Maji ubungo...... Dawasco kunani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maji ubungo...... Dawasco kunani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ba Brio, Sep 8, 2012.

 1. B

  Ba Brio Member

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jamani Dawasco mko wapi huku ubungo kibo/rombo/baruti/ maji hayatoki kwa zaidi ya miezi miwili sasa. Je kuna shida gani? Kwa nini msituarifu kupitia vyombo vya habari kuna shida gani? Huku ni kukosa uwajibikaji na kutudharau walipa kodi.(lack of resonsibility and accountability). Watanzania wenzangu hawa tuwafanyeje? Maana kesi za ngedere siku hizi hupelekewa nyani....!!!!
   
 2. m

  markj JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  sema wewe ndugu yangu! mana watu humu jf wanasifia kuwa kamanda wetu mnyika kalitatua hili swala, wakati maji kwa morogoro road kutoka kibamba huko mpaka ubungo hakuna kabisaaa miezi sasa! mh.mnyika katoa report inayoelezea jitihada zake lakini isome utaielewa jamaa kafwatilia mno, ila watu wengine wanaleta ushabiki kuwa katatua tatizo tayari kumbe bado lipo! sasa hivi tunakuwa hatuendi
   
 3. B

  Ba Brio Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu tatizo bado ni kubwa sana kwa kweli! Hizi mamlaka ni za kuvunjilia mbali tu maana hawajielewi. Siku moja nimeandika hapa immediately walaleta maji siku 3 mfululizo.Yalimwagika tu bure! Sasa hizo siku sehemu nyingine wanakuwa wanakosa maji na pia sisi hatuyahitaji kwa mfululizo huo maana tulishazoea yakitoka tunajaza vyombo vyetu tukisubiri wiki inayofuata tujaze tena. Ninachoona hapa ni kwamba hawa watu hawana ratiba nzuri au hawafuati ratiba kutuhudumia. Mgao upande mmoja tu kivipi???
   
 4. m

  markj JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  na chakunishangaza sasa hawa jamaa! ukipita kwenye maofisi yao utafikiri wafanya kazi na watekeleza majukumu, mana ni ma vx na magari kibao yamejazana kuingia na kutoka, mbwembwe nyingi. yani maji yamekuwa kero, wanakera sio siri, mh. kamanda mnyika juzi weekend alikuwepo mitaa ya mbezi kuzindua tawi la cdm, akaahidi kulishughulikia naona katoa taarifa fulani, tuvute subira, mambo yatakaa poa
   
 5. B

  Ba Brio Member

  #5
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hebu ngoja tuone kama kitafanyika kitu kaka.tatizo letu wabongo siyo wafuatiliaji. Maji/umeme inaweza ikatike mwezi na wala asitokee mtu kuuliza. Tumeshazoea maisha duni ya kutokuhoji maswala ya msingi ya haki zetu.
   
 6. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hakika matatizo ya maji katika maeneo mengi ya Ubungo hadi Mbezi ni makubwa sana na kila siku kuna story mpya ila maji hakuna.
   
 7. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,334
  Likes Received: 2,657
  Trophy Points: 280
  Suala la tatizo la maji kutatuliwa hapa Dar ni ndoto kutokana na uchakavu na teknolojia duni ya Dawasco na miundombinu mibovu ya Dawasa. Unaambiwa zaidi ya 60% ya maji yote yanayozalishwa Ruvu huwa yanapotea wakati wa kuyasafirisha.
  Ushawahi kujiuliza mitambo ya Ruvu ilijengwa kuhudumia idadi ya watu wangapi?
  Leo hii Dar kuna watu wangapi?
  Idadi ya watu imeongezeka na upotevu wa maji umeongezeka maradufu,hivyo hata mbunge angekuwa ni mkurugenzi wa Dawasco bado tatizo lingekua palepale.
   
 8. B

  Ba Brio Member

  #8
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wachina si walitandaza mabomba mapya? Huu uchakavu namna gani!
   
Loading...