DAWASA yatoa ratiba ya mgawo wa maji Dar

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,368
Reaction score
18,677
Kutokana na uhaba wa maji jijini Dar es Salaam, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imetangaza ratiba ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa mpango wa dharura kwa wakazi wa jiji hilo, hatua inayolenga kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa usawa wakati wa changamoto za uzalishaji na usambazaji.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa leo Jumamosi Desemba 13, 2025, mgawo wa maji umegawanywa kwa kanda mbalimbali zikiwamo Kimara, Mshikamano, Bangulo, Kisarawe pamoja na maeneo yanayohudumiwa na matanki makuu ya Kisanga, Salasala, Vikawe, Changanyikeni, Mbweni na Tegeta A.

Katika kanda ya Kimara hadi Mjini Kati, maji yatapatikana kwa siku ya Jumapili hadi Jumatano, yakihudumia maeneo ya Kimara, Ubungo, Kijitonyama, Mwenge, Muhimbili, Msasani, Masaki, Upanga na maeneo ya kati ya jiji.

Ratiba hiyo pia inaonyesha mgao kwa njia za Kimara–Tazara, Kimara–Magomeni na Kimara–Kibamba na Unyamwezini kwa siku ya Jumatatu.

Kwa upande wa kanda ya Mshikamano, mgao utahusisha maeneo ya Makabe, Mbezi Mwisho, Machimbo na Madafu/Takukuru, huku baadhi ya maeneo yakipata maji kwa siku mbili hadi tatu kwa wiki kulingana na njia ya usambazaji.
 
Attachments

Duh kweli Gundu naona zamu yetu ni Ijumaa na hadi leo hayatoki kwahiyo tusubiri hadi ijumaa tena
 
Tunamshukuru mama kwa maono yake. Tunasonga mbele...
 
Watu wananunua maji ya kunywa marekani watajuaje wananchi wanakosa maji
 
Baada ya miaka 60 ya uhuru jiji kubwa kama hili linapambana na mgao wa maji 😀
 
Hili la mgao wa maji kwa Mega City kama DAR mwaka 2025 kwa kweli linatia aibu mno
 
Duh kweli Gundu naona zamu yetu ni Ijumaa na hadi leo hayatoki kwahiyo tusubiri hadi ijumaa tena
Wanasiasa wa ngazi za juu ndio wenye haki ya kupata maji yauhakika. Raia wengine tuendelee kudumisha amani
 
Hii ratiba sidhani kama wanaifuata huku goba tunaenda week ya pili sasa hakuna maji kabisa
 
Back
Top Bottom