KERO Maji hayatoki zaidi ya wiki maeneo yote ya Goba

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
7,289
Reaction score
11,788
Habari wakuu,

Kumekuwa na changamoto ya maji takriban week sasa Goba mtaa wa Tegeta A njia ya kuelekea kwa Bedui, na maeneo mengine yote ya Goba maji yamekuwa hayatoki na hata mtaani wanaouza hawapatikani kwa hali hii wananchi wa huku tunateseka sana, mwenye kujua chanzo cha hii kero atufungue.


 
Sad enough walitoa tangazo juzi kuwa maji yatakatika kwa saa 24, jumamosi hadi jumapili. Ajabu hadi leo hakuna taarifa yoyote.

Na maji yalikatwa siku nyingi kabla hata ya hilo tangazo. Niliwasiliana na Meneja huduma kwa wateja akasema atanirudia ila hakunitafuta tena.
 
Kumekua na changamoto ya maji takribanI week sasa Goba mtaa wa Tegeta A njia ya kuelekea kwa bedui, maji yamekua hayatoki na hata mtaani wanaouza hawapatikani kwa hali hii wananchi wa huku tunateseka sana, mwenye kujua chanzo cha hii kero atufungue.
Goba nzima hakuna maji Dawasa ukiwapigia hawana majibu, mara ooh tutakupigia huku wananchi tunateseka
 
Ni huduma gani ambayo kwa sasa unaona inaenda smooth bila kusuasua? Kipaumbele ni kulinda madaraka hayo mengine ni ziada.
 
Tulieni Mama Anaupiga mwingi.
Kwani Aweso anasemaje?
 
Ni huduma gani ambayo kwa sasa unaona inaenda smooth bila kusuasua? Kipaumbele ni kulinda madaraka hayo mengine ni ziada.
Dah wanatukosea sana kama hawazingatii kero za wananchi
 
Goba nzima hakuna maji Dawasa ukiwapigia hawana majibu, mara ooh tutakupigia huku wananchi tunateseka
Afu mbaya zaidi hata maji ya kununua kwa watu wa mikokoteni hakuna
 
Hata goba uwanjani/shule hatuna maji siku ya 5 leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…