Majengo ya Morogoro, Nani mjenzi?

Ndugu zangu,

Wiki iliyopita nilikuwa Mji kasoro bahari, a.k.a Moro town. Nilichokiona mjini pale kimenishangaza sana!

Ujenzi tu wa Moro, ni vituko, nyumba nyingi za Moro mjini (Mfano Nanenane & Kihonda) zimejengwa hovyo hovyo tu, utadhani viwanja havikupimwa. Nyumba zenyewe sasa, utadhani mjengaji alishikiwa bunduki wakati akijenga!

Nyumba hazikamiliki, nyumba zimejengwa hovyo hovyo kama magodauni, unakuta jumba kubwa lakini halina shepu, halijakamilika, vyoo sasa, daaaah! Kiufupi ni hovyo hovyo tu...

Sasa nikawa najiuliza;

1. Hizi nyumba mjengaji ni mmoja?

2. Nani anaidhinisha ramani zao. mpaka waanze kujenga?

3. Kwanini mtu ahangaike kujenga lijumba likuuubwa kama hawezi kulimudu gharama za umaliziaji na asijenge kajumba kadogo kazuri?

4. Hivi wakazi wa Moro, hawaendagi miji mingine kama Moshi, Mwanza, Babati, Dsm, Sumbawanga na kadhalika wakajionea watu wanavyojenga nyumba nzuri?

5. Kama wanaona, kwanini hawatamani?

6. Kama wanatamani, kwanini na wao hawaji kujenga mji wao vizuri?

Naomba kuwasilisha!

wewe unatoka mji gani wa Tanzania ambao utofauti wake na morogoro ni mkubwa kisai cha kukufanya uwe na nguvu ya kuiona morogoro ni ya ajabu? Nadhani ulilinganisha moro na Jo'berg then ukaandika meseji yako.
 
Haya je yakoje
 

Attachments

  • 1427997439773.jpg
    1427997439773.jpg
    70.9 KB · Views: 294
Pamoja na kuwa mleta thread ameenda to the extreme lakini kuna ukweli fulani ambao hatuwezi kuupuuzia....

Ninaishi Morogoro na Kuna maeneo mengi mazuri yaliyojengeka kiasi kunitamanisha Nami ninajenga Moro

Tukirudi kwenye ukweli, Nyumba nyingi zinajengwa bila vibali na ukihangaika na vibali wanakushangaa. Ninakumbuka wengi walionishangaa wakati nahangaika na vibali japo nilijua umuhimu wake pamoja na usumbufu wa manispaa (michoro na umiliki havikuwa na tatizo lakini ilichukua miezi karibu mitano mpaka nilipotishia kwenda kushtaki kwa Mkurugenzi)

Lakini pia Kuna kukosa umakini katika utoaji Vibali....Kama eneo linalotolewa vibali limeanza kujengwa inapaswa kabla ya kutoa kibali Manispaa ijiridhishe kuona muonekano wa jengo husika unaendana na ujenzi ambao tayari upo. Mfano eneo ninalopanga sasa Nyumba zimejengwa kwa vibali lakini zilivyopishana mpaka zinakera...hii imegeukia kule, hii huku yaani shaghala baghala...

Nikawaza kwa nini gharama zinazolipwa kwa vibali zisitumike kujiridhisha mkao wa jengo site (site plan) kabla kibali kutolewa?
 
Kina Mkude wao wamekalia ubishi tu usio na msingi katika masuala ya ujenzi wamemwachia kila kitu mbunge wao Aboud na familia yake.
 
Duhh mshkaji muongo sana sema unataka kufafanua kwa watu kuwa umefika morogoro.
 
Morogoro sijui wamelogwaa? Mji upo karibu na jiji kubwa lakini umedumaa kupitiliza. Pamekaa kushoto sana, niliishi kwa kipindi kifupi mwaka 2013, sikutamani kuendelea ishi katika mji huo.
Pamoja na kuwa wamezungukwa na vyanzo vya maji, maji yao ni machafu yameja Typhoid.
Kitu pekee kilicho endelea Moro ni ma bar na Band za muziki., kwani kila Bar ina live Band, VIP lounge ....
 
Ila tuache utani wakuu Moro ni mji wenye jina kubwa tokea kitambo sana lakini jina lake halifanani na jinsi mji ulivyo,kwanza barabara za town aibu tupu hata kumtembeza mgeni,utafikiri watu wa mji huu hawachangii kodi!,ukija kwenye soko kuu la Mkoa mama weeeee,bayaaaaaa na manispaa wapo tu,Mbunge mwenyewe Aziz Abood ndio mafuta kabisa,badala ya kutetea mambo ya msingi Bungeni yeye anadhani kutoa mabasi ya bure kuzikia ndicho kilichompeleka Bungeni,yaani huu Mkoa ni majanga tupu,mzunguruko wa fedha ni mdogo sana,unaweza ukamwomba mshkaji wako akuazime laki tu,atakwambia hana,jamani tusibweteke sisi wakazi wa Moro,Mji wetu bado sana,visehemu vya kula bata vyenyewe vya kuhesabika,eti samaki samaki na viber,vina majina makuubwa lakini hakuna lolote pa kawaida tu
 
Hili ndio litakuwa jengo kubwa kuu Morogoro mjini eti kama Ubungo Plaza
 

Attachments

  • 1428004648652.jpg
    1428004648652.jpg
    124.9 KB · Views: 221
Mtoa mada hujatembea moro kbs, nenda forest, kilakala bong'ola, visole, nugutu,mazimbu, kihonda yoote, area 5 area 6, kola, Kuhusu nyumba za zaman mbona iringa kati kat ya mji unakuta nyumbq ya udongo.Tanga pia mtwara tatizo wenyewe hawatak kuuza mkuu yataisha hayo
 
Tusidanganyane hapa, Apart from Dodoma na Sumbawanga miji mingne yoote inayobaki ni kama vile hakuna Mipango miji
 
Back
Top Bottom