sijakuelewa hapoUvumi ulioenea kuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Steven Ngonyani a.k.a. Prof. Maji Marefu (C.C.M) amefariki dunia
Sio wa kweli baada ya yeye mwenyewe kutembelea baadhi ya mitaa kuuthibitishia uma kuwa bado anahema.
Habari zinasema kuwa, uvumi huo uliwashtua wengi na kutokana na simu pamoja na watu wengi kufika nyumbani kwake ilimpasa mbunge huyo kutembea na Lap top yake ili kwa kadri alivyoweza-awaonyeshe watu kile kilichofanyika akiwa nchini India kwa matibabu.
Hata hivyo, shuhuda mmoja anasema kuwa hali ya mbunge huyo bado haiko sawa na ndio maana hayupo kwenye kikao kinachoendelea sasa DODOMA.
source: Wadau kutoka eneo la tukio. Korogwe
Mimi naomba Pro. Maji Marefu apate afya njema. Kuhusu suala la eti akifa jimbo litaangukia mikononi mwa CDM hilo kwa wilaya ya Korogwe vijijini bado maana wakazi wa kule ni wazigua ambao wamelishwa limbwata na CCM.
Ukianzia vijiji vyote vya Kwalokonge Magamba, Kweisewa, Masimbani, Toronto n.k bado muamko ni mdogo sana mpaka labda vuguvugu lipite kwanza.
Mchawi hafi ki-rahisi aisee!!
pole profangeondoka tu, mchawi mkubwa.