Maji ni Mtego wa Umasikini (poverty trap)

Nimeisoma mada ya Mh. Zitto na kuielewa vizuri, jukumu la usambazi maji ni la wananchi na Serikali. Wananchi tunatakiwa kuonyesha juhudi fulani ili kuivutia Serikali kuongeza nguvu katika kutimiza lengo la kupata MAJI SAFI NA SALAMA.
 
Hapa watu tunaongelea maji jombaa.....haya mambo ya uchochezi pelekeni huko.
 
Tunashindwaje kuchimba visima kila ward ikiwa tuna pesa za kununulia Vichwa vya treni visivyokuwa na mwenyewe?
Unauhakika kwamba kila WARD ina maji chini ya ardhi?

Si kila mahala pana maji chini ya ardhi.
 
Unauhakika kwamba kila WARD ina maji chini ya ardhi?

Si kila mahala pana maji chini ya ardhi.
Unashauri nini kwenye zile Ward ambazo water table ipo karibu?

Kwenye zile Ward ambazo water table haipo karibu, unafikiri wanapata wapi maji kwa ajili matumizi muhimu ya nyumbani?

Kama wanayapata kwenye Ward iliyopo jirani yenye water table iliyokaribu, mtawasaidiaje hao watu na hiyo adha ya kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta maji?
 
Ushauri wangu ni kwamba.

1. Ufanyike utafiti kubaini maeneo yenye maji safi na salama chini ya ardhi. Utafiti uonyeshe kiasi cha maji kilichopo na uwezo wa kila chanzo.

2. Ufanyike utafiti kubainisha ni maeneo yepi yanafaa kupatiwa maji kutoka kwa kila chanzo kilichobainishwa.

Mfano. Iwekwe bayani ni wapi panatakiwa kupewa majo ya kimbiji na ni wapi panatakiwa kupata maji kutoka ziwa victoria. Tanganyika nk.

3. Mwisho miradi nikubwa ya kusambaza maji ianzishwe iwe kama ilivyo miradi ya REA au ya UMEME.

Kwamba tuaanza na wilaya hii na mwakani wilaya ingine inafuatia.

Hili la kutaka kisima kila kijiji ni kupoteza muda pesa na direction. Ni kwamba haiwezekani maana huko vijijini waliopewa visima wameshindwa kuvifanyia ukarabati na vimejifia.
 
Mwisho Wizara ya maji iajiri watu wa kusimamia miradi yao huko vijijini.

Wizara ya afya haikabidhi zahanati kwa wanakijiji.

Wizara ya kilimo inao wataalamu vijijini.

Wizara ya maji ikisha chimba kisima kijijini inaondoka. Hapo kisima hukosa mmiliki na huishia kujifia.
 
Jambo gani mojawapo Zitto alilosema ambalo wewe unatafsiri ni uchochezi?
Weka hapa tafsiri ya uchochezi.
 
Amini nakwambia. ..watu wamezoea maisha ya purukushani .

Ukiwawekea ustaarabu wanaharibu miundo mbinu. ..hasa visima.

Swala la kwenda kutafuta maji ni kichaka cha kufanya mambo mengi kijijini
 
Ni wajibu wananchi kujiletea maendeleo, na serikali INA wajibu mkubwa wa kusimania juhudi hizo za wananchi. Kuna mgawanyo, wa yapi yafanwe na wananchi na yapi na serikali. Bahati mbaya tunapishana ktk vipaumbele. Hakuna mbadala wa kupata maji zaidi ya mabomba, visima au mabwawa, lakini watalii kuja nchini wanaweza kuja nchini kwa ndege za mashirika mengine.
 
Bw. Zitto, Hao walioshindwa kumaliza tatizo la maji kwa miaka zaidi ya 50 huko vijijini wanapata kura nyingi sana huko kila uchaguzi. Kwa hiyo watu wa vijijini wako happy na hali yao hiyo. Leave them alone.
 
Bw. Zitto, Hao walioshindwa kumaliza tatizo la maji kwa miaka zaidi ya 50 huko vijijini wanapata kura nyingi sana huko kila uchaguzi. Kwa hiyo watu wa vijijini wako happy na hali yao hiyo. Leave them alone.
Nasikitika kwamba unawasemea watu wa vijijini tena kwa hasi! Vijijini wanaonewa sana, hata hizo kura usemazo naamini si za utashi wao. Wakati majumba mjini yanavunjwa kupisha magorofa, wao zahanati bati zinavuja!
 
Tanzania tumekuwa tukilalamika kwa muda mrefu kuwa tunawekewa vikwazo kwenye misaada kwa sababu ya Ushoga. Nikakumbuka magojwa makuu ya Tanzania kuwa ni Ujinga, Umasikini, na Kukosa maarifa (maradhi). Kama tumeshindwa kutofautisha kati ya ushoga na Tabia mbaya kweli wanasiasa na wasomi (phd na maprofesa) bado tunasumbuliwa na ujinga.

Nini Maana ya shoga (Gay)

> Ni mtu ambaye anaongea kama mwanamke na tabia zake zinakuwa kama mwanamke siyo ugonjwa wa kujitakia lakini lazima aheshimiwe kwa sababu yupo hivyo kutokana na maumbile na tabia zake

Tafsiri wa Watanzania (tabia mbaya)

> Tumekuwa tukimtafisiri shoga kama ni mtu ambaye anafanya mapenzi kinyume cha maumbile, 'hii ni tabia tu' ambayo mtu anakuwa nayo kwa kujitakia kwa hiyo ni tabia mbaya ambayo mwanamke na mwanaume wanayo kwa sasa.

Wapi tujitoe ujinga.

> Ni muda watanzania tukafocus kwenye mipango miji (Master plan) ili kuwa na mipango endelevu la sivyo tutasubiri sana kupata maendeleo na itakuwa less developing country milele (Shithole).
 
Change is hard but necessary, progress is never easy but always possible. JOE BIDEN
 
Jinsi ya kutatua matatizo matatu ya Mwl. Nyerere (Ujinga, Umasikini na Maradhi) - JamiiForums
 
WATER is not a poverty trap, DEMOCRACY is
 

Zitto umeongea point lakini naomba niongezee. Tatizo la Maji halitaweza kuisha mpaka tatizo la umeme nafuu nitatuliwe. Kitu kimoja ambacho watu wengi hawajui ni kwamba Maji safi na salama yanahitaji umeme. Tatizo letu ni kwamba umeme wa sasa wa Gas kwasababu ya mikataba mibaya ni gharama kubwa na ndiyo maana ni vema ku-support miradi ya umeme nafuu. Nchi yetu kwa hivyo tattizo kubwa ni umeme na sio maji. Tukiwa na umeme hatutakuwa na sababu ya kutoa maji mbali maana tutakuwa na uwezo wa kutumia pumps kuvuta maji. Lakini vilevile umeme utasaidia kusafisha maji. Nimeshangazwa sana mfano hapa Dallas ninapoishi hatujawahi kuwa na ugojwa hata mara moja wa maji wakati tunatumia maji ya bomba bila kuchemsha. Hivyo basi inaelekea pamoja na kuwa na maji inabidi tuwe na maji safi na salama. Lakini niongeze tu ukiangalia vizuri tatizo la elimu vilevile umeme ni tatizo maana tutaweka vipi technologia kwenye madarasa yetu bila umeme? Mitandao kama hii utapataje bila umeme, vitabu vya bei rahisi siku hizi ni kwenye internet tena kwa dunia nzima, lectures…..PHD papers …. Yaani umeme ni tatizo kubwa sana kwenye strategy yetu ya nchi.
 
Wanasiasa waliiharibu miradi kwa kuwabeba wakandarasi wengi wasio na sifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…