MAMA POROJO
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 4,974
- 785
Je ipo sheria yeyote inayompa askari Polisi, JKT, Magereza, JWTZ, na FFU furusa ya kupata huduma ya usafiri bure katika mabasi yanayofanya biashara katika nchi ya Tanzania? Tabia hii inakwaza wawekezaji wenye uwezo wa kuwekeza katika biashara ya usafirishaji, kama yupo mwenye ushahidi atusaidie tujue kiwango cha madhara ambayo Watanzania wanayapata na wataendelea kuyapata kwa ajili ya kundi la askari ambao kwa sasa ndio wanaolipwa vizuri kuliko watumishi wengine wa uma na bado wanataka huduma ya usafiri wa bure.Kama sheria haipo nini kifanyike sasa kukomesha tabia hii?.
Sio kweli hata kidogo GT
Kwa sababu hawa wanajeshi sio kwamba wanatoa huduma za kujenga madaraja bure, no hawa wanalipwa kila mwezi bila kazi yoyote wanayofanya, na ndo maana zikitokea kazi za dhalula wanafanya, unaweza kuniambia wanafanya kazi gani specific hawa jamaa, wakati wanalipwa kila mwezi
Na kama ndo hivyo kila mtu atataka kusafiri bure, nani kama Mwalimu aliyewafundisha watu, kwanini hasisafiri bure?, na Madaktari je wanaokoa Maisha ya watu, mbona nao hawasafiri bure?
Hakuna mantiki katika hili kuwa askari wasafiri bure kwa sababu zipi?
Kwanza askari wa Tanzania wengi hawana nidhamu na maadili hata kwa wananchi wao, wengi wamekuwa wakiwapiga na kuwaonea wananchi, pili kuna makundi makubwa sana ya ujambazi ambayo na Maaskari wanashiriki.
Hivyo basi mimi sioni kama wao ni muhimu sana kuliko watu wengi mpaka waweze kusafiri bure
In short bado sitaki mwana usalama achelewe kazini kwa sababu hawezi kiupewa usafiri na issue iliopo hapa ni system iliopo ndio mbovu lakini kama ikiwekwa sawa then naamini tusingekuwa na huu mjadala humu
Nisichokipenda ni ma elitists ambao wamejikita kwenye media na sehemu zingine wanatabia za kuwadharau hawa watu ambao wakiambiwa waweke maisha yao onthe line kwa ajili yangu na wewe hawatoquestion hiyo order
suala la nidhani ni dogo sana...hili ni jambo la kutatuliwa kiusalama na mawasialano baina ya raia na wanajeshi lakini siyo mambo ya kuwatukana
Isije kuwa yale yale ya wanajeshi wa UK wanaorudi toka vitani wanatemewa mate na matusi wakivaa magwanda yao kwenye miji ya Peter borough na Leicester
we can do better than hizi cheap shots dhidi ya wanajeshi
ambao kwa sasa ndio wanaolipwa vizuri kuliko watumishi wengine wa uma na bado wanataka huduma ya usafiri wa bure.
Hivi ile tabia ya kujichukulia sheria mikononi mwao wameacha au serikali ilisema nini kuhusu kuwacharaza wale wanaolipa kodi ili wao wawe jeshini?
Hii ni grief waliyonayo moyoni ambayo hawana pa kuitolea ndo maana wanapopata nafasi wanafanya uncounsciously ili kupeleka information kwenye society of their pain
Mshahara wa askari private kabla ya kukatwa kodi ni Tshs 170,000 approx. Na allowance ya chakula kama Tshs 50,000 hivi kwa mwezi! Ofisa wa ngazi ya chini ni sh 350,000 kabla ya kodi!!! Huko ni kulipwa vizuri??? Na Jenerali ana 1.5M, gari + extra allowances whats the difference nafikiri mishahara mizuri ni ya wanasiasa sio wanajeshi. Hawasemi kwa vile ndio maadili yao lakini hawana amani hata kidogo na hawana wa kuwasemea, Hata wabunge wanakwenda maeneo ya wanajeshi wakati wa campaign tu then mbunge gani ulimsikia akitetea maslahi ya wanajeshi? Viongozi wao ni mabilionea, remember Mb..ma with meremeta na Tanzanite + Wa...tara ni mwenye pesa nyingi sana lakini wanajeshi sasa hata kuipata kombati unatoa rushwa!

Inaweza kuwa kweli wanalipwa kidogo, but si kidogo kushinda mwalimu au mfanyakazi mwimgine tu wa serikali. Kinachouma hapa ni kwamba wakarti mtu analipwa 180,000 analipa nauli ya kwenda job, je huyo askari kwa ni i aslipe? Pia wanafuzi hata watoto wa std 1 wanalipa, mbona WAJESHI WASILIPE? Sioni mantiki kabisa
Mshahara wa askari private kabla ya kukatwa kodi ni Tshs 170,000 approx. Na allowance ya chakula kama Tshs 50,000 hivi kwa mwezi! Ofisa wa ngazi ya chini ni sh 350,000 kabla ya kodi!!! Huko ni kulipwa vizuri??? Na Jenerali ana 1.5M, gari + extra allowances whats the difference nafikiri mishahara mizuri ni ya wanasiasa sio wanajeshi. Hawasemi kwa vile ndio maadili yao lakini hawana amani hata kidogo na hawana wa kuwasemea, Hata wabunge wanakwenda maeneo ya wanajeshi wakati wa campaign tu then mbunge gani ulimsikia akitetea maslahi ya wanajeshi? Viongozi wao ni mabilionea, remember Mb..ma with meremeta na Tanzanite + Wa...tara ni mwenye pesa nyingi sana lakini wanajeshi sasa hata kuipata kombati unatoa rushwa!
Kipato kidogo hakiwezi kuhalalisha upate huduma ya kudhulumu biashara za wenzako. Kitendo cha kupata huduma bila malipo ni kitendo cha dhuluma au ni ketendo cha wizi. Hakuna tofauti yoyote na mhalifu au kibaka anayechukua mali ya mtu na kutokomea nayo. Ni kwanini basi kama ni watu wanaositahili kupewa huduma za dezo, lakini wakiwa mahotelini, sokoni, maduka ya dawa na kwenginepo wanalipa? Tatizo ni kuwa wenye magari ya kusafirisha abiria (daladala) hawana umoja. Kwa sababu kama wakiamua kung'ang'ana na maaskari wasiolipa hadi mahakamani ndipo kitaeleweka kuwa kitendo wanachikifanya ni haki yao au ni kitendo cha wizi. Je kitendo cha askari barabarani kushika magari na kudai rushwa pia ni sawa kwa sababu mishahara yao ni midogo. Ni lazima askari waishi kwa kipato chao wanachokipata. Kwa sasa askari wa JWTZ mishahara yao ni mizuri na yalifanyika marekebisho ya pension zao wakati wa awamu ya tatu, kila askari anayestaafu analipwa asilimia 50 ya mshahara wa cheo alichokuwa nacho, kama kutakuwepo na ongezeko la mishahara ya ngazi aliyokuwa nayo. Ongezeko hili pia litakwenda sambamba na pension yake kuongezeka kwa kiwango cha mshahara unaolipwa kwa wakati huo.