Hakuna jeshi la zimamoto bali ni kikosi cha zimamoto na uokoaji pia uhamiaji sio jeshi bali ni idara ya uhamiaji!Hebu tupitie kwa ufupi aina ya majeshi yetu na majukumu yake ya kila siku
-JWTZ- hili ndio kama jeshi kuu linalihusika na ulinzi na usalama wa mipaka yetu....naweza kusema ndio jeshi mama na mara chache kuonekana mitaani na linapoonekana mitaani kwenye mavazi yao rasmi ujue hali sio shwari sana... (kuna haja ya kuwa na mjadala kwenye jina)
-JPT/TPDF/TP- Hili ni jeshi la polisi Tanzania, ndio jeshi lililozoeleka zaidi kwa wananchi ndio jeshi linalihusika na kushughulika na maisha ya kawaida ya kila siku ya mwananchi! Kuanzia usalama wa ndani, nyaraka mbalimbali, kesi , hukumu vifungo hata misamaha na madawati ya jinsia na kwa sehemu msaada wa kisheria...! Tungeruhusu mijadala ya wazi hili ndio lilipaswa kuitwa Jeshi la wananchi
-JKT- Jeshi la kujenga Taifa , hili ni jeshi la damu changa madhumuni yake ni kuwafundisha vijana wote wanapomaliza elimu ya kidato cha sita nk uzalendo ukakamavu na stadi anuwai kabla ya kuendelea na elimu ya juu....hapa kuna nguvu kazi kubwa sana inapotea bure nguvu kazi ya kujenga taifa katika nyanja mbalimbali kuanzia kilimo ufundi ufugaji mpaka biashara na sayansi na teknolojia... kile kitengo cha SUMA-JKT kama kungekuwa na uhuru wa majadiliano kingepaswa kipelekwe JKT na wanajeshi waachiwe jukumu lao la msingi
-JLMT- Jeshi la mgambo Tanzania, hili ni jeshi ambalo sio rasmi sana likiwa haitofautiani sana na polisi jamii (kitengo kinachoelekea kufutwa awamu hii)haya ni majeshi ya msingi lakini yasiyopewa kipaumbele sana...haya ndio yanajua kila kitu nyumba kwa nyumba mtu kwa mtu na mtaa kwa mtaa...tungekuwa na mijadala huru hili tungelijadili kitaifa ili iwe ndio msingi rasmi wa majeshi yote na kuwe na program maalum zinazohusika na kutambulika kisheria
-Tuna majeshi mengine kama ya zimamoto nk lakini haya hayawezi kuwa sehemu ya mjadala kwakuwa ni vitengo ndani ya jeshi la polisi
Je katiba yetu inatuambia nini kwenye dhima na utayari wa kuwa na mijadala kama hii?
Nawasilisha....!!!
Naona ameanza na Jwtz then akaja na Pt/TpdfNi kitu kile kile tofauti ni lugha tu
TPDF-Tanzania Peoples Defence Forces.
JWTZ-Jeshi La Wananchi Wa Tanzania...
Kuna mahala nilipitia kukuta kama sikoseiMmh hapana japo kwa tafsiri ya kiswahili ni mlinda usalama wa Mali na RAIA
Jamaa alichanganya madesa TPDF ndo JWTZ kwa kiswahili na sio pilisiNaona ameanza na Jwtz then akaja na Pt/Tpdf
Hakuna mantiki yoyote kwenye hiyo ordha. Police ni neno moja linalotaja taaluma mojawapo kama zilivyo taaluma nyingine kama vile mwalimu, daktar n.kKuna mahala nilipitia kukuta kama sikosei
P-people
O-offences
L-liberty
I-investigation
C-criminal
E -enforcement
Kwa haraka haraka sikuangalia viunganishi, sijui kuna ukweli hapo?
Hakuna mantiki yoyote kwenye hiyo ordha. Police ni neno moja linalotaja taaluma mojawapo kama zilivyo taaluma nyingine kama vile mwalimu, daktar n.k
Sijui kwasasa ikoje ila zamani ilikuwa ukimaliza form six ama chuo ndio unaenda JKT na ukitoka huko ndio unaenda chuo kikuu ama kwenye ajira yakoJmn km nitakuwa nimekosea naomveni mnisahihishe,JWTZ,Polisi,magereza na JKT yote hayo in majeshi ya taifa au serikali lkn kwann JKT wakimaliza mafunzo ajira zao huwa km zinasumbua sumbua hv,ukilingabisha na majeshi mengine?
Hapana MP sio cheo mkuu ni kitengo ndani ya jeshi (MP:Military Police) kazi yao ni kusimamia nidhamu ndani ya jeshi..cheo cha chini ni PRIVATE hivyo MP anaweza kuwa wa cheo chochote kile endapo atakuwa amepata mafunzo ya MP.Nadhani hiki ndio cheo cha chini kabisa cha askari au mwanajeshi View attachment 387158