili kuepuka majibu yenye uzito mkubwa kuzidi swali lenyewe...akisema anatutambia tunaotumia pangaboy kwamba kafunga AC tutaelewa ila hii ya kufunga AC ambayo seem imejengwa kwenye nyumba ya maana kisha ushindwe kuweka walau tank la lita 1000 kiasi cha kusubiri hayo ya AC ni kulishana matango pori!
 
Back
Top Bottom