Maji Bwawa la Nyerere yafikia mita 136, uzalishaji umeme kuanza Januari 2024

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Mliojidai kuua legacy ya Magufuli mpo? Ukosefu wenu wa akili umesababisha mlie kila mnapoiona legacy ikimeremeta.


Morogoro. Kina cha maji katika Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) umefikia 136.3 kati ya mita 163 kinachopazwa kufikiwa ili kuanza uzalishaji.

Ujazaji maji kwenye Bwawa hilo litakalozalisha megawati 2115, ulianza Desemba 22, 2022 baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua.

Hadi kufikia juzi, ujazo wa maji umefikiamita 136.3 kutoka mita 71.5, Desemba 22 mwaka jana wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipozindua rasmi ujazwaji maji katika Bwawa hilo ambalo litakuwa na uwezo wa kuzalishaji Megawati 2,115.

Jana Jumamosi, Machi 11,2023, timu ya Bodi ya Maji Bonde la Rufiji na waandishi wa habari walifika kujionea hali ya mradi unavyoendelea.

Mhandisi Mkazi wa Mradi wa JNHPP, Rutengano Mwandambo alisema hadi kufikia mwishoni mwa Februari 2022 mradi kwa ujumla ulikuwa umefikia asilimia 83.

"Mtakumbuka Rais Samia alizindua ujazaji maji Desemva 2022 mwaka jana na hadi kufikia leo (jana) maji yamefikia mita za ujazo 136.3 kutoka usawa wa bahari," alisema

Mhandisi Mwandambo alisema ili uzalishaji uweze kufanyika lazima maji yafikie mita 163.

Kwa maana hiyo kwa sasa zimebaki mita takaribini 27 na yeye (Mwandambo) alisema,"kwa hali ilivyo hana shaka maji yatajitoshereza."

Alisema matarajio yao hadi kufikia Agosti mwaka huu,"tutakuwa tumemaliza kufunga mtambo wa kwanza. Wa pili utakuwa Oktoba na wa tatu Novemba au Desemba na uzalishaji wa kwanza wa majaribio Januari mwakani kwa mujibu wa ratiba."

Timu hiyo ya Bonde la Rufiji na waandishi wa habari walitembelezwa maeneo mbalimbali na kujionea jinsi maji yalivyojaa na kuanza tengeneza bahar na au ziwa na ufungaji wa mashine na shughuli zingine zikiendelea.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Bonde la Rufiji, Mhandisi Mhandisi Florence Mahay alisema ili bwawa hilo liweze kujaa lazima wasimamie na kuratibu shughuli za maji kwa sekta zote kutoka vyanzo vya maji na mito wanayoisimamia.

Mhandisi Mahay alisema ili hilo lifanikiwe,"ni kuhakikisha sheria ya mita 60 kutoka vyanzo vya maji haviharibiwi kwa shughuli za kibinadamu na wamekuwa wakiendelea kushirikiana na jumuiya za watumiaji maji ili kuwadhibiti waharibifu."

Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa wakulima, wafugaji na wananchi kwa ujumla kuwa walinzi wa vyanzo vya maji kwani kuviharibu kwa ubinafsi kuna athari kwa watu wengi.

Pia, alibainisha mkakati wa kuajiri vijana 50 waliopata mafunzo Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) watakaokuwa na jukumu la kuvilinda vyanzo vyote vya maji kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Alisema timu hiyo maalum ya watu 50 waliopata mafunzoJKT,"tutawaajiri kwa kushirikiana na Tanesco ili kuhakikisha tunavilinda vyanzo vya maji dhidi ya waharibifu."

"Sisi Bonde la Rufiji ambao ndio tegemeo la maji la Bwawa la Nyerere, tuwahakikishie Watanzania, litajaa kwa wakati na waharibifu wa vyanzo vya maji wanachukulia hatua," alisema

Naye Profesa Japhet Kashaigili wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ambaye amekuwa akifanya tafiti mbalimbali za uhifadhi wa mazingira na rasilimali za maji alisema kuna athari nyingi zinazababishwa na shughuli za kibinadamu kama Kilimo, uchomaji wa misiti na kilimo cha kuhamahama.

"Cha msingi, kwa mradi huu mkubwa wa Bwawa, inahitaji kila mmoja kuvilinda vyanzo vya maji na kama tukiweza kupunguza basi tutakuwa tumefanikiwa kwa sehemu kubwa," aliswma Profesa Kashaigili
 
Napenda kujua kama waliopo huko Mbarali na Pande hizo za Iringa wamezuiwa kufanya umwagiliaji!? Na kama ndio Hivyo si njaa itazidi!? Napenda kujua tu
 
Kuna nchi viongozi wanafanya mambo makubwa na hawapigi makelele na kumtaja mtu mmoja maana ninguvu ya wananchi!!!
Sijui bongo nivile tunakula sana maugali mpaka akili zinadumaa???
Kumsifu mtu mmoja Kwa kazi inayofanywa na Kodi za wananchi ni kielelezo cha LOW IQ,SQ na EQ mtawalia
 
Ndugu zangu watanzania,

Serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa mama wa shoka Jasiri imara mzalendo mchapa kazi Hodari komandoo wa kisiasa Na kiongozi muongoza njia mama Samia suluhu Hassani inakwenda kufanikisha uzalishaji wa megawatti 2115 za umeme kupitia Bwawa la mwalimu Nyerere linalokwenda kuanza Uzalishaji huo mwezi January.

Mpaka Sasa na mwezi huu Tayari ujazo wa maji umeshafikia mita 136 Kati ya mita za ujazo wa maji 163 kutoka Usawa wa Bahari zinazotakiwa ili kuanza Uzalishaji huo wa umeme, kukamilika na kuanza kwa uzalishaji wa umeme inakwenda kutimiza Ndoto za Baba wa Taifa chini ya usimamaizi madhubuti wa serikali ya CCM chini ya Rais Samia,Hatua hii inakwenda kumaliza kabisa Tatizo la mgao wa umeme hapa nchini,inakwenda kuwasha umeme mpaka vichakani kuliko na wanyama ili watalii waangalie wanyama wetu mpaka usiku,

Hatua hii ya upatikanaji wa umeme wa uhakika itachochea Biashara nyingi Sana mpaka vijijini,itavutia wawekezaji mbalimbali katika maeneo na secta mbalimbali kuwekeza,itaongeza ajira kwa vijana wengi Sana kwa kufungua biashara zinazotegemea umeme hasa maeneo ya vijijini na pembezoni Kama vile saloon, kuchomelea,mafundi selemala,wauza vinywaji vya baridi,Biashara ya samaki wabichi,Vinywaji baridi,ufunguzi wa gereji maeneo tofauti Tofauti,steshenari ,mashine za kusaga na kukoboa nafaka Kama vile mpunga na mahindi,mashine za kukamulia mafuta ya Alizeti N.k.

Pia hatua hii itachochea mapinduzi ya viwanda mbalimbali kwa kuwa viwanda vinahitaji umeme mwingi na mkubwa,Hivyo upatikanaji wa umeme wa uhakika utawashawishi watanzania wengi na wafanyabiashara au wawekezaji wa kigeni kufungua viwanda hapa nchini na kufanya uzalishaji wa bidhàa kwa gharama nafuu na hivyo kufanya bidhàa nyingi kupatikana kwa wingi,urahisi na kwa Bei nafuu,lakini pia uwepo wa viwanda itachochea uzalishaji wa fursa za ajira kwa vijana,kuongeza mapato kwa serikali pamoja na kuongeza mzunguko wa fedha mitaani.

Kwa hakika Rais Samia na serikali Yake Amedhamiria kwa dhati kabisa katika kuleta mapinduzi ya uchumi hapa nchini kwa maarifa na akili tu pasipo kutumia nguvu na mabavu,Anakwenda kuufanya uchumi wetu uedeleee kuchangamka Zaid na zaidi kutokana na wingi wa shughuli za kiuchumi zitakazo funguliwa mitaani zitakazo chagizwa na uwepo wa umeme wa kutosha na uhakika.

Watanzania wenzangu Nawaombeni Tuendelee kuiunga mkono serikali hii ya CCM ambayo imeonyesha ushupavu na umadhubuti katika kututumikia watanzania kwa moyo wa upendo na uzalendo mkubwa Sana.

Hongera Sana Rais Samia Rais wetu shupavu na Jasiri, kwa ukakamavu wako mkubwa Sana wa kujenga na kukamilisha miradi mikubwa Sana ya kimkakati Kama huu wa umeme,kwa hakika umewaziba midomo waliofikiri hutafanikisha mradi huu,umewathibitishia uimara wako na umadhubuti wako kiuongozi,umewaonyesha kwa vitendo kuwa wewe Ni kiongozi Jasiri na imara usiye yumba Wala kuyumbishwa,usiye teteleka Wala kuteteleshwa, watanzania Tunajivunia uongozi wako na serikali yako inayoaminika na kupendwa na mamillion ya watanzania walio bega kwa bega na wewe,Ndio sababu ya kuona utulivu na Amani iliyo Tamalaki hapa nchini,Ndio maana unaona inaungwa mkono ndani na nje ya Taifa letu.

Watanzania tumeridhishwa na hatua na mikakati ya serikali yako katika kushughulika na kero na changamoto mbalimbali,Tunafurahishwa na ukweli na uwazi wako katika Uendeshaji Wa serikali yetu,Tunafurahishwa na namna unavyotuthamini,kutujali,kutuheshimu,kutusikiliza na kutupenda watanzania pamoja na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa letu,Hongera kwa kujenga umoja wa kitaifa ,Hongera kwa kuliweka Taifa pamoja ,Hongera kwa kuleta Tabasamu na furaha katika mioyo ya watanzania wa makundi yote.Asante

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Sambamba na hilo napenda kusisitiza juu ya zoezi la upandaji wa miti maeneo mbalimbali ya nchi kufidia miti iliyokatwa eneo la mradi. Pia kurejesha mazingira katika hali ya ukijani ili upatikanaji wa maji uwe wa uhakika.
Natoa pongezi kwa wakuu wa wilaya waliofanya upandaji miti kwenye mikoa yao.
 
We jidanganye tu

Unamjua marope wewe?. Subiri excuse mpya atayokuja nayo hautaamini!!

Umewahi sikia kitu inaitwa uchovu wa transmission line?
 
Unakumbuka kwenye uzinduzi wa gesi pale Kinyerezi? Tuliambiwa the same statement.Uhalisia kwenye Dunia yetu huku ya tatu ni mdogo sana maneno mengi,vitendo sifuri
Huu ni uongozi wa Rais Samia Mama mkweli na mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu,Hivyo napenda umwamini Rais wetu na serikali Yake kuwa changamoto ndogo ndogo za kukatika katika kwa umeme zinakwenda kufika kikomo
 
Nape na Makamba wakizitizama hotuba zao kupindi kile wapo bungeni wanadai mradi ungesababisha uharibifu wa mazingira sijui sasa hivi wanajisikiaje,mara sijui bayo anuai,mara miti elfu ngapi inakatwa haya sasa leo Makamba sijui anajisikiaje.

Mwanzoni mradi ulipigwa vita vikwazo vingi mara sijui Crane limefanya nini, mara fedha zinachelewa,wabunge baada ya kupiga kelele wameona aibu.
 
Huu ni uongozi wa Rais Samia Mama mkweli na mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu,Hivyo napenda umwamini Rais wetu na serikali Yake kuwa changamoto ndogo ndogo za kukatika katika kwa umeme zinakwenda kufika kikomo
Hakuna mwanasiasa mwenye sifa hizo Duniani mkuu
 
Kuna nchi viongozi wanafanya mambo makubwa na hawapigi makelele na kumtaja mtu mmoja maana ninguvu ya wananchi!!!
Sijui bongo nivile tunakula sana maugali mpaka akili zinadumaa???
Kumsifu mtu mmoja Kwa kazi inayofanywa na Kodi za wananchi ni kielelezo cha LOW IQ,SQ na EQ mtawalia
Nchi imejaa wajinga na wanafiki wengi.

Hakuna asiyependa umeme wa uhakika lakini ukweli ni kwamba hili bwawa wala siyo suluhisho la tatizo la umeme.

Suala siyo kulijaza maji bwawa mwanzoni bali ni uhakika kuwa bwawa hilo litakuwa na maji mwaka mzima. Fikiria tu kuwa bwawa linahitaji misimu miwili ya mvua ndiyo lijae kwa kiwango cha kuweza kuzalisha umeme. Halafu maji yaliyojaa kwa misimu miwili ya mvua yanatosheleza kuzalisha umeme kwa mwaka mmoja tu. Hivyo ni lazima muda mwingine lifungwe tena kusubiria lijae.

Tunaongelea kilimo cha umwagiliaji. Hii ina maana mito hiyo hiyo inayopeleka maji kwenye bwawa la umeme ndiyo inatarajiwa kutoa maji ya kumwagilia mashamba ya nafaka.

Hekima ilikuwa kuendeleza vyanzo vya umeme visivyotumia maji.
 
Back
Top Bottom