Vikosi vya majeshi kutoka nchini Senegal vimethibitisha kuingia katika ardhi ya Gambia katika muda ambao rais mpya Adama Barroe anaapishwa.
Msemaji wa jeshi la Senegal Kanali Abdou Ndiaye ameiambia BBC kwamba vikosi hivyo vimevuka mpaka na kupiga hatua kuelekea katika mji mkuu wa nchi hiyo,Banjul.
Na kusema kwamba vikosi hivyo mpaka sasa havijakabiliana na ukinzani wa aina yoyote ingawa viliweka bayana kwamba vilikuwa vimejizatiti kwa mapigano ikibidi.
Mapema baraza la usalama la Umoja wa mataifa inasemekana kwa siri limekuwa likiunga mkono juhudi za vikosi vya ECOWAS, kuhakikisha kwamba rais Barrow anachukua madaraka kutoka kwa rais aliyemaliza muda wake Yahya Jammeh.
Rais huyo wa zamani wa Gambia,awali aligoma kuachilia madaraka.
Rais wa sasa Adama Barrow ameapishwa leo katika nchini jirani kwenye ubalozi wa Gambia ulioko mjini Dakar nchini Senegal na kufuatiwa na shamra shamra ubalozini hapo.
Mpaka sasa haijafahamika wazi lini lini rais mpya wa Gambia ataweza kurejea nchini mwake na kuchukua hatamu za uongozi kwa mara ya kwanza akiwa rais
Ipo siku watakuja kusalimia tuNgoja tusubiri kesho tuone.. Naomba ECOWAS na huku kwetu wawe wanafika hata kuchungulia tu inatosha
Duuuh...hatari
Hivi mfano raia wakadhurika na hayo majeshi ya ecowas, na mkuu wa majeshi ya gambia kasema hatopigana, itakuwa ni sahihi? Maana hiyo ni kama vita, risasi hailali njaa vitani... Nauliza kitu nusichokijua ili nieleweshwe, ni sawa? Au maamuzi aliyochukua ndio sahihi? Msaada wakuu!!Nimependa sana msimamo wa mkuu wa majeshi wa gambia.
Nataman kungekua na wakuu kama hawa wa majeshi zile nchi ambazo zinaongozwa kidikteta kwamba viongozi mda wao unaisha lakini hawtok madarakani
Anaposema hatapigana anamaanisha kuepusha mapigano. majeshi wenyeji wasiporesist majeshi ya kigeni yatapigana na nani. Kifupi ana busara kwamba acha majeshi ya nje yaungane na ya ndani kulinda usalama na wakati huohuo kumkamata jammeh bila kudhuru RAIA.Hivi mfano raia wakadhurika na hayo majeshi ya ecowas, na mkuu wa majeshi ya gambia kasema hatopigana, itakuwa ni sahihi? Maana hiyo ni kama vita, risasi hailali njaa vitani... Nauliza kitu nusichokijua ili nieleweshwe, ni sawa? Au maamuzi aliyochukua ndio sahihi? Msaada wakuu!!
Tumechoka na njaa tu.tunahela ya kuendea huko?Tanzania nao wajiunge umoja huo nadhani ni poa sana
Habari wakuu....nipo naangalia FRANCE 24 mda huu..! Wanadai majeshi ya Senegal yameingia Gambia,maneno hayo yamesemwa na msemaji wa jeshi...Mkuu wa majeshi wa Gambia yuko pamoja na wafuasi wa Barrow wakishangilia Street
Source :FRANCE 24
Uamuzi.wa mkuu wa majesh ni sahihiHivi mfano raia wakadhurika na hayo majeshi ya ecowas, na mkuu wa majeshi ya gambia kasema hatopigana, itakuwa ni sahihi? Maana hiyo ni kama vita, risasi hailali njaa vitani... Nauliza kitu nusichokijua ili nieleweshwe, ni sawa? Au maamuzi aliyochukua ndio sahihi? Msaada wakuu!!