Maji Marefu Kuishitaki CHADEMA .....!!!!!

Maji marefu wewe ni msomi uliyebobea mpaka kufikia hadhi ya kuwa profesa, wanafunzi wako wa chuo kikuu wakiona hii habari hawataipenda kabisa.

Ha ha ha ha hahaha....... Chuo kipi hicho Mkuu????. Prof wa ukweli huyu! Mr "Long water". Ngoja tusubiri kesi!
 
Aende huko mahakamani.. Au awaloge kama anaweza.. Ati mganga Professor..! Kusema kweli ni aibu kubwa kuwa na mbunge (mwakilishi wananchi) ambae ni mganga wa kienyeji ambae ana kashfa kibao za utapeli.. Tunaelekea wapi kama Taifa..? Tutapingaje kuuawa na kutolewa viungo kwa jamii ya wananchi wenye ulemavu wa ngozi ikiwa ndani ya bunge tunao waganga wa kienyeji ambao wanahucika na kuchochea mauaji hayo..?
 
ninauhakika mbunge wa CDM angekwenda kwenye kambi ya CCM iliyo maeneo ya leganga pia,angepata kesi na angefunguliwa mashtaka yafuatayo
1.Amehatarisha amani kwenye CCM ngome
2.Amejaribu Kubaka Mvaa Hereni
3.Amekutwa na Bangi
4.Amekutwa na Siraha ya Kivita
Ila kwa kuwa ni CDM,haina uzito...
Majimarefu ulichofuata kambi ya CDM Elephant ni nini lakini wakati unajua ngoma inogile?...
 
inawezekanaje picha ya kutengenezwa ichapwe kwenye mwananchi na Tanzania Daima? mmh haya sijui hata hivyo huo muda ulipatikana wapi wa kwenda kuwasiliana na mwanasheria 'maarufu' ili kuishtaki CDM? Picha imeoneka ajuzi tu leo mahakamani.....
 
Maji marefu wewe ni msomi uliyebobea mpaka kufikia hadhi ya kuwa profesa, wanafunzi wako wa chuo kikuu wakiona hii habari hawataipenda kabisa.

ebu rudia tena,ni msomi? Mh labda elimu ya ma...ni
 
Mbunge pekee asiyejua kusoma wala kuandika,nadhani yuko na mwingine wa CCM Mkoa wa Iringa naye nio Tabula Laza
 
Anafikiri siasa ni Uganga wa Kienyeji? Amuulize Mkapa na wenzie . . .
 

yeah kikawaida wachawi huchomwa moto! alifuata nini kwenye kambi ya cdm??
 
hapo anasoma au anaangalia picha??
pete ka za adam amgawie moja mwenzie anataabika kaibiwa
 
Jamani, mahakama itakuwa Gamboshi na muongoza mashitaka atakuwa ni Dk Matunge

Kweli hii picha ni ya kuloga yeye alikuwa mbali picha imelogwa ikamsogeza kwa Nassari. Ni sawa tu kwa vile chadema walijua wanashughulika na mlozi wakamzidi
 
Maji marefu wewe ni msomi uliyebobea mpaka kufikia hadhi ya kuwa profesa, wanafunzi wako wa chuo kikuu wakiona hii habari hawataipenda kabisa.

Aaah aah hatari kweli kweli, huyu nae ni profesa! Naomba kujuzwa hiyo university ya kufundisha tunguli ipo mkoa gani maana nijuavyo huyu bwana maji marefu ana uprofesa wa kuruka na nyungo! Ni juzi tu hapo alipoamua kurudi kwenye fani ya kupaa baada ya kuimiss anapokuwa mjengoni. Hivi ile sheria ya kudhibiti profesa na madokta uchwara iliishia wapi?
 
Hivi utaratibu wa kuwachoma hawa wachawi moto uko kanda ya ziwa tu mbona huyu jamaa anajitanua sana?
 
Mimi nafikiri aulizwe vizuri kama madai yake ni ya kuona , kusikia au ramli? na kama ramli ajaribu ku update mitambo yake na kama aliifanyia overhaul hivi karibuni aangalie isije ikaw kapewa spea za wapiga ramli wa kichina?
 

jamani anahangaika kwenda mahakamani wakati ana njia mbadala??? si awaroge tu mwananchi wote??
 
ebu rudia tena,ni msomi? Mh labda elimu ya ma...ni
ndio, umesoma sahihi ni msomi aliyebobea na anakifedhehesha chama chake kwa kuwa ni mwanataaluma mahiri katika fani yake japokuwa huwa hawavitaji vyuo vyao hawa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…