Majeshi ya Ecowas kuivamia Gambia

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Salaam jf

Jeshi la Senegal limesema kuwa majeshi ya Afrika Magharibi yataingilia suala la Gambia usiku wa kuamkia tarehe ya mwisho wa madaraka ya Rais Yayha Jammeh ambayo ni leo ili akabidhi madaraka kwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanywa mwezi uliopita,Adama Barrow ambaye kwa sasa yuko nchini Senegal..

Vikosi kutoka Senegal vimesogea katika mipaka ya Gambia, Nigeria pia imetuma vikosi vya anga katika eneo hilo.

Senegali imeomba Jumuiya ya Usalama ya Umoja wa Mataifa kushinikiza Umoja wa nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kuchukua hatua za msingi katika kuhakikisha Rais mteule wa Gambia anakabidhiwa madaraka.

Kwa nini Senegal inaongoza Mpango wa Kumng'oa?
Ecowas, Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, iliipa Senegal jukumu hilo kwa sababu taifa hilo linaizunguka Gambia.

Kanali Abdou Ndiaye, msemaji wa jeshi la Senegal, amesema Ecowas iliamua kumuwekea Jammeh mkakati huo ili kujaribu kupata suluhu ya kidiplomasia.

"Mambo yote yako tayari na wanajeshi wa Ecowas wako tayari kuingilia kati baada ya saa sita iwapo hatutapata suluhu ya kidiplomasia kwa mzozo huu wa Gambia,"alisema.

Wanajeshi hao wa Ecowas wanasubiri Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lipitishe azimio la kutumiwa kwa "hatua zozote zile" kusaidia kuondolewa madarakani kwa Be Jammeh. Wanajeshi wote wa Gambia ni takriban 2,500.

Nigeria imesema imetuma ndege za kivita na ndege nyingine za kawaida, pamoja na wanajeshi 200 nchini Senegal. Wanajeshi hao walienda Senegal Jumatano asubuhi.

Meli za kivita za Nigeria pia zimewekwa tayari baharini.Manowari moja iliondoka Lagos Jumanne na itakuwa na jukumu la kuwaokoa raia wa Nigeria walio nchini Gambia.Ghana pia inachangia wanajeshi

Chanzo: BBC
 
Safi saana ila Jemah nae akili hana. Alishindwaje kuagiza matokeo kufutwa na uchaguzi kurudiwa?
 
Majeshi ya muungano wa Afrika Magharibi yataongozwa na Senegal na Nigeria kuivamia Gambia siku moja kabla ya kuapishwa Kwa Rais mpya Adama barrow, hatua hii inafanyika ili kumtoa ikibidi kwa nguvu Rais anaegoma kuondoka Madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu ,

Msemaji wa Jeshi la Senegal Kanali Abdou Ndi'aye amesema wanataka kuhakikisha Rais mteule Adama Barrow anakabidhiwa madaraka kutoka kwa Rais Yahya Jammeh hatua hiyo imekuja baada ya Rais Jammeh kutangaza hali ya hatari ikiwa ni siku moja kabla ya kuachia madaraka,

Aidha majeshi hayo awali yameomba jumuia ya kimataifa kuhakikisha kwamba Rais jammeh anaachia madaraka, tayari majeshi ya anga ya Nigeria na jeshi la Senegal yamesogea mpakani mwa Gambia tayari kwa kuivamia usiku wa leo ili kumshinikiza Yahaya jammeh aondoke
Mpuuzi Jammy, jeshi la watu 2500, poorly trained, poor ammunition apambane na ECOWAS! Hopeless! Kama Qaddafi, Sadam Hussein......
 
Nchi za africa tuheshimu katiba jamani, this is Ao wrong kabisa yani , hata wakiamua kuivamia Gambia sekunde moja tu nchi yenyewe ndogo tu waepushe kumwaga damu kwa lazimaa,

√√ Nigeria kipindi cha nyuma ilipata wakati mgumu sana, kipindi kirefu sana ilikuwa chini ya jeshi na mfumo wao ulikuwa ni wa kimapinduzi na mapinduzi ikawa jadi watu kama ...Maman vataa,,, Shaghali,,,,,,Murtallah muhammded,,, na Gowoni. walipindua na walipinduliwa , yani mapaka Nigeria inakuwa ya Kidemocracia ni karibuni karibuni ilikuwa ni Sani Abacha kama sijakosea
 
Hongera ECOWAS kwa hatua sitahiki. Litakuwa fundisho kwa watu wa aina hii maana wako wengi. Africa mashariki tunashindwa hili kwa vile hakuna umoja thabiti zaidi ya unafiki. Burundi, Rwanda, DRC, (z'bar) kote huko figisu tupu na zinajulikana lkn mmoja akiboronga hili mwingine naye kesho anaiga.
 
nchi za Africa mashariki nako kunataka kuwa kama huko, tungepata jeshi moja la kudhibiti na kutunza democracia tunako elekea mapinduzi yatakuwa hayaepukiki , but sidhani kama kweli Ecowas kweli wanaweza kumdhibiti huyo president
 
...
Wanajeshi hao wa Ecowas wanasubiri Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lipitishe azimio la kutumiwa kwa "hatua zozote zile" kusaidia kuondolewa madarakani kwa Be Jammeh. Wanajeshi wote wa Gambia ni takriban 2,500 ...
Duh! Japo wanasema wingi sio issue bali ubora ila this is too little! Sasa Jameh anatoa wapi jeuri kama jeshi lenyewe ndio hilo.
 
Nchi za africa tuheshimu katiba jamani, this is Ao wrong kabisa yani , hata wakiamua kuivamia Gambia sekunde moja tu nchi yenyewe ndogo tu waepushe kumwaga damu kwa lazimaa,

√√ Nigeria kipindi cha nyuma ilipata wakati mgumu sana, kipindi kirefu sana ilikuwa chini ya jeshi na mfumo wao ulikuwa ni wa kimapinduzi na mapinduzi ikawa jadi watu kama ...Maman vataa,,, Shaghali,,,,,,Murtallah muhammded,,, na Gowoni. walipindua na walipinduliwa , yani mapaka Nigeria inakuwa ya Kidemocracia ni karibuni karibuni ilikuwa ni Sani Abacha kama sijakosea
Iheshimu Katiba ya Nyumbani Kwako Katiba za Nchi za Africa Zishachokwa Hacha Vita Ianze Watie Akili Hao Wang`ang`ania Madaraka.
 
Back
Top Bottom