Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,239
- 4,272
Malamba Mawili maji ni ya mgao yanaweza maliza wiki 2 bila kutoka na yakitoka yanatoka usiku wa manane yakitoka kidogo kidodo, yanachirizika hayana kasi hata kidogo kiasi ambacho baadhi ya watu ambao nyumba zao zimepo kwenye miinuko kidogo maji hayafiki kabisa.
Kuna baadhi ya watu wana miezi hawajawahi kuyaona maji yakitoka kwenye nyumba zao, wanaishi kwa kununua maji yanayouzwa na magari kwa 15000 mpaka 20000 kwa dumu lita 1000.
Napata mashaka huenda hayo magari yakawa yanamilikiwa na baadhi ya watu wa idara ya maji na kusukuma maji kwa kasi ndogo au kutosukuma maji kuyaleta Malamba kwa wiki au wiki 3 au mwezi kabisa wakati mwingine ukawa ni mpamgo mkakati wao wa kuhakikisha magari yao yanapata wateja kila siku.
Wakazi wa Malamba Mawili wanateseka sana na maji, kwa sababu ya gharama wengi hulazimika kutumia maji ya chumvi yalichombwa chini ambayo si salama, kwani mengi huwa yanakuwa yana muingiliano na mifereji ya maji machafu.
DAWASSA tatueni kero ya maji Malamba Mawili, kama mnashindwa kuyasukuma kila siku angalau yawe yanakuja hata baada ya siku 2 na yawe yanakuja kwa kasi kubwa ili hata walio kwenye miinuko wapate, pia muache kuyaleta usiku wa manane.
Natoa wito kwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso awaagize DAWASSA washughulikie changamoto hii kwani mara kadhaa tumeripoti lakini bado kuna kujivutavuta katika kufanya maamuzi, huku sisi tukiendelea kuteseka.
Pia soma:
DAWASA wakiri kuwepo na tatizo la maji maeneo ya Malamba Mawili kutokana na kuwepo na vilima vikali wasema wanaendelea na jitihada mbalimbali za kufanya maboresho ya huduma za Maji katika eneo hili kwa kufanya mradi wa kuongeza msukumo wa maji kwa kulaza bomba lenye kipenyo cha inchi 8 kwa umbali wa KM 3.5 katika maeneo hayo lengo ni kuboresha huduma.
Zaidi soma: DAWASA yatoa ufafanuzi kuhusu changamoto ya maji Malamba Mawili

- DAWASA Kibamba wakaazi wa Malamba mawili hatupati maji, tumewakosea nini?
- Mwezi wa tano (5). Mbezi malamba mawili hatuna maji hivi serikali ina mpango gani na sisi?
- Maji Dar ni Shida isiyomithilika wakati Mto Ruvu umejaa!